Naombeni msaada wenu nahisi nimeibiwa na Yono auction mate

INFAITH

Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
12
Reaction score
5
Kabla ya kueleza tukio ningependa kuuliza hivi jukumu la YONO Auction Mart ni lipi maana dada yangu anahisi kuibiwa..!
Kimsingi siku chache zilizopita dada yangu alikamatwa na gari kwa kosa la kutokuwa na road lisence baada ya muda wake kuisha. Yono walikamata gari na kulipeleka kwenye ofisi zao maeneno ya TEMESA.
Ikabidi dada yangu aende TRA kulipia road lisence na kwenda kwenye ofisi za Yono kwa lengo la kuchukua gari lake baada ya kulipia hiyo road lisence, ajabu ni kwamba YONo HAWAKUMPA GARI BADALA YAKE WAKAMWELEZA ANATAKIWA KULIPIA SH50,000 ikiwa ni malipo ya kukamata gari na 56,200 ya kulaza gari kwa siku mbili (2). ikabidi dada yangu awaulize swali kwani kosa si tayari kishalishughulikia kwa kulipia road lisence TRA? lakini wakasisistiza kuwa hizo gharama lazima zilipwe, hakika hakupewa gari mpaka pale alipolipa sh. 106,200 ndo wakampa gari. Je malipo haya jamani ni halali? kwani sheria ya trafic inasemaje? kwa nyongeza risiti ya malipo hayo anayo. naombeni msaada niweze kumshauri maana anataka aende TRA na kwenye mamlaka zingine kutafuta haki haki ingawa ni pesa ndogo.!!!!!karibuni kwa michango waungwana.
 
ndio ni halali na umshauri asirudie kuchelewa kulipa road license kama hela hana kwa wakati huo ni bora apaki gari atumie usafiri mbadala.
 
Kabla ya kueleza tukio ningependa kuuliza hivi jukumu la YONO Auction Mart ni lipi maana dada yangu anahisi kuibiwa..!
Kimsingi siku chache zilizopita dada yangu alikamatwa na gari kwa kosa la kutokuwa na road lisence baada ya muda wake kuisha. Yono walikamata gari na kulipeleka kwenye ofisi zao maeneno ya TEMESA.
Ikabidi dada yangu aende TRA kulipia road lisence na kwenda kwenye ofisi za Yono kwa lengo la kuchukua gari lake baada ya kulipia hiyo road lisence, ajabu ni kwamba YONo HAWAKUMPA GARI BADALA YAKE WAKAMWELEZA ANATAKIWA KULIPIA SH50,000 ikiwa ni malipo ya kukamata gari na 56,200 ya kulaza gari kwa siku mbili (2). ikabidi dada yangu awaulize swali kwani kosa si tayari kishalishughulikia kwa kulipia road lisence TRA? lakini wakasisistiza kuwa hizo gharama lazima zilipwe, hakika hakupewa gari mpaka pale alipolipa sh. 106,200 ndo wakampa gari. Je malipo haya jamani ni halali? kwani sheria ya trafic inasemaje? kwa nyongeza risiti ya malipo hayo anayo. naombeni msaada niweze kumshauri maana anataka aende TRA na kwenye mamlaka zingine kutafuta haki haki ingawa ni pesa ndogo.!!!!!karibuni kwa michango waungwana.
Ni halali
 
Halali kabisa, ndio malipo yao hao waliokushika.

Dada'ko angelipa road license on time yasingemkuta hayo.
 
uhalali unakujaje maana ninavyofahamu YONO wao wamepewa kazi ya kukamata na wanalipwa na Serikali, tafadhali mwenye uthibitisho wa nyaraka yoyote ya hii kampuni atupie hapa nione uhalali huo
 
Ur in denial brother....tulia tu hakuna wa kukupa majibu unayotaka kuyasikia mkuu huo ulioambiwa ndiyo ukweli.
 
Kashaibiwa huyo , ukilipa tra unatakiwa pia kukipa pake TEMESA kwa ajiri ya park
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi wa Yono si waaminifu. Serikali itangaze wazi tozo za makosa na faini zake ili ujanja wa kubambikiana gharama ufe. Pia maswala ya faini au tozo kupokelewa cash ni chanzo cha rushwa na serikali kupoteza mapato. Kwanini serikali isilazimishe hawa madalali kuweka matangazo ya wazi hadi kwenye ofisi zao utaratibu wa malipo ili pale watu waende na risiti tu hata kama ni parking fees?
 
Kawaida mkuu, hata leseni ya biashara ukichelewa unapigwa penati 25%+50000 ya kufuatwa ofisini kwako kama wakikukamata, ila ukienda ofisini mwenyewe kulipa kwa kuchelewa utapigwa 25% tu.
 
Back
Top Bottom