Naombeni msaada wa dawa ya kuzuia kukoroma usiku

Mwenzenu nimekuwa na tatizo la kukoroma saana usiku mpaka imekuwa kero kwa mke wangu. Kuna kipindi alikuwa ana lalamika eti namkosesha usingizi kwasababu ya kukoroma kwangu.

Nilibisha nikaona anaanza vituko, nikampiga mkwara usiku huu nilivyokuwa nimelala amerecord video fulani yangu nikiwa usingizini na kuniamsha.

Nilivyoamka akaniambia kuwa amechoka, anakosa usingizi kwasababu ya kulala kwangu. Nikataka kupiga mkwara kama kawaida yangu akanionyesha video, kuangalia hivi ni mimi kweli.

Nakoroma kama vile mtu ambaye ana maji kwenye koo, nikashindwa la kusema.

Naomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza jua tatizo hili linachangiwa na nini na dawa yake ni nini.

Naomba anisaidie mwenzenu ndoa yangu mbichi kabisa lakini kwa style hii naona hatuna marefu uko mbeleni. Mimi situmii pombe, au sina kitambi sasa sijui tatizo litakuwa wapi?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Change position mkuu hakuna namna
 
Kukoroma haijawahi kuwa tatizo la kuvunja ndoa, kakuchoka anakutafutia sababu.
Hivi unajua kuna koroma kama engine ya train? Binafsi siwezi kulala na mtu anayekoroma. Usingizi sitapata. Nilipokuwa A level shule Moja hivi nilikuwa kiongozi na viongozi wakuu tuna vyumba maalum vya kulala wawiliwawili. Mate wangu alikuwa mkoromaji kiasi kwamba iliniathiri nikawa silali usiku na mchana nasinzia karibu nipate mental disturbance. Ikabidi shule impe chumba chake mwenyewe. Hivyo kukoroma ni tatizo kubwa mno. Kuna dawa za asili za kusaidia Hilo tatizo japo sijui ufanisi wake.
 
Dawa ni moja tu ach kulala anza kukesha utanishukuru badae
Bahati mbaya, hauwezi kujijua kuwa unakoroma, kwani unakoroma ukiwa usingizini. Hivyo, inawezekana hata wewe huwa UNAKOROMA sana, hujijui tu!
Pia, ushauri kuwa kubadilisha aina ya ulalaji, nao hautasaidia, kwani tulalapo huwa tunajigeuza geuza mara kwa mara tukiwa usingizini, hivyo hatujijui kama tunajigeuza.
 
Hivi unajua kuna koroma kama engine ya train? Binafsi siwezi kulala na mtu anayekoroma. Usingizi sitapata. Nilipokuwa A level shule Moja hivi nilikuwa kiongozi na viongozi wakuu tuna vyumba maalum vya kulala wawiliwawili. Mate wangu alikuwa mkoromaji kiasi kwamba iliniathiri nikawa silali usiku na mchana nasinzia karibu nipate mental disturbance. Ikabidi shule impe chumba chake mwenyewe. Hivyo kukoroma ni tatizo kubwa mno. Kuna dawa za asili za kusaidia Hilo tatizo japo sijui ufanisi wake.
Kukoroma NI tatizo kubwa
 
Pole sana,kukoroma ni hali inampata mtu yeyote,na kelele kuna watu ndio fantacy zao,so ziheshimiwe
 
Likely una sleep apnea. Google sleep apnea na utapata maelezo mengi na ya kina na jinsi ya kupunguza kukoroma. Kuna mpaka mazoezi ya kufanya na app za kulipia zitakazokuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kuimarisha hiyo misuli ya koo inayo-collapse usiku ukilala na hivyo kupelekea kukoroma.

Kisababishi kikubwa mara nyingi ni kuongezeka uzito au kuishi sedentary life. Na ushauri wa kwanza kwa daktari huwa ni kuambiwa upunguze uzito na/au uanze kufanya mazoezi. Utashauriwa pia uache kulalia mgongo na ulale kwa ubavu japo hili siyo suluhisho la kudumu.

Suluhisho la kuaminika ni kutumia CPAP machine. Hii ina mask unavaa usiku na inasukuma hewa unapokuwa umelala na kuhakikisha hizo muscles za kwenye koo hazi-collapse. Njia nyingine ni kutengenezewa mouth guard kama zile wanazovaaga akina Mandonga kwenye ngumi. Hii inatengenezwa kitaalamu baada ya kupima configuration ya taya lako na usiku unaivaa. Inasaidia kuhakikisha kuwa hewa inapita usiku bila kuzuiwa unapokuwa umelala.

Shida ya sleep apnea mbali na kukoroma kuna kipindi hewa inashindwa kupita kabisa na hivyo ubongo inabidi ukuamshe vinginevyo unaweza kukata moto watu wakaimba parapanda. Kwa hivyo usiku kucha ubongo haupumziki uko stand by kukushtua uamke ili upate Oxygen unayoihitaji sana. Ndiyo maana kesho yake mkoromaji mwenye sleep apnea anakuwa amechoka sana hata kama atakuwa amelala masaa 10. Kama uko bado kijana ni sawa lakini huko mbele ya safari sleep apnea inatajwa kuwa ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha strokes (+ heart attacks); na magonjwa mengine ya akili kama dementia na hata Arzheimer. Ubongo unahitaji supply nzuri ya Oxygen 24/7!

Na hiyo shtuka shtuka ya ubongo pia inaathiri sana afya ya moyo. Usiku moyo unatakiwa kupumzika na mapigo ya moyo hupungua sana mpaka kufikia hata 50s kama uko physically fit. Ukiwa mkoromaji sana maana yake moyo haupumziki maana unakuwa stand by usiku kucha kusukuma damu kwa wingi kwenda kwenye ubongo ili kuhakikisha ubongo una Oxygen ya kutosha. Mapigo ya moyo kwa mkoromaji yana-fluctuate sana usiku kucha moyo ukipambana kuhakikisha kuwa ubongo unapata damu (Oxygen) ya kutosha. Matokeo yake baada ya miaka 10 hivi au huko uzeeni unaweza kupatwa na shida za moyo kama moyo kupanuka na matatizo mengine.

Huku kwetu tunachukulia jambo hili kirahisi tu lakini tafiti mbalimbali zimeanza kulihusisha na ishu ya wanaume kufa mapema maana wakoromaji wengi ni wanaume hasa ukizingatia kuwa wenyewe ndiyo wanywaji wa pombe, wavuta sigara na wepesi wa kunenepeana - mambo ambayo yanatajwa kuwa yanaweza kusababisha ukoromaji na sleep apnea. Kwa hivyo tusichukulie ukoromaji kuwa ni jambo la kawaida. Wakati mwingine unaweza kusababisha matatizo makubwa japo ni kwa muda mrefu!

Kama walivyoshauri wadau hapo juu kwa sasa mwambie mkeo akusaidie kwa kuhakikisha kuwa unalala kwa ubavu. Anza kufanya mazoezi ili kupunguza mafuta mwilini (hata kama huna kitambi) na kuimarisha afya nzima. Fanya mazoezi ya kuimarisha hiyo misuli ya koo (Google au tafuta app nzuri itakayokuongoza). Kama hakuna mabadiliko basi nenda ukaonane na sleep specialist na yeye atakupima kama una sleep apnea ama la...na atapendekeza mambo ya kufanya.

Jitahidi ulimalize hilo tatizo...

Happy New Year mkuu
 
Nunua redio uwe unalala nayo usiku kucha hiyo sauti ya mkoromo itanyonywa na ya redio
 
FB_IMG_16844222333754342.jpg
 
nashukuru sana kaka, kupitia uzi wa broh, nimepata kujifunza vingi kutoka kwako, namna alivyoeleza broh, ndivyo na mimi ninavyoteseka hata nikiwa kwenye halaiki ya watu, nikipatwa na usingiz kidogo inakuwa shida lakin pia kuamka na uchovu.
 
Mimi nilikuwa na sleep apnea pia. Yaani ilifikia mahali nikifika kwenye red light zikichelewa tu kubadilika mimi nasinzia huku nimeshika usukani mpaka watu wanipigie honi. Nalala hata masaa 10 lakini nikiamka nakuwa hoi hatari.

Nilikwenda kwa specialist na kweli akanipima na kukuta nina sleep apnea tena critical. Aliniandikia hiyo CPAP machine na nilininunua (ni ghali - dola 4999). Hii ilinisaidia sana na nikaanza kulala vizuri bila kukoroma na uchovu ukaisha lakini sikupenda niwe mtumiaji wa kudumu.

Nilifanya mambo mengine mpaka nikaachana nayo na mpaka sasa kukoroma ni kama vile nimeacha labda kidogo nikilala chali. Na nimedhamiria kuacha kabisa hata nikilala chali. Ni kwa kufanya mazoezi tu na kufuata masharti mengine japo ni zoezi la pole pole na linachukua muda.

Natumaini hata wewe utaweza kuachana na tatizo hilo hasa kama bado uko under 45 maana huko mbele ya safari ni hatari sana kiafya!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom