Dada husife imani kiasi hicho;
Lea mwanao, muombe Mungu mwanaume wako anakuja. .
Utakayempenda, utakayemthamini na mtajenga maisha yenu vizuri tu kwa kidogo mtakachojaliwa
Nina ndugu zangu mmoja kaolewa juzi tu na 36 mwingine aliolewaga name 40. .
Mungu yu Mwema, akupe hitaji la moyo wako na Akutangulie ufanye chaguzi lililo sahihi
Dada sijui nianzie wapi..... Labda nianze kwa maswali
1. Hisia zipi unazotaka ziwepo baina yenu huku Mna mwezi mmoja tu?!
2. Jamaa ana haraka na umetoa sababu ya haraka yake kuwa ana watoto. Huoni kuwa haraka yake ni "justifiable"?
3. Kwanini unataka ndoa?
4. Kipi ni bora kwako hisia au kuwa na mtu ambaye ni committed?
5. Kwa umri wako sio muda wa kutafuta hisia, na kuweka vigezo vingi kwa mwanaume. Upo tayari kubeba majukumu ya kuwa mama wa watoto watatu?
6.Kwa sasa hao watoto wanaishi wapi?!
7. Je umeshazungumza na jamaa kuhusu mtaishi wapi baada ya ndoa?!
Mwisho, ndoa nyingi watu wanaishi ili maisha yaende. Ukitafuta hisia kwa kweli mtu anaweza kukupa hizo hisia lakini baada ya miezi kadhaa ukajuta.
Miaka 30 umri umeenda ila kama ungekuwa huna mtoto. Kwakuwa una mtoto huna hasra saana chakufanya tuliza akili mwambie asubiri kidogo mjenge urafiki ndipo muoane usikudupuke ndugu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.