Naombeni ushauri kwa huyu demu jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni ushauri kwa huyu demu jamani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jt jr, Feb 3, 2012.

 1. Jt jr

  Jt jr Senior Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 182
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jamani kuna msichana nilimtongoza nikiwa shule ya msingi lakini hatukufika mwafaka kwa kuwa tulivyomaliza shule kila mtu aliendelea na secondary na hatukuwa na mawasiliano kila mtu akawa na issue zake. Baadae alitafuta namba yangu ya cm nikiwa form5 nikawa naye kwa mda lakini baadae tuliachana kwa kile alichodai kuwa simjali, ila ni kwa sababu ya shule. Alirudia kunitafuta nilipomaliza form6 tukaka tukaongea mengi akaniweka wazi kuwa ana mtoto teyari na aliyezaa nae mtu mwenye mke, anadai ilitokea bahati mbaya na mtoto alichukuliwa na babake, nikiwa chuoni amenitafuta tena tukawa tunachart akanielezea stori zake zote na wanaume aliokuwa nao yeye akadai ilikuwa ni harakati ya kumtafuta anayemfaa maishani. kaniambia ananipenda, na Akaahidi hatarudia ujinga wake wa nyuma nikambadilishia na laini ya cm, mpaka sasa tunapanga tuje kuoana. Ila najiuliza itakuwaje?na huku teyari ana mtoto ingawa alichukuliwa na baba yake, kitu kingine nalingana naye umri. Naombeni ushauri wenu wanajamii km ni busara kuwa nae.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Piga chini huyo sio mwaminifu, unajua mahawala huwa hawaachani katu!!
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Unavyojieleza inaelekea kama wewe bado ni kijana. Kwa nini usitafute kitu brand new badala ya kukaa unang'ang'ana na Used? Tumia vizuri ujana wako.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mmh huu si ushauri mzuri bwana mkubwa,
  mimi nakushauli kama umelidhika naye muoe huyo, kwani hayo mengine ni mapito tuu na ukweli ameshakuambia angeweza kukuficha pia, nadhani huyo ndo mkeo umli si kigezo bwana.
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Usikilize Moyo wako.
   
 6. rweyy

  rweyy Senior Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  dogo kama unampenda kutoka moyoni bc huyo ndo mwanamke wa kuoa
   
 7. D

  DOOKY JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Majibu unayomwenyewe. Kama roho ina wasiwasi means hakufai achana naye
   
 8. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  masuala ya mapenzi ndugu wakati mwingine hayahitaji ushauri! Lakini kwa sababu hapa ni mahala pake ngoja nikudadavulie ninachoweza!
  1.kulingana na maelezo yako huyo binti unampenda sana kwa hio mie sioni Tatizo liko wapi kama utaamua kumuoa! Suala la yeye ana mtoto si hoja bali ni maamuzi yenu wawili ndo yatakayowapa dira na dhamira ya kuoana!
  2.uaminifu! Hapa ndo kuna tatizo! Ingawa huyo binti ana mtoto mmoja inawezekana akawa ndo mwaminifu kuliko hata wewe! Inawezekana wewe una watoto wengine tayari au umisha tundika watoto wa watu mimba ila kwako wewe huoni ni tatizo bali utaangalia huyo unaemuoa tu!
  3.kujali! Inawezekana ni kweli ulikuwa humjali sana binti kwa sababu ulikuwa na mihangaiko na masomo! Binti Amejaribu kupenda wengine imeshindikana hivo moyo wake uko kwako mpokee!
  Muhimu:::kumbuka hakuna mtu asie na mapungufu! Cha muhimu ni kukubaliana ni jinsi gani mtarekebisha makosa na kuanza maisha ya me na ke!
  Kila la heri!
  Kumbuka!!! Mapenzi hayalazimishwi......
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  sahau yaliyopita, mtoto sio tija kwani wengi wao wanawakojoa chooni au wanatubambika ambao sio wetu hivyo kama mmependana na tabia zinaridhisha muoe tu.
   
 10. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,073
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  ukishakua na doubt na partner wako that means huna uhakuka na maamuzi ya moyo wako,mimi nakushauri usiwe na haraka hebu subiri kidogo mpaka moyo wako utakaporidhia pasip kushauriwa na mtu au kuambiwa
   
 11. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa uliosema, na mimi kwa kuwa napenda tende basi nakupa point hapa.
   
 12. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kama mmeshaanza kufanya mipango ya kuoana ina maana tayari kimeshaeleweka na kila mmoja ameridhika na mwenzake, so huna haja ya kuwa na kigugumizi - chukua mzigo jumla huo mzee, umri sio big deal
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Na kweli! Jinsi anavyopata shida kukusahau ndivyo atakavyopata shida kumsahaui baba mtoto na wengine waliowahi kushika kijiti! Kimbia ufe aisee
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Used ndio sera za nchi, hauoni serikali imepitisha hiyo kitu!,
  Brandnew. Mmmmh unaweza kushubiri mpaka ukawa sugar daddy.
   
Loading...