Keyzer Soze
Member
- Dec 30, 2016
- 27
- 22
Habarini wana jamvi? Nina mwaka na nusu sasa tangu nifunge ndoa na sasa tuna mtoto wa kiume ana miezi mitatu,sasa kabla hatujapata mtoto mke wangu alikuwa anabehave kama malaika vile kitu utakachomwelekeza anakuelewa poa sana na sehemu ambayo anaona amekosea atarud chini yanaisha, sasa issue imekuja baada ya kupata mtoto cuz kipindi cha mimba alikuwa na wivu uliopitiliza tofauti na mwanzo,mpaka nkahisi anajifanyisha muda mwingine na ugomvi mkubwa ulikuwa kuhusu simu ambayo mwanzoni alikuwa anaishika lakini anabehave anapokuwa nayo na evidence zote ambazo nlikuwa naona zitamkwaza nafuta mapema tu,lakini sasa hv imefikia mpaka nambadilishia password basi hapo atatuna wiki nzima, nikimwonesha napo inakuwa tabu anaweza kuanzisha chat na mtu akijifanya ni mm saa nyingine hata wale watu wangu wa msingi akimaliza anafuta (hili nilithibitishiwa na watu wanne tofauti like jana mbona sikuelewa unaongelea nn! Nauliza jana tulichat kwan, ndio mtu anakuonesha text zako ambazo katuma wife), na katabia kingine utakuta keshajiweka dp wakati na yeye anasimu yake,na sio kama simuwekagi muda mwingine unakuta anaweka picha like kama za kichokozi na status za kimbea, anabaki anasikilizia kuangalia kwenye cm yake kama ntabadilisha dp yangu,nikibadili mzozo na juzi kilichoniboa kaanzisha chati na kiongozi wangu ofisini ambae namuheshimu sana kwanza kanizidi umri,na hizo chat yeye anaweza anzisha na namba yyte akijisikia yule mother alihisi sio mimi baada ya siku kadhaa akaniita akanambia na kunionesha sms, ikabidi niwe mpole nimwambie hizi kasumba za wife,niliporudi nkamwelezea alichokifanya kwamba hakijanipendeza na nilishawahi kumuonya cha kushangaza basi kajinunisha,huyo mtoto ndio anatumika kama kigezo hapo ntanyimwa hata kumgusa,basi ikabidi niwe mpole,baada ya muda naangalia status yake kaandika "Siui mende kwa nyundo" yani niliona moja kwa moja unanihusu na anajifanyisha makusudi.
Naombeni ushauri wenu ndugu zanguni yani home pamekuwa si sehemu salama ya kuwahi kurud ukitoka kazini.
Naombeni ushauri wenu ndugu zanguni yani home pamekuwa si sehemu salama ya kuwahi kurud ukitoka kazini.