Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 12,105
- 35,140
Heri na baraka ziwe nanyi.
Ushauri, mawazo, michango yenu itanisaidia sana.
Ni binti aliyenipenda sana nakumbuka alivyoniambia kwavile alivyonipenda hakuwa tayari kuniona mimi natangulia kufa bora aanze yeye.
Kwa jinsi tulivyopendana haielezeki, ilianza hivi, baada ya migogoro kwao alitakiwa arudi kijijini akaniomba nimtafutie kazi, kuhangaika huku na huku akapata, shida ikazidi kwao kwani alikua anakaa na mama wa kambo na baba yake hana kauli.
Akaniomba tena nimtafutie pakukaa, nikahangaika tena akapata, nako shida tena ikawa kubwa, akaniomba nimpangie chumba.
Kwavile nilivyompenda nikaamua tukakae wote kwangu na mimi ndio nilianza maisha baada ya muda, taarifa zikafika kwa baba yake alipinga sana lakini akatoa masharti yaliyokua yananigharimu hela nyingi mno, nikajipa moyo nitafanikisha, binti ninae ndani matatizo yakawa yanapishana binti ni kuumwa tu, miaka ikaenda mpaka wa 3.
Sikufanikisha, mpaka binti mwenyewe akaamua kuniacha kwa kudanganywa na vijana wajanja wakati mimi nampenda.
Mwaka sasa tangu aniache, ninateseka sana.
Ushauri wenu jamani.