Naombeni ushauri juu ya hili tafadhali

Naombeni ushauri juu ya hili tafadhali

Milale

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
494
Reaction score
189
Habari za majukumu wanaJF.

Naandika uzi huu ikiwa ni saa kumi na robo za usiku, nimewaza na kuwazua ila hili naona limenizidi uwezo na nimeshindwa kulitatua.

Jambo hili sikupenda kuliweka hapa jf ila imebidi niliweke huenda nikapata msaada zaidi na kujua cha kufanya.

Baba na mama walibahatika kupata mtoto mmoja tu wa kiume ambaye ni mimi.
Familia yetu hatukuwa na maisha mazuri tulikuwa maisha duni sana. Baba alikuwa mtu wa pombe na wanawake sana, pia ilikuwa haiwezi kupita wiki bila mama kupigwa.

Basi matatizo ya wazazi kutoelewana katika familia yetu yaliendelea yaliyopelekea kuacha shule nikiwa kidato cha pili mwaka 2008》
Baada ya hapo nilitoka nyumbani na kuja jijini kutafuta maisha.

Ghafla nae mama wakaachana na baba na nilipomuuliza mama sababu ya kuachana alinijibu kuwa asingeweza kuondoka na kuniacha pekee yangu kwa baba nikiwa bado mdogo. Ila kwa vile umri wangu umesogea sogea na nimejitambua tiyari, ana haki ya kuondoka.

Basi mama akawa mkoa mwingine, baba mkoa mwingine pia mimi mkoa mwingine.

Ila wakati niko jijini sikuwa nawasiliana kabisa na baba yangu nikikumbuka mateso yake kwa mama na kwangu pia yaliyopekea mimi kuacha shule licha ya kuwa nilikuwa nashika namba moja kila mtihani na mtihani wa darasa la saba nikishika namba mbili kimkoa enzi nikiwa shule ya msingi, kifupi niliongoza darasa kuanzia darasa la 3 mpaka 7.

Wakati nikisota jijini nikawa nawaza kabsa huenda yule si baba yangu mzazi.

Nifupishe stori

2015 baba maisha yake yalianza kubadilika na kuanza kuwa mazuri ila sikuwa nikijali kabsa japo nilikuwa napigika mtaani sikuwa na habari juu ya maisha yake maana niliona kuwa maisha yangu kuwa magumu yeye ndo chanzo.

Ghafla mwaka 2016 mawasiliano yangu na yake yalianza kurejea na kuanza kuniomba nimuombee msamaha kwa mama arudi nyumbani. Hapo tiyari alikuwa na pesa ya kutosha baada ya kujiingiza katika siasa na kupata cheo fulani akaniahidi kunijengea nyumba DSM au popote pale nitakapotaka endapo nitamshawishi mama arudi home.

Ila sikuwa namuelewa kabsa nilikuwa namsikiliza yanaishia pale nilihisi kuwa hata angenipa dunia nisingeweza, maana pia maisha yangu hapo yalikuwa yameanza kuwa na mwanga japo haikuwa sana.

Ghafla alianza kunitumia pesa mara kwa mara, na pesa yake ya kwanza ilikuwa miliono tano. Kulingana na pesa alizokuwa ananitumia nilijikuta nasahau yote na mawasiliano yakaanza kurejea taratibu na tukawa marafiki mpaka sasa.

Ila kuanzia kipindi hicho amekuwa akinibembeleza sana nimuombee msamaha kwa mama arudi nyumbani ila kati ya mambo ambayo mama hataki hata kusikia ni hilo.

Baba akipata namba ya mama siku hiyo hiyo mama lazima avunje laini.
Mama anasisitiza kuwa hata asikie anamiliki dunia kamwe hatarejea wala hahitaji chochote bora alale njaa kuliko kurudi kwa baba.

Mama nimempangia nyumba anaishi mwenyewe na binti wa kazi, ila kinachoniumiza ni hiki baba nikiongea naye mpaka machozi yanamtoka akiniomba nimuombee msamaha kwa mama ili arudi.

Pia nimeshindwa hata kumjengea nyumba mama yangu kwa kuhofia kuwa baba ataona kuwa mimi ndo chanzo cha mama kutotaka kurudi.

Kwa kifupi nimeshindwa jinsi ya kulitatua hili naombeni mawazo yenu ndugu zangu,
Ili nijue jinsi ya kulitatua maana baba kila siku tunawasiliana na ombi lake kuu ni hili la kuomba nimuombee msamaha maana yeye kashindwa.
 
Kama alivyosema ndugu hapo juu, tafuta ndugu wa pande zote mbili kwa baba na mama halafu kila mtu atoe yake ya moyoni.

Wewe ni victim mkubwa maana hukuweza kumaliza shule sababau ya sekeseke zile inabidi na wewe utoe la moyoni. Pesa au vitu unavyopewa havitakupa utu wako ulioupoteza sabababu ya mateso aliyowapa baba yako wewe na mama yako.

Mama anaweza asirudi kwa baba ila cha msingi amsamehe basi. Moyo ukishatetereka kuurudisha shida.
 
Pesa sabuni ya roho.
Moyo umeshalainika kwa dolali.

Msamehe baba yako ila mwache mama aamue kumsamehe kwa wakati wake. Don't push her.

Huyo baba yako hana watu wa heshima wa kumsaidia kumshawishi mamako amsamehe?

NB. Baba asichanganye kusamehe na kurudiana😆😆
 
Kama alivyosema ndugu hapo juu, tafuta ndugu wa pande zote mbili kwa baba na mama halafu kila mtu atoe yake ya moyoni.

Wewe ni victim mkubwa maana hukuweza kumaliza shule sababau ya sekeseke zile inabidi na wewe utoe la moyoni. Pesa au vitu unavyopewa havitakupa utu wako ulioupoteza sabababu ya mateso aliyowapa baba yako wewe na mama yako.

Mama anaweza asirudi kwa baba ila cha msingi amsamehe basi. Moyo ukishatetereka kuurudisha shida.
Kweli kabsa ila mimi suala la kutokumaliza shule sababu ya lile sekeseke kwa sasa haliniumizi kichwa naona kama MUNGU alipanga iwe vile. sabab licha ya kutoendelea nimefanikiwa kufikia malengo yote niliyojiwekea na kuwa vile nilivyopanga niwe kipindi kile, na muda mwingine nawaza huenda lisingekuwa lile sekeseke ningesoma nikamaliza chuo nikaajiriwa ningechelewa kuyafikia niliyoyafikia sasa.

Ila katika swala la kushirikisha viongozi wa dini ni sahihi kabsa ila mama ukitaka mkosane na hata wiki iishe bila kuongea mwambie swala hili maana pia wamejaribu ila haikuzaa matunda.
 
DAFU NA NDIMU, Hili jambo linanitesa sana natamani saaana kuona wazazi wangu wakiishi pamoja mimi nimeshasamehe ila kwa upande wa mama ukiliongelea sana utashangaa anapanga safari ya ghafla kwenda nje. Hapo na mawasiliano yatakataa kwa muda.
 
Huwezi jua may be dingi katubu kaona ujinga kujifanya yeye ni bondia.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti malipo ni hapa hapa duniani, samehe 7 *70 Amini nakwambia yale uwafanyiao wenzako hata wewe yatakupata au kizazi chako
 
Pole sana Milale kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana.
Umekua mkubwa lakini wewe bado ni mtoto. Jaribu kutafuta watu wazima na viongozi wa dini labda wanaweza kukusaidia hilo
 
Milale,

Samahani mkuu kama nitakukwaza kwahili nalotaka kuandika hapa.

Kwajinsi ulivyoelezea hapo, kwajicho la tatu nahisi kulikuwa na muingiliano flani ambao haukuwa matched. Ukiangalia mafanikio yenu wewe na baba yako, yalianza baada ya mama yenu kuwa mbali na ninyi. Nachelea kusema, baba yako nq mama yako nyota zao kiuchumi hazikuendana (mshana jr atakuja kunisahihisha hapa)

Kuna watu wakiungana kufanya kazi pamoja hata watumie mabilioni ya pesa ama nguvu kiasi gani, wanaanguka. Ila unashangaa wakiachana kila mmoja akafanya yake, kuna mmoja anafanikiwa sana namwingine anarudi nyuma. Kiufupi niseme, nyota ya mama yako haokuenda ana baba yako hata kidogo (kiuchumi) mimi nina kaka yangu ambaye ana wake wawili, alikuwaa akitaka kwenda kazini, hata kama alilala kwa mke fulani, lazima usafi asubuhi na nguo za kazi akavalie kwa mke mwingine (ambaye kwa maneno yake mwenyewe anasema akinywa chai yake asubuhi wakati anaenda kazini siku hiyo anapata pesa hatari) sisemi mama yako ana nyota ya umasikini La! Hasha, ila hawakumatch na baba yako.

Mshana Jr
 
Haya mambo ni madogo mkuu.. Kama una pesa na Afya nzuri, Sioni Matatizo makubwa zaidi ya hayo
Katika maisha pesa si kitu pekee kinachoweza kukupa furaha, kuna muda mwingine unahisi jambo fulani lingefanikiwa huenda lingeongeza furaha yako maradufu.
 
Mkuu muombee msamaha kwa mama ila swala la kurudiana msijaribu kumlazimisha.
Mateso aliyoyapitia yeye ndiye ayajuaye kwa kina vitendo vyote alivyofanyiawa na baba yako.
Asante kwa ushauri mkuu
 
Pole sana aisee.

Wewe jenga nyumba, acha usela. Timiza wajibu wako tu hayo mengine ya baba kuomba msamaha hayakuhusu.
Unajua mateso aliyokuwa anapewa room na baba yako!?

Unajua wanawake wanafanyiwa ukatili mbaya sana ila hawasemi either kwa kuona itakuwa aibu au fedheha mbele ya watu. Vyumba vinaficha mengi mno.

Kuna mengi yamejificha, huwezi jua.
1. Yawezekana babako kubadilika kweli. Au anataka amtese zaidi.
2. Au anatafuta tu usalama kwenye siasa.
Siasa nazo zina mambo mengi sana.
 
Milale,
Wengi tumepitia huko hivyo usimlazimlazimishe. Baba wa mtoto wangu wa kwanza niliachana naye na mimba ya miezi minne. Alikuja kumwona mwanangu akiwa na miaka 12. That was the last time. Uongo uongo uongo na kujikweza vilimponza. Mimi mwanangu ana baba aliyemuasili hivyo sina mawasiliana na huyo baba. Mama yako usimluaumu kwa lolote. majaribu tunayopitia kwenye ndoa si lazima watoto wafahamu kila kitu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom