Mello
Senior Member
- May 7, 2017
- 110
- 207
Aliyekua mke wangu Kisha tukaachana Miaka 7 iliyopita, Tulibahatika kupata mtoto mmoja, mwaka jana akaamua kuchepuka na mwanaume mwingine na Kupata Mimba, sasa hivi karibuni amejifungua kwa Operation na Kupoteza Mtoto Ilikua ni yeye au mtoto mmoja kati yake Apone au Afe. Bahati mbaya au Nzuri Yeye amepona na kwa masikitiko mtoto amefariki akiwa tumboni. Sasa, kwanza hajaniambia hilo tukio pengine kwakua Bado yuko Hospital, wala hakuna ndugu yake aliyenipigia, Je, naweza kumpigia simu na kumtakia pole kwa hilo lililotokea? Maana amebaki kua mzazi mwenzangu na kwakua ananitunzia mtoto. Nipo njia panda.