Naombeni msaada wenu wana jamii..!

Naombeni msaada wenu wana jamii..!

mc1886

Member
Joined
Feb 6, 2013
Posts
33
Reaction score
0
Waswahili wanasema mficha uchi hazi,
Ni mwaka wangu wa mwisho sasa chuo kikuu, Semester hii nimeshindwa kulipa ada kwa sababu ya ukata. Nimesoma kwa shida sana mpaka kufika nilipo sasa, nimebakiza semester 2 tu nimalize Chuo, Lakini naona mambo yamekuwa magumu hapa mwishoni (Magumu sana). Naona nipostpond semester hizi mbili ili nitafute ada kwanza. Hapa mjini (DAR) social network inahusika kwa kiasi kikubwa. Nina good communication skills, Management skills, sales and marketing skills. Nimesha fanya internship kwenye shirika moja la Maendeleo (Development Organization), Nishawahikuvolunteer kama project coordinator kwa muda wa mwaka mzima, kwa kuorodhesha machache. Niko tayari kufanya yoyote ilimradi ni halali.
Naombeni msaada wenu wanajamii, najua huu ni mtandao kubwa sana, kwa sasa nahitaji kazi. (Yoyote halali) Niko tayari kutoa details zangu (C.V) kwa yeyote atakaye hitaji.

Asanteni kwa muda wenu.
 
Duh!ni uwezo tu sina,ila ningekua nao hakika ningekusaidia.nimekuonea huruma sana mkuu,kama vp jaribu kupitisha bakuli kwa wana ukoo wako wote wanaweza kukusaidia.
 
Duh!ni uwezo tu sina,ila ningekua nao hakika ningekusaidia.nimekuonea huruma sana mkuu,kama vp jaribu kupitisha bakuli kwa wana ukoo wako wote wanaweza kukusaidia.

Asante sana Perry. Yah ni wazo zuri kabisa,tatizo ni kuwa natokea koo maskini. Ila bado ninalotumaini.
 
pole sana,labda uongee na mkuu@Invisible wana jf tupitishe bakuli tuko wengi sana so haitakuwa a lot individually....
 
pole sana,labda uongee na mkuu@Invisible wana jf tupitishe bakuli tuko wengi sana so haitakuwa a lot individually....

True tukipitisha bakuli hata elf tano tano c mbaya tho wengine can give more,,instead of kuchangiana maharusi minimum elfu hamsin bora tukamsaidia mwenzetu..Unasoma Course gani??nyumbani je hamna hata shamba angalau ukaweka bond kwa mtu ukapata ada?wasoma chuo gani?mkopo hukupata??nani alikuwa anakulipia before?
 
Dogo mwenyew nimetokea familia maskini nilipitia haya lakin namshukuru mungu nilifanikiwa na ss nina master Mkuu invisible nafikir ataona ni jinsi gn tukusaidie binafsi niko tayari kukuchangia mdogo wangu pole sana mdogo wangu
 
Ndugu, jamaa na Marafiki ndiyo walikuwa wakinisuport, sababu wazee walishatangulia mbele ya haki muda sana. Sina altenative nyingine ndo maana nimelileta suala hili hapa. Asante sana kwa kuguswa. Naomba niku PM no yangu ya simu alfu ntakupa details zote unazohitaji kufahamu..
 
True tukipitisha bakuli hata elf tano tano c mbaya tho wengine can give more,,instead of kuchangiana maharusi minimum elfu hamsin bora tukamsaidia mwenzetu..Unasoma Course gani??nyumbani je hamna hata shamba angalau ukaweka bond kwa mtu ukapata ada?wasoma chuo gani?mkopo hukupata??nani alikuwa anakulipia before?

Asante sana kwa kuguswa. Ndugu, jamaa na Marafiki ndiyo walikuwa wakinisuport, sababu wazee walishatangulia mbele ya haki muda sana. Sina altenative nyingine ndo maana nimelileta suala hili hapa. Nafanya degree ya maendeleo, napenda nikupe details zangu zote, je kuna njia yoyote naweza kuitumia walau private?
 
Dogo mwenyew nimetokea familia maskini nilipitia haya lakin namshukuru mungu nilifanikiwa na ss nina master Mkuu invisible nafikir ataona ni jinsi gn tukusaidie binafsi niko tayari kukuchangia mdogo wangu pole sana mdogo wangu

Asante sana mkuu! Nina amini kuwa Mungu atafungua njia, na hii semester haitapita bure. I have that feeling.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom