Naombeni msaada wa ushauri nasaha

na hakika wanasheria wana mbinu za kumsaidia.
Kupata mali kama ndoa ilikuwa ya miaka 12..


sina uhakika kwa hiyo nauliza.
kwa Tanzania mwanamke anaweza kumpa mume talaka???
ntashukuru kupata jibu Kiranga.

Kiswahili tunasema "mwanamke anaomba talaka yake" 🙂 Hawezi kumpa mwanamme talaka kwa sababu mwanamke hajaoa, kaolewa. Mfumodume.

Kisheria, wote wanaomba talaka.

http://tanzanet.org/downloads/laws/the_law_of_marriage_act_1971_(5_1971).pdf

(d) Separation and Divorce

Right to 99.

Subject to the provisions of sections 77, 100 and 101, any petition for separation or married person may petition the court for a decree of separation or divorce on the ground that his or her marriage has broken down,but no decree of divorce shall be granted unless the court is satisfied that the breakdown is irreparable.
 
Hawezi kwenda mahakamani tu na kusema nimekuja kufungua kesi ya madai ya talaka, so anachotakiwa kufanya ni either kwenda baraza la kata na kufungua kesi huko, kata wakishindwa watampa go ahead ya kwenda mahakamani au kanisani ambako nako wataendesha kesi za usuluhishi kanisa likishindwa sasa nao watampa baru ya kwenda mahakamani
 
thax dear,iyo board inaundwaje? tuanzie hapo...maana mume wake hamtaki ila ni mchaga anajikausha tu ili wasigawane mali wakati wamechuma wote kipindi wameoana hawakuwa hata na bodaboda

ndio zao,anajifanya anampenda mke kumbe anawaza mgao wa mali,ngoja na mm nipate mwongozo baba nanilii atanitambua!
 

.....mume hataki kutoa talaka na anadai hana shida na mkewe.

Vipi, nini msimamo wa mke?
Huenda ukanijibu (mume kamfukuza, hazungumzi nae nk)
Lakini kwenye baraza la wazee mke ndio ataonekana ameondoka, wkt mumewe bdo anamtaka.

Kwa msimamo wa huyo mume, mke yupo tayari kusuluhishwa na kurudiana na mumewe?
 
natamani kujua huyo dada alikuwa akijishughulisha na nini wakati akiishi na mumewe...
 
bibie.@Smile huyu mume anataka kumtesa tu mke wake hampendi huyo mke ushauri uliopo ni kuwa huyo Mwanamke aende Mahakamani kumshitaki mumewe ndipo atakapopata haki zake pasipo na njia hiyo hawezi kupata haki yake. Hakuna ndoa hapo wala hakuna mapenzi hapo.
 
Smile kuna hatua ana takiwa apitie ili aweze kupewa talaka, kwanza anatakiwa aende na madai yake kwenye baraza la usuluhishi wa ndoa na mume wake ataitwa kusuluhishwa mpaka waakikishe imeshindikana kusuluhisha ndio wana file devorce.
Kutoka nje ya ndoa inaweza ikawa sababu ya kupewa talaka lakini ushahidi utahitajika.
Kwa swala la mali kama walichuma wote watagawana na kama kuna mali mwanamke alizikuta pale kabla ya ndoa hizo zinabaki kuwa za mwanaume.
Mshauri aende kwanza mahakama ya mwanzo.

Lazima ziwepo sababu za kutosha za kuvunja hii ndoa!

 
Na akisema atumie njia ya kanisani itakuwa ngumu kupata talaka!
Wachungaji huwa hawkubali kuvunja ndoa kabisa.

Bora aende kwenye baraza la usuluhishi lakini nikiangalia hapa hii ndoa haiwezi kuvunjwa maana inaonekana hakuna sababu mathubuti na huyu mwanaume atakomaa ana mpenda na watazungushwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Hizi ndoa jamn,kama kungekua na uwezekano wa kulegeza viapo wangelegezaga tuuu mana wanandoa wengi hawapo tayar kwa SHIDA...ila kwa RAHA wote wamo
 

LiverpoolFC Muumba hapendi wanaharamu.jisomee Malachi 2: 15-17
 
thax dear,iyo board inaundwaje? tuanzie hapo...maana mume wake hamtaki ila ni mchaga anajikausha tu ili wasigawane mali wakati wamechuma wote kipindi wameoana hawakuwa hata na bodaboda

Hayo mabaraza ya usuluhishi yapo chini ya wizara ya ... na ustawi wa jamii ..... yapo kila mkoa/wilaya. Hivyo anaweza kuanzia hapo. Makanisa pia yana hayo mabaraza lakini huwa wagumu sana kutoa certificate ya kushindwa kusuluhisha.

Akisha anza huo utaratibu wa kisheria hakutakuwa na kujikausha wala nini! Hawezi kusema anampenda mke wake huku hataki kuishi nae!
 

Ni kweli kama lengo ni talaka huwa ngumu sana kupitia kanisa.

Huyo mwanaume hawezi tu kusema anampenda mke wake wakati hataki kuishi nae. Wamekuwa katika separation kwa miaka 2, hawashiriki katika tendo la ndoa sasa atang'ang'aniaje kuwa anampenda? Inabidi huyo dada ajieleze vizuri kwanini anaona ndoa yao ni irreparably broken and thus warranting divorce.
 
kumbe Rutashubanyuma na mwaJ mnajua hii mambo ya sheria ntawatafuta soon.
 
natamani kujua huyo dada alikuwa akijishughulisha na nini wakati akiishi na mumewe...
wanas maduka alikuwa anauza duka lao kubwa tu yeye na mumewe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…