Naombeni msaada wenu sana..!

usy

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2019
Posts
209
Reaction score
165
Habari za Jumapili wana jamvi..
Naombeni msaada kwa mwenye ujuzi juu ya hili. Nataka nisome Diploma ya Clinical medicine mwaka wa masomo 2019/2020 na vigezo vyote vilivyopo kwenye Nacte quide book ninavyo.
Wasiwasi wangu upo hapa, Mimi ni graduate wa bachelor degree mwaka 2018 na siku soma kozi za afya ila vyeti vyangu vya form four na form six vina qualifications za kusoma kozi tajwa hapo juu...
lengo langu ni kubadilisha career kutoka kwenye hiyo niliyo graduate na kuhamia kwenye kada ya Afya, Je kutokana na utaratibu uliopo naweza fanya hivyo au mpaka nisubiri miaka kadhaa ipite kama wasemavyo baadhi ya watu?

Ahsanteni, msaada wenu ni muhimu sana kwangu..!
 
Mkuu una moyo sana!

Nahisi huna misimamo katika maamuzi yako. Nataka kuamini kwamba hiyo course uliyohitimu uliichagua mwenyewe na kuwekeza time yako, pesa zako, nguvu zako etc etc.

Hakuna course mbaya mkuu, na wala ajira isiwe ndio driving force yako katika maamuzi yako.

Think again mkuu
 
nashukuru mkuu kwa mawazo yako,, ni kweli kozi niliyosoma nilichagua Mimi ila Nina sababu maalum zinazonifanya nifanye ninachotaka kufanya na sio ajira..
 
Lengo lako ni kupata ajira, right?

Anyway, Elimu haina mwisho na huyo aliyekudanganya msomi kama wewe na akafanikiwa mwambie namkubali sana. Aje atusaidie kumdanganya na bosi wetu mkuu kuwa maendeleo hayana chama.

Kifupi ni kwamba kama una pesa yako mfukoni hakuna haja ya kupoteza muda. We apply, lipa ada, piga shule.

Ila chonde usije ukatufanyia operesheni ya kichwa wakati tukitaka kutibiwa tezi dume

Kila la kheri swahiba
 
Ahsante mkuu,, lengo langu sio ajira lengo langu ni kurud katika ndoto yangu ya miaka mingi ambayo ilikatishwa na siasa chafu na tamaa ( naweza kusema hivi)..
 
nashukuru mkuu kwa mawazo yako,, ni kweli kozi niliyosoma nilichagua Mimi ila Nina sababu maalum zinazonifanya nifanye ninachotaka kufanya na sio ajira..
Ni sababu gani hizo?? Jiskie huru ku-share hapa maana humu kuna watu wana experience na mambo kadhaa wa kadhaa
 
Ahsante mkuu,, lengo langu sio ajira lengo langu ni kurud katika ndoto yangu ya miaka mingi ambayo ilikatishwa na siasa chafu na tamaa ( naweza kusema hivi)..
Pole. Kwahiyo digrii yako umesomea "Political Science"?
 
Ni sababu gani hizo?? Jiskie huru ku-share hapa maana humu kuna watu wana experience na mambo kadhaa wa kadhaa
kusoma na kujihusisha na mambo yahusuyo afya ya binadamu ni ndoto yangu tangu nikiwa mdgo, ila ilikuja kupoteza mwelekeo mwaka 2015 pale nilipoamini katika siasa chafu pamoja na tamaa..
 
sijasoma political science ila nimesoma hizi kozi za mafuta na gas (Petroleum) zilizoazishwa na wanasiasa.
Mjomba kimbia Mtwara hapo ukalambe ajira... Rostam si kafungua limtambo hapo Kigamboni?
 
Mjomba kimbia Mtwara hapo ukalambe ajira... Rostam si kafungua limtambo hapo Kigamboni?
hizi ndo aina ya hizo siasa zilizonipoteza.. vitu kama hivi unaaminishwa ukiwa nje ya hii field ila ukiingia ndani ukaona uhalisia utajuta
 
Yes Fanya hima kijana hujachelewa hakuna Mtu anayamiliki maisha yako zaidi ya wewe Mwenyewe.

Wala hutakiwi kusubiri miaka ipite,nawajua wengi sana wamesoma shahada kama sociology,taxation, political,economics waliamua kutumia vyeti vya Form four kusoma kozi za afya na wako very happy.

Muhimu ni usichague vyuo vya serikali, chagua private
Vya serikali wanalimit muda wa kumaliza form four.
Na wanakuja kukujulisha baada ya selection kutoka.
Enjoy Your life,Life is too short.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…