verizon na spirit zinaweza kufanya kazi bt nilazima ununue pin online 40-50 us na haziwezi nunua tigopesa wala kujiunga na kifurushi chochote
Mkuu usijaribu kununua simu ya sprint, Verizon, au boost maana hazita Fanya kazi Tz
Kwenye at&t na T-Mobile kama ni unlocked zitafanya kazi na nyingi hata kama ni locked basi zinaweza kuwa unlocked na Ku function Tz
kaka unajua kama band ya t-mobile ni 1700? simu iliyotengenezwa special kwa ajili ya t-mobile ni hardware locked hata uende kwa nani huwez ifungua hadi ubadilishe motherboard
duh sijui umesema nini na wewe! Kama simu haifanyi yote hayo ni ya kazi gani! Okoa nguvu na muda sema asinunue verizon, sprint au boost
kwanza simu za verizon na sprint nyingi ni cdma (haziingizi chip) sijui kama bongo simu za hivi zinatumika
at&t na t-mobile nyingi ni gsm ndio maana mara nyingi zinaweka kuwa unlocked.
Unlocking code inategemea na site unayonunua zingine unaweza zipata hata kwa $5, kwa apple na nokia hata bure unapata codes zake
mbona me na bbry verizon na nagonga chip zote
Bado hata sijaelewa
Unaweza kununua simu imeandikwa at&t au verizon au sprint na ukija bongo ukaitumia bila shida??
Msaada tafadhari
chief-mkwawa, @c6, CYBERTEQ, privacy, mwl rct njunwa wamavoko
Mkuu Bulldog Nilipotea humu kwa muda ila jibu la moja kwa moja kwa swali lako ni gumu...!! Kuna yes na no yote ni kutegemeana na Brand ya simu pia Carrier husika..!!
Kigezo cha Bands kama waliotangulia kukitaja ni muhimu ili kupata mtandao lakini pia angalia kuna ambazo utapata mtandao lakini requests zote za kwenye phone app kama kurecharge account yako kwa vocha au hata kununua vifurushi na hizi huduma za kifedha utashindwa kuzitumia kutokana na kutokuwa na mifumo hiyo katika Carrier husika.
****
Kibongo bongo nitakushauri zaidi angalia T-Mobile pamoja na At&T pia uwe na uhakika kuwa ni simu ambayo itakubali ui unlock (chukua ambayo ipo tayari unlocked)
haya spoon feeding sasa.
kwanza angalia simu unayotaka kuinunua jina lake.
mfano inaitwa galaxy bulldog
nenda gsmarena kaitafute hio galaxy bulldog uone frequency zake, utaziona kwa juu
ukishaziona band zake hakikisha ina band 2100 (karibia simu zote zina 2100 kasoro chache tu)
ukishahakikisha ina band 2100 sasa ndo unakuja mambo ya ku unlock,
marekani na nchi nyingi zilizoendelea ku unlock simu ni halali, hawa huku bongo ni madalali tu ukiwapa hela nao wanaenda kukulipia hivyo kama unanua kwa mtu unaemjua anaweza kui unlock kabisa akakuletea