Naombeni msaada: Dawa ya kupunguza uzito/unene/kitambi

Nikupe namba ya demu anaapiga vizinga balaa..yani ukiwa nae kila dk 10 ni stress tupu, ulimpenda atakupa stress utapunguaa
 
Chakula chenye wanga kidogo kitakupunguza uzito kwa 70%
Mazoezi yatapunguza uzito kwa 30%

Kwa hiyo acha kula ,ugali,wali,chapati,bagia ,maandazi ,na pendelea kula vyakula vya protini kama samaki,nyama,kuku,na mayai pamoja na matunda na maharage na utapungua vizuri huku ukishiba.

baada ya kuacha wanga anza mazoezi ya kutembea na usikimbie mpaka baada ya kutembea kwa miezi 2
 
Hakikisha unafanya mazoezi kwa juma moja mara 5 siku mbili utapumzika. Anza kutembea kwa Dk 30 kila siku, utakuwa unatembea kwa uchache wa Kilomita 3 kwa siku kisha utaanza ongeza taratibu.
 
Punguza kula, wabongo tuna tabia ya kula milo 3 wakati sometimes hakuna physical activity yoyote unayofanya. Kula kidogo, fanya mazoezi.
 
Wana JF habarini, bila ya kupoteza muda na maneno mengi naombeni mnisaidie ushauri wa dawa nzuri ya kupunguza unene, hasa kitambi.

Nawategemea jamani
Tuanze kwanza hapa,
Una kilo ngapi?
Unataka kupunguza Kilo ngapi?
BMI yako ngapi na unatakiwa kuwa na ngapi?

Ukinijibu hayo nitakusaidia, mimi ni kati ya watu waliokuwa mabonge but as am speaking nimekata kilo 14.

I look good, sina kitambi, nyama zimekaza etc....
 
Sina nyama nyingi ila sema hili tumbo lina vijinyama fulani vya kizembe ndo nataka kudeal navyo mkuu ila sehemu zingine sina shida
 
1.Anza kubeti,
2. kopa mkopo mkubwa kuliko uwezo wako(tafuna yote)
3.Oa mke mcharuko

Hizi ndio njia bora za kupungua, naona mazoezi unayakwepa kwepa.. Njia waliyokupa wachangiaji hapo ndio the best kabisa.. Mazoezi na misosi utapungua taratibu mpka pale unapotaka kisha unaanza kumaintain, ila jambo kubwa mwili hauondoki haraka, jikaze matokeo ni mdogo mdogo.. Tungekuwa tunaishi karibu karibu ningekusaidia, kuna jamaa nilimsaidia sasa hivi yuko safi tu, minyama uzembe imepungua pungua.
 
Thanks nashukuru kwa ushauri
 
Siku nyingine ukitoa thread ujue kabisa kuna majibu negative utapata. Inaudhi sana watu wanakushauri halafu unaleta ujuaji mwisho wa siku watu wanakukejeli tu unakosa unachokitaka.

Mie binafsi nilikuwa na kilo 116 na nimepungua mpk sasa nina maintain kilo 80 na kitambi chote kimeondoka. Ninachofanya nikukimbia kwa wiki kilomita 20 (kwa jumla) sijabadili sana mfumo wa kula ila nimepungua sana. Hayo madawa achana nayo yatakuletea madhara. Ukifanya mazoezi utakuwa shupavu, utaunguza mafuta, utapungua mwili, utopata magonjwa kama malaria, typhoid na utajiepusha na magonjwa ya mifumo ya maisha kama presha, kisukari n.k

Ukitaka matokeo mazuri jikane na fanya mazoezi. Ni ngumu sana lakini uzuri siku hizi kuna watu wengi wanafanya mazoezi ukijiunga nao watakutia moyo. Wengi wanashauri hivyo na ndio njia bora kuliko zote usiwabeze na ukipenda kusikia unachotaka kusikia.

Ukiona asilimia kubwa wanashauri kitu hicho hicho ujue ndio chenye ukweli. Achana na hayo madawa sijui ya Forever Living utapigwa tu hela. Kina Obama, Bill Gates, wacheza Sinema, kina Kanye West na mkewe wote wanafanya mazoezi kufanya miili yao iwe kama unavyoiona. Kama vidonge vingekuwa vinasaidia hao wenye fedha wote si wangetumia vidonge tu
Naunga mkono hoja tizi ndio kila kitu mie pia hiwa nakimbia kila siku kilomita tano kitambi kimepungua na sifanyi diet na pia kama hakuna jua sehemu yenye kilomita chini ya tano sipandi gari natembea
 
Naunga mkono hoja tizi ndio kila kitu mie pia hiwa nakimbia kila siku kilomita tano kitambi kimepungua na sifanyi diet na pia kama hakuna jua sehemu yenye kilomita chini ya tano sipandi gari natembea
Hiv kuruka kamba nayo inaweza ikawa effective kama kukimbia? Kwa kuwa ratiba yangu iko tight na siwez kukimbia saa 11 usiku kwa maeneo yangu huku.
 
Back
Top Bottom