Naomba ushauri wako juu ya mpango huu wa Ujasiriamali

Wernery G Kapinga

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
372
119
Nina mpango wa kuwa mjasilia mali wa kilimo cha viazi (irish potatoes) Mkoa wa Njombe. Nikiwa aktika jitihada za kutafuta mtaji marafiki walinishauri nitengeneze mpango kazi (project plan) halafu nitumie kuomba mkopo kenye taasisi za kifedha. Baada ya kutengeneza na kuchanganua matumizi ya pesa, yafuatayo niliambiwa kufanya ili kupata mkopo huo.

1. Niwe na mali ambayo naweza kuthaminisha kwa mkopo km vile nyumba, gari, kiwanja.
2. Nitafute wadhamini 2
3. Niwe na mwenzangu wa mradi huo. yaani nisiwe peke yangu.
4. Nitafute walao kianzio kisichopungua 100,000/=

Sasa vigezo hivi vinanipa wakati mgumu kutekeleza hasa mali ya kuthaminisha pamoja na kianzio. Mimi ni mgeni njombe ila nilipata bahati ya kutembelea maeneo fulani vijijini na kuona mashamba mengi sana na nikaambiwa naweza kuyakodi na kufanyia shughuli hiyo. na kwa upande wa soko la viazi ni zuri tu hasa miezi ya 8,9 na 10. Hapo ndipo nilianzampango hilo la ujasiria mali.

Ushauri ninaouomba kutoka kwako ni
1. kama unafahamu taasisi ya kutoa mikopo kwa riba na mashart nafuu hasa iliyojirani na njombe
2. Km mdau wa Njombe ulikuwa na wazo hilo, ukiwa tiyari tuuungane tufanye mpango huu au kwa yoyote anayehisi tuungane.
3 Mdau yoyote anayeweza kunisaidi kwa ushauri zaidi na kunikopesha kiazio au ushauri juu ya kianzio hicho

kwa mawasiliano zaidi 0783757008.

Asante
 
Hongera mkuu kwa jitahada zako hadi kufika huko Njombe tayari inaonesha una nia ya dhati kujikwamua. nikuulize tu labda ungeweka wazi kwamba unahitaji kiasi gani cha hela kwa kulima shamba lenye ukubwa gani, na je bei ya kukodi shamba ekari 1 ni kiasi gani?
 
Asante sana mkuu!

kukodi shamba kwa ekari 1 ni sh. 25,000/= sasa nina mpango wa kuanza na ekari 3

Kwa gharama za jumla ukitoa mbegu kwa sababu nilishazilipia kwa mtu, ni sh 500,000/=

kwa maana ya maandalizi ya shamba, mbolea na umwagiliaji (mipira ya maji pamoja na dawa)

Maandalizi ya shamba ni pamoja na vibarua wa kunisaidia.
 
kwanin mkuu kwa kupunguza gharama hasa za umwagiliaji ungelima na kupanda miez ya tisa(september)? sabab na mim nimekaa njombe kwa miaka 2 nikakuta wanalim miez hyo ili mvua isaidie kumwagilia na uvune miez ya wapil na watatu japo supply huwa kubwa kulhjn demand causing low price lakn kwa wew unaeanza mishe ndo ingekusaidia ili upate fedha nyng za kumwagilia mwaka unaofata na ukizingatia njombe hiyo miezi ina joto sana utatumia nguvu nying kumwagilia
kuuza miez ya octoba ni kweli utapata faida nying naweza kusema ni mara 2 na nusu ya cost of production yaan kama umetumia 3ooooo kwenye uzalishaji bac utauza na kupata 75oooo ila sasa mtaji mkonon ni tatizo linalotukumba wengi
so anza na padogo finaly utaanza kilimo cha umwagiliaji
 
Back
Top Bottom