Naombeni ushauri, eti biashara inaendana na nyota?

happy amos

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
251
434
Jamani mi nataka kufungua duka la dawa
Kuna shekhe mmoja kaniambia Nyota yangu sio ya kukaa Dukan
Jaman nauliza eti biashara inaendana na nyota???

Hapa nimechanganyikiwa nimeshanunua vitu....nimeanza ukarabati na umenicost karibia 1mil.....sasa nifanyeje?
Naomben ushauri wapendwa
 
Muulize Mungu kama una nyota ya biashara sio mwanadamu, sisi wote ni wapita njia hatujafika tuendapo. Namaanisha umuombe Mungu, iombee biashara yako usimwamini kila mtu hata shekhe, binadamu wana maneno ila Mungu ana Neno juu yako.
 
Asante sana umenitia moyo
 
Jamani mi nataka kufungua duka la dawa
Kuna shekhe mmoja kaniambia Nyota yangu sio ya kukaa Dukan
Jaman nauliza eti biashara inaendana na nyota??? Hapa nimechanganyikiwa nimeshanunua vitu....nimeanza ukarabati na umenicost karibia 1mil.....sasa nifanyeje? Naomben ushauri wapendwa
Dawa gani za mtaji wa 1m? Au miziziology?
 
Jamani mi nataka kufungua duka la dawa
Kuna shekhe mmoja kaniambia Nyota yangu sio ya kukaa Dukan
Jaman nauliza eti biashara inaendana na nyota??? Hapa nimechanganyikiwa nimeshanunua vitu....nimeanza ukarabati na umenicost karibia 1mil.....sasa nifanyeje? Naomben ushauri wapendwa
Kosa lako ni kumsikiza huyu unayemuita Shekhe, hata hivyo mtu anayekaribia kuwa kichaa hawezi kujua atakuwa kichaa!! kwa hiyo huwezi kuwa kichaa ila ukiendelea kumsikiliza huyu jamaa basi utakuwa!!
 
Kama umeamini maneno ya binadamu kuhusu suala analolijua muumba pekee,kweli milembe hakuepukiki.
 
Katika maisha yako usije ukajaribu kuchanganya......

1 - Nuru na Giza

2 - Mafuta na Maji

3 - Kusimama na Kukaa

4 - Shetani na Malaika
 
ndg .. wew vipi!!
duka ni lako
bidhaa ni zako
biashara ni yako.... Sasa shekhe wa nini ??
hebu jitambue are you mad?
just fungua milango ya duka lako, wateja watakuja wenyewe....!!
 
Pole sana Ndugu.

Usiamini maneno ya huyo anayejiita Shekhe, we fanya biashara zako kwa Juhudi huku ukimuomba Mungu.

Anayegawa riziki ni Mungu pekee wala siyo nyota yako au maneno ya Shekhe.

Mungu akusimamie.
 
Hakuna nyota duniani.
Nyota ni mkutano wa gesi zilizokua na joto kali na kusababisha moto mkubwa.

Ila humiliki nyota. Au kuna nyota ulinunua? Mwambie ndio hauna nyota.
 
Pole sana Ndugu.

Usiamini maneno ya huyo anayejiita Shekhe, we fanya biashara zako kwa Juhudi huku ukimuomba Mungu.

Anayegawa riziki ni Mungu pekee wala siyo nyota yako au maneno ya Shekhe.

Mungu akusimamie.
Asante
 
Utakuwa ulienda mwnyw ndo maan kaamua kukupa majb ya hvyo maan haingiii akikini mtu akute unakarbat akwambie huna nyota y kukaa dukan
 
Back
Top Bottom