Naomba ushauri wenu, napitia mtihani mkubwa nahisi mbele utakuwa mkubwa zaidi

Baada ya kufunga ndoa na mke wangu umri miaka 18, mwezi mmoja baada alianza kuumwa ugonjwa wa kuishiwa damu ambapo kabla niliambiwa ni tatizo alilokuwa nalo toka utotoni sasa lilikwisha pona haya maneneo niliambiwa kabla sijamuoa lakini baada ya ndoa tatzo likarudi akawa ni wa kuishiwa damu nyingi kwa njia ya kublead yaan akiwa period.

Ikatokea migongano ya wazazi wetu pande zote baada ya wazazi wangu kumpeleka kwa mganga wa kienyeji na mganga kuwaambia huyu mtoto alilogwa toka utotoni na hawezi kupona maana hata madaktari walifanya vipimo na kukutwa hana tatzo lolote katika mfumo wa uzazi bas hapo nikawa nimemrudisha kwao kwa shinikizo la wazazi wangu ili akapatiwe dawa za kienyeji mpaka apone.

Amekaa kwao kwa miezi minne huku wazazi wetu wakiwa katika mvutano. Wazazi wangu wakitaka niachane nae na nisimrudishe maana wazazi wake wanakatakataa kuwa mtoto wao hakulogwa wala nini.

Mama alijaribu kunisihi sana kuwa nimuache huyu mtoto kwao na kama kuoa bas ntaoa mwingine.

Sikuweza kumuelewa mama maana binti nlikuwa nampenda maana alikuwa na tabia nzuri na dini pia.

Baada ya kuwa nawasiliana na mke wangu mara kwa mara na kumuuliza hali yake akawa ananiambia kwa sasa yupo sawa na hana tatzo la damu wala tumbo tena.

Basi mapenz yalinijawa ghafla mwezi ulopita nkaamua kwenda kijijini kuwaomba wazazi ridhaa nimfuate mke wangu maana bado nampenda na mm na yeye hatukugombana.
Baba zangu wadogo na babu walikubali ila mama akakubali shingiupande kwa kusema hapana huyo hajapona watakuwa wanakudanganya.

Wazee wakajaribu kumshawishi mwsho wa ck akukubali shingo upande na mm nkaondoka na kumfuata mke wangu kwao bila kipingamizi chichote wazaz wake wakanipa mke wangu nkarudi nae.

Kinachonstua tushaenda hospitalini zaidi ya mara tatu na anapigwa utrasound ya kizaz madactar wanasema hakuna tatzo lkn mpaka sasa hv mke wangu kapungukiwa 60% ya damu na bado tumbo linamuuma kuliko hata mwanzo lkn tatzo halionekani.

Nimewaza sana mpaka sasa nimeshaingia gharama kubwa natibisha ugonjwa nsio ufahamu na kumbuka kwa tatzo lake hili wataalam walisema hawezi kushika mimba.

Naaza kuyaona maneno ya mama usoni kwangu na kuwaza namna ntakavyo mrudisha huyu mtoto kwao akatibiwe na dawa za kienyeji mpaka apone maana naona mzigo unaenda kuwa mkubwa na mm sio mzoefu katika ndoa.

Naombeni ushauri wenu sitaki matusi wala kejeli ntasikiliza ushauri wenu wadau na ntachukua kitakachopaswa kuchukuliwa.

Nawasilisha...
Kama nikweli isiwe ni stor tu, Naamini inawezekana kuna nguvu za giza zinamtaabisha tena unaweza kuta alitolewa sadaka au kuna majini yana nyonya damu yake atasumbuka hivyo wee itakua inaongezeka na kupungua afu mwisho wa siku utampoteza maana huyo tayar anatawaliwa na mamlaka ya giza, Kuna watu wanaoitwa wakuu wa Giza hawa sio mashetani ni wanafamilia baba,mjomba, shangazi nk yeyote kwenye familia anaeweza kuwa kisababishi cha kuitesa familia au ukoo mzima, tatizo la huyu binti linaweza kuwa ni kutoka kwa mkuu wa ukoo, ila pia yamkini mapepo hayo hayamruhusu kuwa na ndoa au kuishi kwenye ndoa ndiomaana baada ya kufunga ndoa tu tatizo limeibuka kwa speed.
SOLUTIO
Mtafute mtumiahi wa Mungu wa kweli mwenye mamlaka ya Kitume, au kanisa lenye mtembeo wa kitume, ila wasiwe mitume janja janja hawa watakuhudumia mwishowe uone maombi hayasaidii, na watakimbilia kukutoza Pesa. MAOMBI NI BURE, kwa huruma tu sikutaka ni recommend uende kwa mtumishi gani nisije onekana nampigia debe ila wewe nitakwambia ni Mtumishi yupi ana mamlaka ya kuvunja mizizi na mashina ya nguvu za giza. Sio watumishi wote wenye mamlaka hizi. Uta ni dm nikuelekeze
 
Pole sana bro, hii naishuhudia hadi sasa katika moja ya mihangaiko yangu, dunia ina mengi zaidi ya tuyajuayo. Bro usimuache mkeo bali msaidie mkeo, zunguka.
Naongeza .Hakika pambana tu jaribu kuvaa viatu vya mkeo vipi atajiskia utakapomuacha kwasababu tu ya maradhi. Wapo waombezi dini tofaout tofaut zunguka ni mtihan huo ila Mungu atakuvusha.
 
Upungufu wa damu hautokani na kurogwa labda mkeo ana sickle cell anemia. Acha kuwasikiliza Wazazi wako kuhusu ndoa yenu vinginevyo watakuharibia ndoa.
Baada ya kufunga ndoa na mke wangu umri miaka 18, mwezi mmoja baada alianza kuumwa ugonjwa wa kuishiwa damu ambapo kabla niliambiwa ni tatizo alilokuwa nalo toka utotoni sasa lilikwisha pona haya maneneo niliambiwa kabla sijamuoa lakini baada ya ndoa tatzo likarudi akawa ni wa kuishiwa damu nyingi kwa njia ya kublead yaan akiwa period.

Ikatokea migongano ya wazazi wetu pande zote baada ya wazazi wangu kumpeleka kwa mganga wa kienyeji na mganga kuwaambia huyu mtoto alilogwa toka utotoni na hawezi kupona maana hata madaktari walifanya vipimo na kukutwa hana tatzo lolote katika mfumo wa uzazi bas hapo nikawa nimemrudisha kwao kwa shinikizo la wazazi wangu ili akapatiwe dawa za kienyeji mpaka apone.

Amekaa kwao kwa miezi minne huku wazazi wetu wakiwa katika mvutano. Wazazi wangu wakitaka niachane nae na nisimrudishe maana wazazi wake wanakatakataa kuwa mtoto wao hakulogwa wala nini.

Mama alijaribu kunisihi sana kuwa nimuache huyu mtoto kwao na kama kuoa bas ntaoa mwingine.

Sikuweza kumuelewa mama maana binti nlikuwa nampenda maana alikuwa na tabia nzuri na dini pia.

Baada ya kuwa nawasiliana na mke wangu mara kwa mara na kumuuliza hali yake akawa ananiambia kwa sasa yupo sawa na hana tatzo la damu wala tumbo tena.

Basi mapenz yalinijawa ghafla mwezi ulopita nkaamua kwenda kijijini kuwaomba wazazi ridhaa nimfuate mke wangu maana bado nampenda na mm na yeye hatukugombana.
Baba zangu wadogo na babu walikubali ila mama akakubali shingiupande kwa kusema hapana huyo hajapona watakuwa wanakudanganya.

Wazee wakajaribu kumshawishi mwsho wa ck akukubali shingo upande na mm nkaondoka na kumfuata mke wangu kwao bila kipingamizi chichote wazaz wake wakanipa mke wangu nkarudi nae.

Kinachonstua tushaenda hospitalini zaidi ya mara tatu na anapigwa utrasound ya kizaz madactar wanasema hakuna tatzo lkn mpaka sasa hv mke wangu kapungukiwa 60% ya damu na bado tumbo linamuuma kuliko hata mwanzo lkn tatzo halionekani.

Nimewaza sana mpaka sasa nimeshaingia gharama kubwa natibisha ugonjwa nsio ufahamu na kumbuka kwa tatzo lake hili wataalam walisema hawezi kushika mimba.

Naaza kuyaona maneno ya mama usoni kwangu na kuwaza namna ntakavyo mrudisha huyu mtoto kwao akatibiwe na dawa za kienyeji mpaka apone maana naona mzigo unaenda kuwa mkubwa na mm sio mzoefu katika ndoa.

Naombeni ushauri wenu sitaki matusi wala kejeli ntasikiliza ushauri wenu wadau na ntachukua kitakachopaswa kuchukuliwa.

Nawasilisha...
 
Mkuu acha kutuangusha bn aisee, ugonjwa hausababishi mke kukimbiwa aisee, matatizo hutokea kwa watu wote

Hebu chukualia mfano ungekua ni wewe umeugua alafu unatelekezwa hivyo????.....unajua hakuna aombaye maradhi wala shida, sasa lakini yatampata nani matatizo kama sio sisi tunaopatwa na mazuri pia???

Mazuri ni yetu na matatizo ni yetu pia kikubwa ni kutafuta njia ya kutoka katika tatizo na sio kukwepa majukumu

Tafuta pesa hudumia mke, kama ni mipango ya Mungu basi mauti ikimkuta iwe nyumbani kwako kiume mzee, sio kutelekeza mwanamke ndugu

Hebu wazia kwa upande hata wa mmoja wa wanafamilia wako kufanyiwa hvyo na mumewe unachukuliaje??

Kama ulimpenda Akiwa mzima basi mpende Akiwa na matatizo pia na M/Mungu atakuridhia kwa wema utakaofanya kwa mkeo
 
pole kwa matatizo lakini tatizo kubwa zaidi ni nyinyi kwenda kwa washirikina kutafuta nafuu basi hiyo imewazidishia majanga zaidi, unitafute private tushauriane...
 
Ukute umempeleka dispensary unasema hospital kubwa.Inaitaji roho ngumu na busara zaidi mana shinikizo la mama ukiwa dhaifu hutolishinda.
 
Baada ya kufunga ndoa na mke wangu umri miaka 18, mwezi mmoja baada alianza kuumwa ugonjwa wa kuishiwa damu ambapo kabla niliambiwa ni tatizo alilokuwa nalo toka utotoni sasa lilikwisha pona haya maneneo niliambiwa kabla sijamuoa lakini baada ya ndoa tatzo likarudi akawa ni wa kuishiwa damu nyingi kwa njia ya kublead yaan akiwa period.

Ikatokea migongano ya wazazi wetu pande zote baada ya wazazi wangu kumpeleka kwa mganga wa kienyeji na mganga kuwaambia huyu mtoto alilogwa toka utotoni na hawezi kupona maana hata madaktari walifanya vipimo na kukutwa hana tatzo lolote katika mfumo wa uzazi bas hapo nikawa nimemrudisha kwao kwa shinikizo la wazazi wangu ili akapatiwe dawa za kienyeji mpaka apone.

Amekaa kwao kwa miezi minne huku wazazi wetu wakiwa katika mvutano. Wazazi wangu wakitaka niachane nae na nisimrudishe maana wazazi wake wanakatakataa kuwa mtoto wao hakulogwa wala nini.

Mama alijaribu kunisihi sana kuwa nimuache huyu mtoto kwao na kama kuoa bas ntaoa mwingine.

Sikuweza kumuelewa mama maana binti nlikuwa nampenda maana alikuwa na tabia nzuri na dini pia.

Baada ya kuwa nawasiliana na mke wangu mara kwa mara na kumuuliza hali yake akawa ananiambia kwa sasa yupo sawa na hana tatzo la damu wala tumbo tena.

Basi mapenz yalinijawa ghafla mwezi ulopita nkaamua kwenda kijijini kuwaomba wazazi ridhaa nimfuate mke wangu maana bado nampenda na mm na yeye hatukugombana.
Baba zangu wadogo na babu walikubali ila mama akakubali shingiupande kwa kusema hapana huyo hajapona watakuwa wanakudanganya.

Wazee wakajaribu kumshawishi mwsho wa ck akukubali shingo upande na mm nkaondoka na kumfuata mke wangu kwao bila kipingamizi chichote wazaz wake wakanipa mke wangu nkarudi nae.

Kinachonstua tushaenda hospitalini zaidi ya mara tatu na anapigwa utrasound ya kizaz madactar wanasema hakuna tatzo lkn mpaka sasa hv mke wangu kapungukiwa 60% ya damu na bado tumbo linamuuma kuliko hata mwanzo lkn tatzo halionekani.

Nimewaza sana mpaka sasa nimeshaingia gharama kubwa natibisha ugonjwa nsio ufahamu na kumbuka kwa tatzo lake hili wataalam walisema hawezi kushika mimba.

Naaza kuyaona maneno ya mama usoni kwangu na kuwaza namna ntakavyo mrudisha huyu mtoto kwao akatibiwe na dawa za kienyeji mpaka apone maana naona mzigo unaenda kuwa mkubwa na mm sio mzoefu katika ndoa.

Naombeni ushauri wenu sitaki matusi wala kejeli ntasikiliza ushauri wenu wadau na ntachukua kitakachopaswa kuchukuliwa.

Nawasilisha...
Acha kubishana bishana.Huyo ni mkeo.Ulikula Kiapo pale kwamba utakuwa naye kipindi chote cha raha na shida,ugonjwa na uzima.Nenda ocean road hospital akapime saratani ya kizazi,msije mkachelewa
 
Yaani una ndugu magaidi kushinda hata Mbowe aliekamatwa yaani umteme mkeo kisa ugonjwa huo ni ugaidi kushinda hata uterorist.Hapo ndo pa kujipatia tuzo mbinguni komaa nae mpaka mwisho la sivyo atakuja kufa kwa kumuongezea stress plus ugonjwa wake kisa hayo mandugu majinga.
 
Huu ni mtihani kama mitihani mingine, jisogeze kwa mola wako, muombe akufungulie, tatizo liishe.. Naamini kuna mambo ya kiswahili(sihri) sasa mambo ya kichawi kuyateketeza kwa imani ya mungu unahitaji uwe na imani kweli kweli, sio wa vugu vugu.. Sijajua dini yako, ila unahitaji kumuomba mola wako akufanyie wepesi.. Ama lah, uende kwa mganga ambako huko kuna 90% ya kupigwa maana mganga nae sio mungu, kuna matapeli kibao.

Kama ni muislam, funga sunna, amka usiku umuombe mola wako, tafuta masheikhe wamsomee dua, sio masheikhe ubwabwa, sheikhe ambae hata wewe unahisi hana makando kando, usafi wa mtu unasaidia dua kuitikiwa kwa haraka, wasikilize na wataalam wa afya pia, huenda mungu akakufanyia wepesi
Tiba ya ruqya kwasasa ni kubahatisha.
 
Ma shaa allah. Ushauri mzuri hasa huko mwisho
 
YESU NDIO JIBU LA SHIDA NA CHANGAMOTO ZAKO ZOTE
NYINGINE ZOTE NI MBWEMBWE TU

binafsi nimeona YESU akifanya sio kwenye maisha yangu tu hata kwa wengine ni kweli na hakika hilo ni jambo dogo sana tena sana kwa Yesu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom