Naombeni ushauri kuhusu biashara ya daladala

Yote waliyosema wadau hapo juu yana maana. Na kuna mengi zaidi unapaswa kuyafahamu kuhusu hii biashara. Ingawaje ya msingi ni machache sana na ukikosea hapo ndo linakuja neno "PASUA KICHWA". Kwa ufupi ni biashara nzuri na mimi binafsi naifanya. Nitarudi baadae kidogo kukupa dondoo.

Update:

Mimi binafsi niliingia katika biashara ya usafirishaji (daladala) kutokana na kuwa na hobby nayo. Niliamini kila kitu nitakijua mbele kwa mbele nikiwa ndani tayari kwasababu kila niliojaribu kuwadadisi kuhusu biashara hii walinikatisha tamaa na wachache walininia moyo. Nikaona isiwe tabu, acha niingie mwenyewe nijionee. Nilipata elimu ya kutosha na nikafikia uamuzi wa kwenda kufanya practical. Nilinunua gari yangu ya kwanza (hiace) kwa kuagiza mwenyewe direct toka Japan na nikazama barabarani. Kufika barabarani ikawa kama ndo nimeanza shule kwani kinachozungumzwa na kinachoendelea kiuhalisia ni vitu viwili tofauti. Baada ya miezi kama sita nikawa nimehitimu kozi na kuweka misingi ya kusonga mbele na nilimudu, huu mwaka wa nne.

Zingatia haya:

1. Nunua gari kwa kuagiza mwenyewe toka Japan, usinunue kwa mtu, hatakama ni nusu ya bei ya kuagiza. Zingatia gari nzuri na pia kulingana na malengo yako kama ni ya muda mfupi au mrefu. Ukiwa na gari nzuri na utunzaji mzuri, garage utakuwa unapasikia tuu.

2. Kuwa konda katika gari yako ya kwanza au kuwa dereva. Utajua ulaji mafuta, wastani wa umbali inaotembea kwa siku, hela inayolaza kwa siku na barabara ilivyo.

3. Tokea ikiwa mpya mikononi mwako, usiruhusu fundi yeyote aifanyie service au kurekebisha chochote zaidi ya mmoja unayemwamini na utakayeingia mkataba nae kwa kumlipa kwa mwezi hatakama gari haijaenda garage.

4. Hela inayopatikana igawe mara 3 katika uwiano wa 2:3:5 kama unataka ufikie malengo ndani ya muda mfupi. Huo uwiano ni Mshahara wako, Matengenezo, Uchakavu wa gari. Mfano; Kwa siku kama gari inalaza 100,000tsh; ukitenga 20,000tsh kama Mshahara wako, 30,000tsh kama Matengenezo na 50,000 uchakavu wa gari huo ni uwiano wa 2:3:5

5. Tafsiri ya gharama za uchakavu iko hivi: Gari kama ilikugharimu 30,000,000tsh kuinunua hadi kuiweka barabarani, basi ukitunza hela ya uchakavu 50,000 kila siku ambayo gari imefanya kazi, utawezakuwa umetunza 30,000,000 ndani ya miaka miwili. Hela hiyo itakuwezesha kununua nyingine zikawa mbili. Ila kama una majukumu mengi na unaona mshahara wa 20,000 kwa siku haukutoshi, basi weka malengo yako ndani ya muda mrefu kidogo ila isizidi miaka mitatu. Hapo utaongeza mshahara na kupunguza uchakavu. Mfano uwiano wa (4:3:3). Mshahara 40,000tsh, matengenezo(uendeshaji) 30,000 na uchakavu 30,000tsh. Baada ya takribani miaka mitatu utakuwa umeweza kurudisha hela uliyonunulia na ukaagiza gari nyingine.

6. Hela ya uchakavu wa gari nakushauri uitunze katika dola na siyo tsh. Fungua akaunti ya dola na uwe unatunza humo. Ukiwa na tsh, nenda kanunue dola na u deposit katika hiyo akaunti.

7. Matumizi yako yasizidi mshahara wako, labda kama umeingiza ziada au umekopa dola ktk akaunti ya gari.

8. Hela ya matengenezo itunze kivyake na ya uchakavu kivyake*. Hapa kwenye uchakavu ndipo wengi huwa tunakosea na matokeo yake unakuta mtu ameanza biashara vizuri na gari nzuri ila mwisho wa siku miaka inapita na gari imechakaa na hawezi hata kununua nyingine hadi anaiegesha juu ya mawe au kila siku kushinda garage.

9. Hela ya matengenezo iheshimiwe na gari ihudumiwe kwa fungu hilo na siivinginevyo. Hii inajumuisha gharama zote za uendeshaji wa biashara yako kama vile malipo ya fundi kwa mwezi, karatasi, vibali, vipuri, oil, filters, brake pads, brake shoes, matairi etc.

10. Dereva mlipe kwa wiki. Mimi madereva wangu huwa wanafanya kazi siku 5 kwa wiki(mfano J3-Ijumaa), kisha siku ya sita ni yake. Konda analipwa kwa siku na dereva. Siku ya saba huwa ni off ambayo hutumika kupeleka gari service kama inahitajika au kama haihitajiki, basi dereva afanye kazi kama anajisikia kwa kiasi mtakachokubaliana akuletee kwa siku hiyo. Gari ya abiria servisse siyo mpaka iharibike, ni pamoja na kuchekiwa mifumo ya kiusalama hasa braking system, matairi, suspension na steering, bila kusahau mfumo wa umeme unaojumuisha taa zote na indicators pamoja na honi. Ajali nyingi chanzo huwa ni hivyo vitu ukiondoa uzembe wa dereva. Pia kucheki level ya fluids kama engine oil, gear box oil, differential, coolant/maji system. Fundi si unamlipa? Peleka gari anytime. Tena atatengeneza vizuri usirudi rudi garage.

11. Weka GPS CarTrack kwenye gari yako, itakusaidia kui monitor popote pale ulipo kupitia simu yako ya mkononi na hivyo dereva hawezi na hatathubutu kukudanganya chochote maana unaiona ilipo na kama inatembea pia unaona ikisogea na pia eneo alipo.

Nilianzaga na daladala moja, na nikajiwekea huo utaratibu, sasahivi zipo kadhaa na ninauwezo wa kuongeza moja au zaidi kila mwaka. Mwanzo ndo huwa mgumu, ila zikishakuwa mbili, makusanyo yanakuwa mara mbili na zikiwa tatu hivyo hivyo yanaongezeka huku gari ya kwanza ikiwa imechoka hivyo unamsukumia mtu anayehitaji kisha unajazia unaagiza mpya. Ilimradi uwe na nidhamu ya pesa na uichukulie kama ajira yako.

Cc @
Investor I
POINTS TAKEN.......
 
Kama dereva/konda ni wewe mwenyewe basi hakuna matata...biashara yoyote ile hata kama ni kuuza karanga inabidi uwepo wewe mwenyewe karibu...changamoto ndogo ndogo hazikosekani...
 
Mkuu nimepata elimu kubwa sana
 
Back
Top Bottom