Wapendwa samahani sana kwa usumbufu,
Nina kitu ambacho kwa kweli kinaniumiza moyo wangu sana, sisi kwetu tumezaliwa wawili na wote ni wasichana, dada yangu ni mkubwa kwangu kwa miaka saba hajaolewa na kwa kweli sijawahi kuona yuko na mwanaume ambaye wanadumu kwa muda hata kwa wiki mbili.
Akiwa na mtu yeye ni mtu wa kumfokea mwanaume na kumtukana hivyo ni dada mwenye kazi nuzri msomi kiasi ila tatizo lake ni hilo.
Shida yangu kubwa iliyonifanya niilete hapa kila nikipata mchumba akija nyumbani kujitambulisha dada yangu anadai ni mpenzi wake wa zamani na maneno hayo anawaeleza wazazi hivyo yule mwanaume hawezi kukubaliwa kuendelea na mimi.
Mara ya kwanza nilijua kweli huyo kaka hakulalamika akaondoka zake ni muda mrefu sana, nikapata mwingine dada akadai hivyo nina amini kwa kuwa tanzania kubwa.
Cha kushangaza nikapata mwanaume wa nchi nyingine nimemleta Tanzania kwa ajili ya kujitambulisha dada yangu baada ya muda akadai yule baba atembea nae kipindi hiki nilichokuja nae Tanzania.Kiukweli niliumia sana.
Yule Mjapan akatuona sisi washenzi akaondoka zake yamebaki mawasiliano ya kawaida tuu. Mungu kanikumbuka tena nimepata jamaa mwingine, baba akashauri tupange tarehe ambayo dada hayupo, na kweli kila kitu kilienda sawa.
Harusi yangu inakaribia sana na mpaka sasa dada yangu hawajawahi kuonana na mchumba wangu huyu mpya na hajapata uhakika kama kweli nina mchumba kwani hata pete ya uchumba sivai kwa kumuogopa yeye.
Naomba ushauri je! nimweleze ukweli dada kuwa nina mchumba ila tamuona siku ya harusi?
Au nimweleze mchumba tabia za dada ili hata likitokea awe anajua?
Baba zangu wadogo wanashauri asiambiwe kitu na siku ya harusi astukizwe tuu kwani hakutakuwa na sherehe kubwa ni lunch tuu na vinywaji.
Asanteni nina imani mmenielewa.
Nisaidieni