Naombeni kujua kuhusu hili

Naombeni kujua kuhusu hili

laurent lecky

Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
8
Reaction score
2
Naombeni kujua mwanafunzi anayesoma combination ya HGE anaweza kuja kufanya kazi gani baadaye????
 
Ndugu combination haiamui kazi ya kufanya,kinachoamua ni mazingira ya wakati husika na kozi utakayosoma ingawa hapa kwetu hata hiyo kozi haiamui kazi utakayofanya.Mainjinia leo ndiyo wanasiasa,kwa kukusaidia HGE inaweza kukusaidia kuwa mchumi,mwalimu,mhasibu,lecturer,banker,mfanyabiashara,afisa masoko,na mjasiriamali kwa uchache.Piga shule kwanza mambo ya kazi utayakuta mbele kwa mbele.
 
Naombeni kujua mwanafunzi anayesoma combination ya HGE anaweza kuja kufanya kazi gani baadaye????
Unaweza kuwa polisi, mwanajeshi, mkulima, mjasiriamali kwa kifupi unaweza kuwa na kazi za aina nyingi tu
 
Naombeni kujua mwanafunzi anayesoma combination ya HGE anaweza kuja kufanya kazi gani baadaye????
hata kuzibua vyoo tu mkuu,mambo ya kufanya kazi kwa kufuata ulichosomea huku bongo utachelewa kufanya maendeleo,wewe soma maliza uje uraiani,kazi utakayokutana nayo ukihisi unaiweza basi komaa nayo hiyo hiyo,ukitaka kufuata eti ulisomea combinations sijui nini,huku mbele utakutana na changamoto ya ukabila kwenye ajira,au uwe na wa kukushika mkono...
 
Hakuna kazi anayopata kwa HGE..... Bali hiyo comby itamuwezesha kusomea course fulani fulani chuo, ambazo hizo course ndizo zitakazomuwezesha kupata kazi fulani.

So kwa HGE anaweza kwenda chuo kusomea a wide range of courses..... Kama unataka kuzifahamu pitia admission guidebook ya mwaka huu ili uweze kujua anaweza kusoma courses zipi chuo kikuu.
 
Kazi yakwanza nikuiandaa akili yako kuwa changanuzi na kuifunza kuzitambua fursa kwenye mazingira yanayokuzunguka, kazi hii utaianza pale tuu unapoanza kuisoma hiyo combination. Baada ya hapo ni malundo ya kazi kama unavyoifahamu Tanzania, ambazo hapo utachagua wewe, ila zote zitatokana na hizo kazi mbili ulizofanya hapo awali.
 
Back
Top Bottom