Naombeni msaada detailed kilimo cha alizeti

ynna

Member
Jul 13, 2017
59
25
Nipo Njombe vijijini (Kata ya Ikondo) ambako mazao yanakubali bila aina yoyote ya mbolea. Ipi mbegu bora ya alizeti yenye mavuno mengi, na makadrio ya gharama ya uendeshaji (running cost) up to revenue and profit kwa ekari 1.

Natanguliza shukrani za dhati wana JF.
 
Badru26, Mkuu umewahi panda hii mbegu? Nimewahi kusoma humu sifa zake nikavutiwa nayo but napenda pia nijue kama kuna mtu ameipanda na matokeo yake.
 
Dj mat,

Hii mbegu inasemekana inazaa sana, eka moja inatoa gunia zisizopungua 20-30 kama ukipatia hali ya hewa vizuri. Gunia moja la alizeti linatoa karibia lita 33 za mafuta ukikamua. Lita moja unauza kuanzia elfu 2,500 hadi elfu 4,000. Ukiwa na ekari tano unaweza kuanza kuona green pasture mdogo mdogo, inshallah.
 
steveachi, Asante sana nashukuru ndugu ila naomba tena kujua baadhi ya vitu,

1. Umemaanisha gunia la debe ngapi?
2. Mafuta yake yana utofauti wowote na mafuta ya aina nyingine za alizeti? Naona bei kubwa sana.

Asante.
 
ynna,

Gunia la debe saba, huku kwetu Morogoro ndio bei zake. Sijui huko kwenu, inategemea na mazingira mkuu.
 
Duuu biashara ya kilimo cha alzet sijaielewa bro mwaka jana nililima songea heka 23 aina ya Kenya Feza nikaambulia gunia 70 tu. Cha ajabu had sasa lita 2500 sitaki kusikia tena hicho kilimo .Huu ndio ni ushuhuda wangu mimi mkulima
 
Kuna mtu namfahamu alilima heka 2 akapata aisee mavumo aliyovuna ni aibu sana na alikamua mafuta lile dumu la lita 5 tu na lenyewe sijui kama aliuza,sana sana vimakapi vilivyopatikana aliishia kuwalishia ng'ombe wake.

Sema kweli mimi sishauri sana hasa mtu wa mikoa ya kusini kwenye mvua nyingi kulima hilo zao nikujitia hasara tu mm mwenyewe nimepata hasara zaid ya mil 2
 
Mm nililima ekari kumi kutumia hiyo mbegu ya hysun 33 niliambulia gunia 22 yaan nilipata hasara tupu ujue humu watu wengine wanashawishi ili ununue mbegu zao wao wapige hela.alizeti inachangamoto kubwa wakati wa kupukuchua inakubidi uajit
 
Kuna mtu namfahamu alilima heka 2 akapata aisee mavumo aliyovuna ni aibu sana na alikamua mafuta lile dumu la lita 5 tu na lenyewe sijui kama aliuza,sana sana vimakapi vilivyopatikana aliishia kuwalishia ng'ombe wake.
Acha kupotosha watu nimekuona kwenye post hii ya pili unasema mara mtu alilima heka moja huku unasema mbili kama hujawahi kulima acha wanaotaka kujaribu wapate ushauri... hii tabia haiwezi kukusaidia kitu.
 
Back
Top Bottom