Naomba ushauri wa binti wa kuoa

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,314
10,017
Wakuu hapa nilipo nina miaka 29.
kwa bahati mbaya bado nakaa kwa wazazi lakini ninajitegemea kwa mambo mengi isipokuwa malazi tu.

Nilikuwa nimepanga naishi mwenyewe lakini niliingiliwa na wezi na kuibiwa hivyo niliamua kurudisha mpira kwa kipa ili nijipange upya.Kilichonileta kwenu ni kwamba nimekuwa sina mahusiano ya kimapenzi ya kueleweka yaani naweza kutaka kumuoa msichana fulani lakin baada ya muda nighair na kuona hanifai . Hii ni ile waswahili wanasema ukimchunguza sana bata.

Pamoja n hayo nimekuwa na uhitaji mkubwa wa kuoa maana nahisi nikiwa na mwenzangu ntakuwa makini zaidi na maishaUtata nilionao ni kwamba kuna rafik yangu alinipa namba ya bint fulani ambaye nimewasiliana naye na kuonana naye jana. Huyu binti amenifahamisha ndugu zake ambao naweza kuwauliza ikiwa nitahitaji kumfaham zaidi.

Sasa wazo langu ni kuwa nimeona nifanye juu chini nimuoe huyu binti bila hata kumfaham vizuri , ilimradi nifaham mawili matatu tu kumhusu maana nikisema nisomane naye tabia kwanza naweza jikuta naahirisha kumuoa.Binti amekubali kwa sharti la kupima afya kwanza, ushauri wenu tafadhali.
 
Ndoa zipo tuu ndugu yangu kufanya hivo unaweza kuangukiwa na jumba bovu kisa tuu ulihitaji kuoa
 
Ndoa zipo tuu ndugu yangu kufanya hivo unaweza kuangukiwa na jumba bovu kisa tuu ulihitaji kuoa
Mkuu ni kweli uyasemayo, lakini naona maisha bila mke kwangu yamekuwa changamoto kubwa. Najiona naendelea kuishi kama mvulana tu na si mwanaume. Nataka nijitwishe majukum nikomaze akili
 
Mwanaume unakuaje desperate hivyo, halafu tena una miaka 29 tu...

Ndoa sio mchezo wa bahati nasibu kwamba unajaribu bahati yako...

Ndoa ni moja ya sehemu katika ratiba ya maisha yako...

Kama ambavyo mambo mengine hufanyi kwa kubahatisha ndivyo hata hilo suala la ndoa lapaswa kuwa...
 
Usioe/kuolewa kisa umekaa sana benchi, Usioe au kuolewa kisa tu umeunganishwa, Usioe au kuolewa kisa tu wengine wanafanya hivo. OA au Kuolewa kwa sababu uliyempata ni MTU SAHIHI KWAKO.
Chukua ushauri huu dogo...
 
Back
Top Bottom