Naombeni msaada kuhusu Bima ya nyumba na vyombo vya usafiri

Naombeni msaada kuhusu Bima ya nyumba na vyombo vya usafiri

Wa kusoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
3,454
Reaction score
2,984
Jamani mm nimejenga nyumba na nimenunua pikipiki kama kumi hivi. Naombeni ushauri wa namna ya kuvikatia bima
 
Kuhusu nyumba unasema ina thamani gani mfano kama ni 50m inapigiwa mara 0.15% ndio utakayolipia,ukija office za bima tunakupa form utajaza baadaye tunakupatia policy document ambayo itakuelezea vitu ambavyo viko covered,kuhusu pikipiki unakija na kadi za pikipiki na unatuambia thamani ya pikipiki kama unataka bima kubwa mfano umenunua 1.6m tubakupigia mara 5% pia tuna add 45,000 kwa ajili ya abili mmoja italeta kama 125,000 lakini hapo utajumlisha na VAT 18%ambayo imepitishwa na bunge na kuanza kufanya kazi kuanzia tarehe 1/7/2015
 
Kuhusu nyumba unasema ina thamani gani mfano kama ni 50m inapigiwa mara 0.15% ndio utakayolipia,ukija office za bima tunakupa form utajaza baadaye tunakupatia policy document ambayo itakuelezea vitu ambavyo viko covered,kuhusu pikipiki unakija na kadi za pikipiki na unatuambia thamani ya pikipiki kama unataka bima kubwa mfano umenunua 1.6m tubakupigia mara 5% pia tuna add 45,000 kwa ajili ya abili mmoja italeta kama 125,000 lakini hapo utajumlisha na VAT 18%ambayo imepitishwa na bunge na kuanza kufanya kazi kuanzia tarehe 1/7/2015
Kampuni gani hii mama. i.e tutajie jina la kampuni tukutafute
 
Sisi ni broker tunafanya kazi na makampuni mbalimbali ya bima,tuko hapa oppsite na ocean road hospital jengo ambalo kuna office za tigo na beforward.
 
Sisi ni broker tunafanya kazi na makampuni mbalimbali ya bima,tuko hapa oppsite na ocean road hospital jengo ambalo kuna office za tigo na beforward.

Mi wa Tabora unanisaidiaje! Tutajie makampuni yenye hizo bima.
 
Makampuni yote ya bima kaka jambazi.yana hizo bima kwa hapo tabora unaweza kwenda national insurance office
 
Pls nipigie kesho me nikupe maelekezo mkuu 0752443420 ni kampuni ya bima UAP insurance kaka
 
kama hujui kitu kaa kimya!!! Kwa akili ya kawaida tu unaweza linganisha bima na kamari????!!

Nimepost makusudi nilijua vilaza kama nyie mtakuja. Wewe umesoma Insurance? Kwa taarifa yako hii ni theory na walimu huwa wanauliza katika mitahani,assigment au test lengo likiwa ni risk assessment. Insurance maswali yake mengi ni ya kufikirika maana risk au uncertainity ni vitu ambavyo vipo nje ya measurement wala occurrences. Ndio maana ukimkuta Mwalimu anaepima uelewa kwenye somo hili hatoi hesabu anauliza vitu vya reasoning au logic tuu kwenye mitihani.
 
Nimepost makusudi nilijua vilaza kama nyie mtakuja. Wewe umesoma Insurance? Kwa taarifa yako hii ni theory na walimu huwa wanauliza katika mitahani,assigment au test lengo likiwa ni risk assessment. Insurance maswali yake mengi ni ya kufikirika maana risk au uncertainity ni vitu ambavyo vipo nje ya measurement wala occurrences. Ndio maana ukimkuta Mwalimu anaepima uelewa kwenye somo hili hatoi hesabu anauliza vitu vya reasoning au logic tuu kwenye mitihani.
sasa hapa kilaza ni nani?!! ume beep umepewa za uso!!!
 
Jamani mm nimejenga nyumba na nimenunua pikipiki kama kumi hivi. Naombeni ushauri wa namna ya kuvikatia bima

BIMA fulani ni za lazima katika nchi fulani. Katika nchi nyingine, bima nyingi hata hazijulikani. Isitoshe, gharama ya bima na fidia inayotolewa hutofautiana sana nchi hadi nchi. Lakini kanuni ya msingi ya bima—kushiriki hatari—haibadiliki.

Kwa kawaida, mtu anayemiliki mali nyingi huwa katika hatari ya kupata hasara kubwa. Vivyo hivyo, athari zinakuwa kubwa zaidi wakati mtu aliye na wajibu mkubwa zaidi wa kifamilia anapokufa au kulemaa. Kuwa na bima kwaweza kuondoa mahangaiko kuhusu hatari ya kupoteza mali au kulemazwa na aksidenti.

Lakini, je, ni hekima kukata bima ingawa huenda mtu asidai kamwe malipo? Je, kubeba gurudumu la ziada garini ni kupoteza fedha kwa kuwa huenda gurudumu hilo lisitumiwe? Dereva aweza kuchochewa kununua gurudumu la ziada kwa sababu linamfanya ajihisi akiwa salama. Ijapokuwa malipo ya kifedha hayawezi kugharimia hasara fulani, huenda yakagharimia hasara nyinginezo.

Bima hugharimia hasara zipi?

Aina za Bima

Bima nyingi zinazokatwa na watu huainishwa chini ya bima za mali, wajibu, afya, ulemavu, na bima ya maisha.

Bima ya mali: Kukata bima kwa uharibifu wa mali—nyumba, biashara, gari, au mali nyinginezo—ni miongoni mwa mipango maarufu sana ya kudhibiti hasara. Hiyo ndiyo bima ambayo John, aliyetajwa katika makala iliyotangulia, aliamua kutokata kwa ajili ya karakana na vifaa vyake vya useremala.

Bima fulani za nyumbani hutia ndani bima ya vifaa fulani vilivyo nyumbani. Endapo unakata bima hii, ni hekima kwako kuorodhesha vifaa vyako vya nyumbani vyenye bima, na uvipige picha au kuvirekodi kwenye video ikiwezekana. Orodha hiyo pamoja na makadirio yoyote au risiti za ununuzi wa vifaa hivyo yapasa kuhifadhiwa mahali salama wala si nyumbani mwako. Madai ya bima yaweza kushughulikiwa haraka zaidi ukiwa na rekodi hizo.

Bima ya wajibu: Mtu yeyote anayeendesha gari, anayemiliki nyumba au mali nyingine isiyohamishika, anayeendesha biashara, au kuajiri wengine ana wajibu wa kulipia hasara ya aksidenti. Aksidenti hiyo yaweza kusababisha uharibifu wa mali, majeraha au kifo cha mtu mwingine. Dereva wa gari au mmiliki wa mali au biashara aweza kuwajibika kulipa gharama ya urekebishaji wa mali au ya matibabu au hata kwa ajili ya maumivu na mateso yanayompata mwingine. Katika nchi nyingi waajiri na madereva wanatakiwa na sheria kuwa na bima ya wajibu ili kulipia gharama hizo. Hata mahali ambapo bima si takwa la kisheria, dereva, mmiliki wa mali, au mwajiri aweza kuwa na wajibu wa kisheria au wa kiadili wa kuwasaidia wahasiriwa wa aksidenti au familia zao.

Bima ya afya: Nchi nyingi zina bima fulani inayogharimiwa na serikali ambayo inaandaa malipo kama vile malipo ya uzeeni na kulipia matibabu ya wazeewazee. Lakini, hata katika nchi zenye mpango huo, bima hiyo yaweza kulipia tu sehemu ya gharama za matibabu au yaweza kulipia tu matibabu fulani. Kwa hiyo, baadhi ya watu hukata pia bima binafsi ili kuwasaidia kulipia gharama zinazosalia. Katika sehemu nyingi wafanyakazi wanaweza kukatiwa bima ya afya wanapoajiriwa.

Mipango fulani ya huduma ya afya, kutia ndani mipango ya utunzaji wa afya na mashirika ya huduma ya afya (HMO), huandaa utunzaji muafaka wa kitiba kwa ada fulani ya kila mwezi au mwaka. Mashirika hayo hujitahidi kupunguza gharama kwa kuandaa huduma za kitiba za gharama ya chini na kwa kuzuia magonjwa. Hata hivyo, katika shirika la HMO, mgonjwa huweza tu kuhudumiwa na madaktari fulani tu au kupokea tiba fulanifulani tofauti na bima ya kawaida ya afya.

Bima ya ulemavu na bima ya maisha: Bima ya ulemavu humpa marupurupu fulani mtu aliyejeruhiwa kiasi cha kutoweza kufanya kazi. Bima ya maisha huwasaidia kifedha wale wanaomtegemea mtu fulani endapo anakufa. Bima hizo zimesaidia familia nyingi kulipa madeni na kujiruzuku maishani baada ya mkimu wa familia kujeruhiwa au kufa.

Kupata Watoa-Bima Wenye Kutegemeka

Bima hutegemea mpango wa kulipa fedha sasa ili kupata ulinzi wa kifedha wakati ujao, kwa sababu hiyo biashara ya bima huvutia walaghai wengi sana. Ndivyo ilivyo katika nchi zinazositawi na zile zilizositawi kiuchumi. Kwa hiyo, ni hekima kujihadhari na zile zinazoitwa eti bima za malipo nafuu na mipango mingine ya bima yenye kutiliwa shaka. Wateja wengi sana wenye matumaini wameambulia patupu wakati makampuni hayo yanaposhindwa kulipa madai yao—au yanapotokomea ghafula!

Kama ilivyo na ununuzi mwingineo muhimu, ni hekima kulinganisha malipo ya makampuni mbalimbali ya bima, na mara nyingi kufanya hivyo huokoa fedha. Mathalani, makampuni fulani hutoza malipo ya chini ya bima ya afya kwa wale wasiovuta sigareti na ya bima ya gari kwa wale waliofaulu mtihani wa udereva. Mteja anayetafuta bima anaweza kupataje kampuni ya bima inayotegemeka?

Hatua ya kwanza yaweza kuwa kujua maoni ya watu wengine kuhusiana na makampuni na mawakala mbalimbali wa bima. Huenda marafiki na majirani wakajua ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni fulani au unyoofu na upendezi binafsi kuelekea wateja wa wakala fulani. Ni vizuri kuwa chonjo kusikia habari zinazotaja makampuni ya bima yenye matatizo.

Isitoshe, rekodi ya kampuni na hali yake ya kifedha yaweza kuchunguzwa kwa kusoma miongozo ya kutathmini makampuni ya bima inayopatikana katika maktaba au maduka ya vitabu au kwenye Internet. Miongozo hiyo yaweza kujibu maswali kama vile: Je, kampuni hiyo ni salama kifedha? Je, imekuwa ikitoa bima kwa mafanikio kwa miaka mingi? Je, yajulikana kwa kushughulikia madai himahima na kwa njia ya kirafiki?

Hata hivyo, miongozo ya kutathmini makampuni ya bima haipasi kuonwa kuwa haiwezi kukosea. Kampuni moja ya bima yenye rasilimali za mabilioni ya dola na iliyodumu kwa muda mrefu, ilichukuliwa na serikali juma moja tu baada ya kusifiwa kuwa bora zaidi na kitabu kimoja maarufu!

Kazi ya Mawakala wa Bima

Kwa kawaida wakala wa bima huwakilisha kampuni mahususi ya bima. Dalali, au wakala aliyejiajiri, aweza kuwasiliana na makampuni mbalimbali ya bima ili kujua bima bora iliyopo kwa malipo fulani hususa. Wote wanahitaji kudumisha uhusiano mzuri na wateja ili biashara yao ifaulu. Wakala wa bima anaweza kuwasaidia sana wateja wake akiwa mwenye kutumainika na akipendezwa nao kibinafsi.

Kwanza, wakala au dalali mzuri anaweza kumsaidia mteja kuchagua bima inayofaa kati ya orodha ndefu ya bima zilizopo. Atamweleza pia mteja wake kinaganaga kuhusu bima hiyo. Kama wengi wajuavyo, hati za bima huwa na mambo mengi sana. Msimamizi wa kampuni moja ya bima alikiri kwamba hakufahamu masuala mengine ya bima ya nyumba yake!

Maelezo ya wakala yanaweza kumsaidia mteja aepuke kutamauka. Kwa mfano, bima nyingi za mali na afya zinatozwa ada fulani. Hicho ni kiasi fulani hususa ambacho lazima mteja wa bima alipe—tuseme, kwa ajili ya urekebishaji wa gari au gharama za matibabu—kabla kampuni ya bima haijalipa fungu lake la madai. Wakala anaweza pia kumtetea mteja wake endapo mteja huyo anakosa kulipwa na kampuni ya bima.
 
Back
Top Bottom