Naombeni msaada please

lonalove

Member
Sep 17, 2016
27
66
Habari zenu wanajamii forum..ndugu zangu hali yangu ni mbaya kiuchumi nikiwa katika wakati huu mgumu wa kusubiri ajira ,nashindwa mpaka kupata mahitaji ya muhimu !.,nimekaa nikafikiria nikaona nianzishe biashara ndogo ya genge japo iweze kunisaidia kwa kipindi hiki kigumu lakini tatizo ni mtaji ,kitu pekee cha thamani nilicho nacho ni hii tecno M3 ambayo ndio naitegemea kupata habari mbalimbali na hata niiuze kupata mtaji pia hautatosha, kwa hiyo naomba mwenye kuguswa na hitaji langu anisaidie chochote hata mia ili niweze kupata mtaji niweze kujishkiza na hii biashara .

Mchanganuo:

-Nahitaji mtaji Wa sh.60,000 kwa ajili ya kuweka kibanda na kununulia bidhaa.

- Sehemu ninayotarajia kufungua genge ni nje ya nyumba ninayokaa ambapo ni kwa shangazi yangu.

-sehemu ninayoishi ni Vijibweni Kigamboni

Hitimisho;
-Najua kuna wengine watachukulia kama ni utapeli ,naheshimu mawazo na mitazamo yao ,lakini nawahakikishia kuwa hii ni shida imenibana mwenzenu na najaribu kuwashirikisheni mnisaidie kama si kwa hela hata kwa ushauri Mzuri utakao nifaa..Kwa atakaye guswa naomba ani PM .Ahsanteni.
 
Weka elimu yako ili wajue umesomea mambo yap iwe rahis kukusaidia , kukikucha ntaku PM
 
Kama wazazi wako kijijini ni heri shambani, patakutoa fasta, mjini hapa bila kazi maalum ni hatareee
 
Umeshajua utauza nini na nini na kipi au kipi kinauzika zaidi katika hayo maeneo unayoishi?

Wapi utanunua na faida utakayopata ukikata mengine kama usafiri n.k.?

Na muda utakaoendesha biashara yako utakapoanza?

....

Njoo PM labda ukiandika habari zaidi huwezi jua.
 
Avatar yako mbona nzuri sana na wewe mwenyewe ndio Lona Love enh! Ila Pole sana kipindi hiki kila mtu kakaza unachohitaji ndio watu wanakitafuta but kuna wao wenyewe utawala huu wanapeta mno na wanawapa watu wengine shida mno... so ndio maana hali inakuwa ngumu kwa wengi... Tumetoka Rwanda tunaelekea China
 
Habari zenu wanajamii forum..ndugu zangu hali yangu ni mbaya kiuchumi nikiwa katika wakati huu mgumu wa kusubiri ajira ,nashindwa mpaka kupata mahitaji ya muhimu !.,nimekaa nikafikiria nikaona nianzishe biashara ndogo ya ngenge japo iweze kunisaidia kwa kipindi hiki kigumu lakini tatizo ni mtaji ,kitu pekee cha thamani nilicho nacho ni hii tecno M3 ambayo ndio naitegemea kupata habari mbalimbali na hata niiuze kupata mtaji pia hautatosha, kwa hiyo naomba mwenye kuguswa na hitaji langu anisaidie chochote hata mia ili niweze kupata mtaji niweze kujishkiza na hii biashara .

Mchanganuo:

-Nahitaji mtaji Wa sh.60,000 kwa ajili ya kuweka kibanda na kununulia bidhaa.

- Sehemu ninayotarajia kufungua genge ni nje ya nyumba ninayokaa ambapo ni kwa shangazi yangu.

-sehemu ninayoishi ni Vijibweni Kigamboni

Hitimisho;
-Najua kuna wengine watachukulia kama ni utapeli ,naheshimu mawazo na mitazamo yao ,lakini nawahakikishia kuwa hii ni shida imenibana mwenzenu na najaribu kuwashirikisheni mnisaidie kama si kwa hela hata kwa ushauri Mzuri utakao nifaa..Kwa atakaye guswa naomba ani PM .Ahsanteni.

Habari.
I hope upo serious maana mambo ya JF wakati mwingine ni mauza uza tuu.
Umesomea nn, na ktk ngazi gani.
Nipo mitaa ya kigamboni pia, na natarajia kuanzisha project flan muda mfupi ujao.

Tuwasiliane na huwezi kujua.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Hivi kwa nini hamtaki kurudi kijijini? Mbona mi ni graduate na nimeamua kurudi tu kijijini baada ya kukaa Dar mwaka mzimas nikiishi kama bundi na sasa huku nalima na naona kabisa ndani ya miaka miwili ntakuwa level nyingine kabisa. Rudi kijijini utajiuza bure mdogo wangu
 
Back
Top Bottom