Naombeni ushauri katika hili (mtaji wa 5.M bishara ya duka la nguo)

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
887
Wakuu, mimi nina mtaji wa 4 millions (Million nne). Kwa sasa nipo Mwanza lakini nilikua na mpango wa kwenda Dar kuanza kujitafta rasmi kwaajiri ya maisha yangu, na nina lengo la kufanya biashara ya duka la nguo za kike na kiume huko Dar,

Dar nina connection na wenyeji wangu wanafanya hii biashara kwenye soko la Kaliakoo lakini mimi nlkua nataka hii biashara niifanyie Tabata au Sinza, sehemu hizo mbili, moja wapo frame nzuri ya biashara ikipatikana ntaenda kufungua duka hilo.

Je, malengo yangu yako sawa, naombeni ushauri wenu wana JF, kuhusu familia mim nipo single sina mke wala mtoto, na nikifika Dar ntapanga chumba cha kuishi.

Naombeni ushauri kwa wale wenyeji wa Tabata na Sinza.
 
Dar kwa moto sana. Nakushauri tafuta sukari hata tani 2 iyo pesa inatosha sana. Njoo burundi kuna uhaba wa sukari kuliko maelezo. Kiasi kwamba ukinunua maziwa kukuwekea sukari itabidi uongeze pesa. Nikuhakikishie itagombaniwa kama danadana na siku 3 utakua umeuza yote. Isipotoka nilaumiwe mimi.

Nguo kwakweli kila mtu anauza nguo saivi.
 

Hii biashara sina experience nayo, labda unipe maelezo zaid
 
Hiyo 5m kwa Sinza na Tabata haitoshi. Nakushauri nenda Kariakoo nunua mzigo wa nguo zinazometameta (glittering) pamoja na kofia kisha peleka huko Mwanza zitanunulika. Wasukuma huwaambii kitu kwa nguo za kuwakawaka. Changanya na sendo za bei rahisi zisizozidi tsh 3000 bei ya kununulia. Wewe utauza kuanzia 5000. Kama hiyo huwezi chukua mzigo wa plain Tshirts za bei rahisi (Tsh 5000 - 6000) kisha kauze huko Mwanza kwa Tsh 9000 hadi 12000. Wanunuzi ni wengi wanaoprint.
 
Kuna kitu nimeona juzi hapo Mwanza Nyamhongolo pale ng'ambo ya stendi mpya.
Tafuta eneo pale, weka duka la maji ya kunywa jumla na reja, soda jumla na reja, tishu jumla na reja, biskut, pipi, jojo na vitu kama hizo.
Huna haja ya kukimbilia Dar, wetuliza fuvu vizuri hapo nilipo kuelekeza utaona kitu cha tofauti na manufaa ya badae. Ile stendi imeanza kukua na soon itachangamka
 

Sasa hyo stend unayoiongelea tayari imeshaondolewa, sahivi imefunguliwa ile mpya iliyojengwa na Magufuli,
 
Uhaba wa bidhaa ktk nchi nzima hua taifa husika linatatua haraka hiyo shida, ukimwambia hayo ataleta Sukari na akute tayari Serikali imeshashusha mzigo wa kutosha na aishie kupata hasara
 
4mil kwa dar si you mtaji. anzia hukohuko kwanza ukishapandisha mtaji ndiyo uwe na mawazo ya kuhamia dar. hiyo 4mil kwa dar ni mtaji wa biashara ya kwenye kikapu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…