R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,295
- 5,458
Habari za wakati huu wakuu.
Nahisi nitazeeka kama si kufa bila kutumia usafiri wa anga na wa majini.
Sijui ni kitu gani kimenikuta ila hiyo aina ya usafiri sijawahi kupanda na wala sifikirii kama ipo siku nitakuja kupanda maana nafsi yangu inahisi kama vile siku nikipanda nitakufa kabisa.
Siku moja mwaka 2002 nilipanda pantoni pale kivukoni kuelekea kule kigamboni ilipofika katikati kuna boat ya azam ilikatiza sasa ilileta mawimbi kiasi fulani ikapelekea ile pantoni ianze kuyumba mpaka watu wakaanza kupiga makelele kama vile boat inataka kuzama.
Ila kwa upande wa ndege ndio sijawahi kabisa mara kwa mara kuna jamaa yangu yupo France huwa ananialika niende kutembea kule lakini naogopa sana kupanda ndege wakuu hata mambo ya biashara zangu huwa kuna business partner wangu ndio anasafiri kwa ajili ya kufuata wateja wa nje ya nchi yaani nipo kama JPM vile ila fadahli hata yeye hapo Zanzibar au Chattle huwa anapanda ndege.
Hivi nifanyaje ili niweze kuondokana na hii hofu ya kutumia hivi vyombo wakuu.