Naombeni msaada katika hili

Jan 20, 2020
65
105
Wakuu heshima kwenu wote wana jf , Leo naomba nifunguke ya moyoni niliyo nayo ambayo yana pelekea Mimi kukata tamaa

Jamani watanzania wenzangu na wasio watanzania Mimi ni kijana wa umri wa miaka 30 sasa nimebahatika kusomea afya katika kitengo cha ukunga na uuguzi katika chuo cha sayansi za Afya kilichopo mkoani Mara nimeingia chuoni pale 2015 na kuhitimu 2017 na napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha mpaka kufikia hatua ya kuhitimu salaama kabisa na kufanikiwa kufaulu vizuri sana katika vitendo na theory

Nilipata GPA ya 4.8 ila sasa katika kusoma kwangu mpaka kuhitimu aliyekuwa akinisomesha alikuwa ni msamalia mwema mmoja alie nipigania kwa kila hali na kipindi nimeanza masomo maisha ya mlezi huyo alie nisomesha yalikua yako vizuri swala la ada ya chuoni ilikua haimsumbui saana ile awali kama ilivo kuja kutokea hatua za mwishoni nimesoma pale chuoni ilivo fikia mwaka wa Mimi kumaliza masomo hali ya kiuchumi kwa mlezi alie kua akinisomesha ikabadilika akashindwa kumalizia ada iliyokua imebakia kiasi cha 1.6 milioni ikanibidi niende niongee na uongozi wa chuo waniruhusu nisome nikihitimu nitatafta tempo nifanye kazi ili niweze kumaliza hilo deni la chuo.

Kweli uongozi uliniruhusu mpaka kuhitimu sasa baada ya kuhitimu kila niendako kutafta kazi wanahitaji vyeti original na lesseni na ukumbuke vyeti vimeshikiliwa chuoni

Bado Nina daiwa sasa uwezekano wa kupata kazi ukawa umeshindikana kabisa ikabidi nijichanganye machimboni kuitafta hiyo ada iliokua ikidaiwa kule machimboni nako hali ikawa ngumu zaidi ikanibidi niachane na kazi ile kwa sababu nilikua napata hela ya kujikimu tu haitoshi hata kupunguza deni la chuoni.

Nimehangaika sana lakini sjafanikiwa nawaombeni ndugu zangu mwenye uwezo wa kunikomboa katika hili anisaidie nitawapatia taarifa zote za chuo na mawasiliano ya chuo nitawapa pamoja na sanduku la posta la chuo nitawapa kwa alie tayari kunisaidia kuvikomboa vyeti vyangu

Naombeni mnisaidie plz huwa nahuzunika sanaa napoziona post za ajira zimetoka nashindwa Kuapply kwa sababu sina vyeti yaani kutokuchukua vyeti kumepelekea mpaka nakua na msongo wa mawazo

Halafu kibaya zaidi sina wa kunitia moyo wa wa kunishauri nimekua Mimi kama Mimi tu jamani umli unaenda mnisaidie plz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili la msongo wa mawazo unaotokana na kukosa ajira limekuwa tatizo linalokua siku hadi siku.najua serikali haina uwezo wa kuwaajili vijana.napendekeza serikali iwe inawakopesha vijana kwa miaka 3 mfurulizo huku ikifuatilia kwa ukaribu kile kinachofanywa na vijana ili kuwanusuru vijana.
 
hili la msongo wa mawazo unaotokana na kukosa ajira limekuwa tatizo linalokua siku hadi siku.najua serikali haina uwezo wa kuwaajili vijana.napendekeza serikali iwe inawakopesha vijana kwa miaka 3 mfurulizo huku ikifuatilia kwa ukaribu kile kinachofanywa na vijana ili kuwanusuru vijana.

Ni kweli mkuu waangalie nchi nyingine walipunguzaje hili tatizo kipindi wako in crisis...
 
Back
Top Bottom