Naombeni ushauri kuhusu masuala ya miradhi

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,438
2,000
Kwa ufupi
Kuna binti aliolewa na jamaa mmoja toka 2015. Mwishoni mwa mwaka jana ikatokea mtafaruku kati yao wakatengana toka mwishoni mwa mwaka jana mpaka hivi karibuni.

Mtafaruku ulisababishwa na jamaa kuishi na mke mwingine kinyemela wakati wakiwa kwenye mtafaruku.

Kutokana na kutokuelewana huko wakatengana bila kupeana talaka,huku makiwa na watoto wawili. Kumbuka kwamba wote walikuwa wafanyakazi hivyo walikuwa na mchango katika kutafuta mali za familia.Jamaa akaanza mahusino na mwanamke mwingine toka mwishoni ambaye inaonekana alifunga naye ndoa kinyemela.

Bahati mbaya jamaa amefariki juzi kati na kuacha watoto watatu. Wawili wa binti aliyetengana naye na mmoja wa binti aliyemuoa kinyemela.

Napenda kufahamu mambo kadhaa kisheria na kimantiki juu ya haki ya huyu binti aliyetengana naye

1. Binti huyu ni mke halali wa marehemu?
2. Ni ipi haki ya huyu binti katika miradhi
 
lossoJR

JF-Expert Member
Oct 11, 2012
2,672
2,000
We ndio basha wa huyo mzazi wa kwanza nini unataka kujua mnanufaika vipi na mali za marehemu, pambaneni na hali zenu
 
Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,288
2,000
Swali lako la kwanza likijibika ndiyo itakuwa rahisi kujibu swali la pili. Na ili kujua kuwa bado ni mke halali au la kuna vitu inatakiwa tujiulize. Je walifunga ndoa rasmi au siyo rasmi? Ndoa rasmi inayotambulika ni ile inayofungwa msikitini, kanisani, bomani au inafungwa kwa viongozi wa kimila na lazima kuwepo na cheti cha ndoa. Ndoa hii inafuata taratibu zote ikiwemo notice ya siku 21 kabla ya ndoa. Hii ndiyo ndoa rasmi. Na kama walifunga ndoa rasmi kwa mujibu wa maelezo yangu hapo juu basi huyo bado ni mke halali wa marehemu kwa sababu mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa halali ni mahakama tu kwa kuidhinisha talaka na si vinginevyo.

Kama hawakufunga ndoa rasmi basi huyo dada hawezi kuwa mke halali wa marehemu hata kwa dawa. And mind you sheria mbali na ndoa rasmi ina kitu kinaitwa presumption of marriage kwa mwanamke na mwanaume walioishi kama mume na mke chini ya dali moja kwa muda usiopungua miaka 2 nao huwa presumed kama wanandoa. Lakini kwa maelezo yako ni kwamba walioana 2015 na wakatengana mwaka jana 2016 kwa hiyo wana mwaka mmoja tu hawajafikisha 2 years hawawezi kuwa mume na mke kama hawajafunga ndoa rasmi!
 
Mkuu asante kwa maelezo mazuri

Hawa walifunga ndoa halali ya kanisani. Kama nilivyoeleza awali,wote walikuwa wafanyakazi. Kwa hiyo mali ni mchango wa kila mmoja japo kama unavyojua hamuwezi kuwa 50/50

Huyu dada amenieleza kuwa kuna uwezekano mumewe alifunga ndoa bomani na binti aliyesababisha kutengana.
 
Kama walifunga ndoa kanisani na hamna talaka iliyotolewa na mahakama basi ndoa yao bado halali na ndoa aliyofunga baadaye marehemu (subsequent marriage) ni batili kwa mujibu wa sheria. Hivyo huyo dada ana haki ya kurithi mali za mumewe
 
OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,438
2,000
Kama walifunga ndoa kanisani na hamna talaka iliyotolewa na mahakama basi ndoa yao bado halali na ndoa aliyofunga baadaye marehemu (subsequent marriage) ni batili kwa mujibu wa sheria. Hivyo huyo dada ana haki ya kurithi mali za mumewe
Nashukuru kwa tips kaka
 
666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,473
2,000
Well, mkuu Okwi, yule mwanamke wa kwanza ndio mke halali wa marehemu na kama ulivyodai walifunga ndoa mwaka 2015 basi kisheria ndoa yao hata mahakama isingeweza kuivunja kwakua wakat wanaachana by then hawakua ata wamezidi miaka miwili, kama sheria ya ndoa inavyoagiza ndoa kuvunjwa endapo itatua imetimiza angalau miaka miwili, sasa point hapa ni kuthibitishia uhalali wa ndoa yenyewe hio ya 2015, na nimeona umegusia jinsi walivyochuma mali hao wanandoa wawili, na hili mbele ya macho ya sheria basi ni haki kwa asilimia 99 ya uyo mwanamke walioana kua ndio mrithi na mmiliki wa mali izo zilizo achwa na marehemu.

Kisheria huyu kimada hana haki zozote zile kama mwandan wa marehem, na walikua wakiishi kinyemela tu kwa muda wote huo aliokua anaishi na mbaya zaidi alikua anatambua kua marehem alikua ameoa (japo hatujajua marehem na huyo mwanamke wa kwanza mwaka 2015 walifunga ndoa ya namna gani, je ya kikristo au?), so mtoto uyu wa kimada wa tatu analindwa na sheria ya watoto ya mwaka 2009 yeye ana haki ya kurithi mali za baba yake.

Mwambie uyo dada aitishe/kuudhuria kikao cha wanandugu wa mume kitakacho keti kupendekeza msimamiaji wa mirathi, mwambie ata wasipomchagua yeye baasi acheke kwa dharau tu aje aende kufungua kesi ya mirathi na hasa wale wakichaguana na kumnyima nafasi, no way out et hatakosa haki zake, thubutu, sheria zetu zimefanyiwa marekebisho kadhaa wa kadhaa ambayo yanawafavor sana wanawake, na huyu atapata haki zake mchana kweupe bila tabu yoyote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom