Naombeni msaada...True story

Ivan Prosper

Senior Member
Nov 28, 2016
153
225
Naandika mkasa huu nikiwa na huzuni nyingi. Kitu kilichonitokea mwenzenu katika kipindi cha miezi minane iliyopita, nisingependa kimtokee hata adui yangu mkubwa kuliko wote. Huenda kwa baadhi yenu, hiki chaweza kuwa kichekesho cha kuwavunja mbavu, na mkaona ni masikhara tu. Lakini Mwenyezi Mungu tu ndiye anayejua yaliyonikuta mwenzenu! Nitasimulia mkasa huu ambao ni wa kweli tena kweli kabisa.

Mimi ni Mpakistan. Ninaishi pamoja na mama na kakaangu. Baba alifariki dunia muda mrefu nyuma. Hivi sasa nina miaka 28. Nilipokuwa na umri wa miaka 26, mara nyingi, nilikuwa nikiota ndoto kuwa nafanya tendo la kujamiiana na wanawake mbalimbali. Wanawake hao walikuwa wazuri na warembo kwelikweli. Nilipozinduka usingizini, nikajihisi kuridhishwa na nguo zangu zilichafuka!
Mwanzo nilidhani ni tamaa tu ya mwili kufanya jimai. Lakini baadae nikaona si bure! Ndoto hizi za usiku zilikuwa na jambo ambalo si la kawaida! Hata hivyo, sikuzitilia maanani sana. Na pilikapilika zangu za maisha mchana zikanisahaulisha jambo hilo.

Nikazungumza na rafiki zangu kuhusu jambo hilo nao wakabaki kunitania tu. Utani wao pamoja na kunicheka kukanifanya nisite kuzungumza jambo hilo na mtu mwingine yeyote yule. Mwaka jana nilifunga ndoa na binti wa binamu yake mama. Lakini kabla ya ndoa kufanyika, nilikutana na mwanamke mmoja bafuni. Alikuwa ni mwanamke wa kawaida kihaiba na alivaa nguo nyeusi.

Alikuwa na uso wa bashasha. Miguu yake ilikuwa mikubwa sana na yote imepinda; haifanani na ya binadamu. Nikapiga yowe, “mamaaa!” Na papo hapo nikazirai. Ndugu zangu wakaja mbio-mbio kuniokoa.

Nilipopata fahamu, nikawafahamisha kilichotokea. Mama akaniambia niswali na nilete dhikri. Nikafanya hivyo na kupata nafuu. Baada ya kufunga ndoa, ndipo ilipokuja siku ngumu zaidi. Furaha ya ndoa ikanisahaulisha kila kitu. Usiku wa kwanza wa fungate, mke wangu akawa na tabia ambayo sikuitarajia kabisa.

Akawa jeuri na akanisukuma kila nilivyotaka kumkaribia. Nikafadhaishwa na jambo hilo, na nikamuhadithia mama. Mama akazungumza na mke wangu. Lakini jambo la kushangaza, mke wangu akasema kuwa yeye hakujua kabisa kama amenifanyia jambo hilo usiku. Kila nilivyotia nia ya kumuingilia mke wangu, kikatokea kitu kisichokuwa cha kawaida. Mambo yakaanza kuwa mabaya. Mimi na mke wangu tukawa tunasikia kelele kwelikweli zilizokuwa zinatokea bafuni.
Pia tukawa tunamsikia mwanamke akicheka kwa sauti kali nje ya dirisha la chumba chetu cha kulala. Zaidi ya hivyo, kila nilipotaka kumuingilia mke wangu, nikawa naona sura za kutisha mbele ya macho yangu na zaidi nikasikia mayowe (kelele za kunizomea).

Mimi na mke wangu sasa tukawa tunaogopa kiasi kwamba tulitoka nduki chumbani kwetu na kukimbilia chumbani kwa mama. Tukaenda kulala pamoja na mama chumbani kwake. Mama naye akaingiwa na woga. Mimi na mke wangu tukaanza kuswali Swala tano. Tukasoma Qur’an muda wote na kuleta dhikri. Tukajitahidi kwa kila hali lakini wapi hatukuweza kuepukana na Jini huyo.
Tulikwenda kwa watu mbalimbali ambao walitushauri tufanye mambo ya ajabu ajabu! Mathalani, walitwambia tuchome mafuta fulani usiku wa manane.
Mtu mmoja akatupatia kipande cha karatasi kilichokuwa na maandishi ya ajabu-ajabu. Mwingine akatwambia angekuja nyumbani kwetu kufanya jambo fulani ambalo lingesafisha kila kitu.

Akataka tumpe pesa nyingi (40, 000 ya Kipakistani). Kila tulichoshauriwa, hatukukubaliana nacho. Yote tuliyoambiwa yalikuwa kinyume na Uislamu na tukawa na shaka nayo. Miezi minane ikapita bila ya mimi na mke wangu kuingiliana. Kimaumbile, mimi ni mzima kabisa, na kiafya ni mzima. Sasa mke wangu amenikimbia na anataka talaka yake. Ndugu wa mke wangu na wazazi wake wananisema vibaya kwamba mimi sina nguvu za kiume (jogoo hapandi mtungi). Kijamii, inaniumiza sana. Maisha yangu ya ndoa ndio basi tena yameharibika. Maneno ambayo yanasemwa dhidi yangu, hakuna mwanaume anayeweza kuyavumilia!

Inatia uchungu kusema, lakini Shetani kafaulu kunivunjia ndoa. Hata hivyo, nilichobakia nacho ni Imani yangu. Naamini kabisa hili ni jambo la muda, linapita tu. Nataka kuoa tena lakini nahitaji tiba. Nahitaji msaada. Nitawezaje kuondokana na kadhia hiyo moja kwa moja?
 

Password

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
779
1,000
Safi sana uwe unaanza hivi hivi kwamba ni story ya kweli itakuwa inavutia zaidi afu utawaokota wengi sana,kwahiyo inamaana huyo jini anakupenda hataki uoe mke haha mkasa wa kusisimua huu,em niagize bapa muendelezo tafadhari.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Pole sana, ukimshinda huyo shetani anayelala nawe ukiwanumesinzia yote yataisha.

Natumaini wajuzi watakupa ushauri na uweze kurudiana na mkeo, mkae maisha ya furaja na kuzaa watoto.
 

kichengere coi

Senior Member
Dec 11, 2016
161
225
nimekusoma vzr lakini kuna sehem sijakuelewa. umesema umeenda sehem mbali mbali ukawa unapewa vitu tofaut bila ww kuvielewa sasa ulienda kufannya nini? unasema ivyo vitu vyote vinakinzana na dini ya kihsilam kwahiyo uisilam unakubali majini? kama unataka uondokane na hilo kubali kulifulia nguo yaani ufanye bila kuchagua iwe kutibiwa na dini au wataalamu binafsi.
 

rootsquare

Member
Sep 30, 2016
31
125
Sikia najua imani yako na yangu nitofauti mimi ni mkristo wakatoriki ila nakumbia kitu utafanikiwa kama utafanya kwa imani nenda kanisa katoriki lolote lilopo karibu nawe omba maji ya baraka. Kisha mwaga majia baraka nyunyuzia maji ya baraka chumbani kwako kabla ya kulala na kuamka kisha fanya ishara ya msalaba kama uteweza najuhakishia utafanikiwa , kunadada kila alikuwa kalala akimka anakuta michirizi ya damu ya mnyama nikamwambia akanyunyuzia kila siku hiyo hali imetoweka.
 

mamaafacebook II

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
2,472
2,000
Hizi si ndio nyuzi huwa wanamuita mshana jr au? Haya mambo huwa yanatokea kweli, au huwa fables tu?
Yanatokea sio fables

Imani yake s thabiti

Unajua unapoomba Mungu kwa imani haswaa jambo lako hua yataka ue mvumilivu kwenye kusubiri majibu

Huyo kiumbe kishamuona mtoa mada imani yake ndio maana anamchezea

Namshauri yafuatayo

Akilala alale na udhu

Aombe dua ya kumkinga na viumbe waovu

Akasomewe ruqya
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,445
2,000
...duh pole mkuu....

...jinni linataka kufaidi peke yake :cool::cool::cool:

...huyo mkeo na yeye sio understanding,kama mlisikia au kuona hayo marue rue WOTE kwa nini anakutangazia vibaya na anataka kukuacha kwa kosa sio lako???

HAMA nyumba,kisha endelea na sala,soon yataondoka,kaza tu mkanda,usiogope.
 

wsaria

Member
Jan 14, 2014
69
125
ndugu yangu pole sana, lakni pia jambo lako sio kubwa wala zito kama unavyoona na kidhani, jibu lake ni kumwamini Mungu wa Yesu Kristo na kumkiri kwa kinywa chako, tafuta kanisa ambalo lipo jirani yako ukaombe uombewe utapata uzima na utaendelea na ndoa yako bila shida....kwa kuanzia hata sasa anza kusema lwa Jina la Yesu kila ukisali utaona badiliko..hongera kwa uzima
 

mashishanga

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
612
500
Kaombewe Huyo jin atatoka vinginevyo hautaweza kuoa maisha yako yote huyo jin mahaba kashakufanya mume, hivyo jitahid kwenda kuombewa
 

Designer_3434

JF-Expert Member
Dec 4, 2015
2,323
2,000
Njoo kwa Yesu rafiki hali kama hiyo hautaiona tena, Yesu ndo shuluhisho la Mambo yote,Karibu sana Kwa Yesu rafiki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom