Naombeni msaada wajuzi wa mambo ya Insurance

obseva

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
541
1,000
Naombaeni msaada wajuzi wa mambo ya Insurance

Nilinunua gari aina ya VOLTs mwaka 2015, na ikapata bima ya kwanza August 2015, yenyewe ikiwa imetengenezwa mwaka 2003, na gharama yake yote ambayo bima ilibeba mwaka huo 2015 ilikuwa million 14.2 ambapo walinicharge premium ya shilingi 586,460(comprehensive).

Mwaka 2016 haikukatiwa bima kabisa, mwenyewe sikuwepo na waliokuwepo walikuwa hawaitumi sana zaidi ya dharura ambazo waliziona ni muhimu pia ili kuongezea uhai na kuifanyisha mazoezi. Kilicho sabibisha niulize, leo nikiongea na insuarers kwa ajili ya kuikatia bima napatiwa premium tofauti tofuati Kiasi najiuliza thamani ya gari leo ni tofauti kwa kadiri ya agent wa bima? Hakuna ulali wa kukokotoa thamani halisi ya leo ya gari hilo?

Sitawataja majini hao mainsuarers na lakini kuna mmoja kaniambia, 492,000/, mwingine 442,000/ Mwingine 468,000/ najiuliza kwanini inakuwa hivyo?

Naombeni msaada wa kimaelezo ili nipate ufahamu, hasa kujua thamani halisi ya gari leo na possible premium. Natanguliza shukurani
 

RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,376
2,000
Hii biashara haijaangaliwa vizuri, mara nyingi hakuna clear procedure za kumfanya mteja aridhike na huduma zaidi ya kuingia gharama za kulipia insurance na mwisho wa siku kunakuwa na mlolongo mrefu wakati unapokuwa na dharura.

Watu wa insurance watakuja na maelezo zaidi mkuu nisiongee sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom