Ndugu wana jamvi kunakijana mmoja namsomesha yupo SUA mwaka wa 1 mkopo wake wa chuo ulienda udsm sasa amefungua chuo tarehe 09.11.2015 akafika chuoni nimelipia taratibu za usajiri kila kitu nikamuachia na hela ya kutumia akaniambia ngoja aufatilie mkopo wake ila Afisa wao wa mikopo amesema watu wa tatizo kama la huyu Dogo wanajulikana kama transfer hivyo asubiri siku 60 Kiukweli niliziona nyingi sana hivi hizi zama za hapa kazi tu unatoa siku 60 unategemea huyu mtu aishije?Basi nikashukuru mungu nikampa Dogo laki tano atumie ,ndugu ikafika 9 .01.2016 siku 60 zimekamilika lakini Bodi ya mikopo wakawa bado hawajampa Dogo mkopo wake alivyodai basi nikampa laki 4 ili aendeleze maisha jamani mpaka Jana nampigia cm Dogo anasema hata allocation bado haijafika chuoni kwake hivi ni kweli au ananilia pesa zangu naombeni majibu wakuuuu inawezekana?Na Luna Rafiki yangu mdogo wake anasoma IAE anatatizo kama la Dogo anasema bado hawajapata ni kweli wakuuu? Jamaaa kamuambia mdogo wake kuwa huku nasikia napenda kumnukuuu' Wewe ni mwanaume hivi hao Bodi ya mikopo mpaka Leo ?Usinifanye mjinga hata Mimi nimesoma kila siku tunasikia matangazo TV na Radio wanafunzi wote wamepata mikopo wewe mpaka Leo huuu ni wakati wa kuamua na sio kuniomba pesa (kulalamika) nimechoka kawaombe loanbord mwisho wa kumnukuuu.Dogo Amelia sana akaniomba nimsaidie nimempa elfu 20.Swali wanajamvi hili tatizo ni kweli au madogo wanakula pea zetu?