Naomba ushauri wa biashara ninayoianza

S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,408
1,713
Wadau,

Mnielimishe kuhusu jambo hili la kibiashara. Nimeanza kutengeneza bidhaa za matumizi ya nyumbani ili kuinua maisha yangu.

Nimepata wateja wa supermarkets ambao wamezipenda na wangelitaka kuzinunua lakini wananiambia hawawezi kufanya hivyo mpaka nitakapokuwa nimezipa bidhaa zangu lebo.

Wameniambia nitakaposhughulikea utaratibu wa lebo ukikamilika basi niwapelekee bila kusita.

Sasa ninaloomba kufahamishwa ni kuhusu utaratibu wa kisheria wa kuipa bidhaa lebo. Sina uzoefu na hilo na hivyo nisingependa kufanya kitu ambacho kitaniletea matatizo hapo baadaye.

Je! Ni vigezo vipi vya kuzingatia kabla sijaipa bidhaa yangu lebo ninayoitaka? nitashukuru kwa msaada wenu kwenye eneo hili.
 
mkuu tafuta bidhaa za kijasiriamali zenye label chukua contact waulize taratibu, pia najua jf hukosi kitu endelea kuvuta subira.
 
brand name unai design alafu unaisajili, bidhaa pia ithibitishwe na TBS, fresh tu mbona
ila ni bidhaa gani?
 
brand name unai design alafu unaisajili, bidhaa pia ithibitishwe na TBS, fresh tu mbona
ila ni bidhaa gani?
Ni bidhaa kama vile Sabuni za Maji (za kufulia, za kuoshea vyombo, za kuoshea vyoo. Pia sabuni za unga na za mche). Hali kadhalika shampoo, losheni na mafuta ya mgando. Hizi ndizo bidhaa zenyewe.
 
Dhibiti kisheria umiliki wa vitu vifuatavyo:
1. Nembo (logo) yako
2. Jina la kampuni yk
3. Jina la bidhaa zako
4. Kaulimbiu (slogan) inayowakilisha kampuni/bidhaa yako.
5. Alama unayotumia kuwakilisha mradi, biashara au huduma unayotoa.

Hii itakulinda kisheria pale mtu, kwa maslahi yk binafsi, atakapotumia vitu hivyo au atakapotaka kufanya hujuma.
Ulinzi huu utaupata kwa kusajili Trademark zako pale Brela
1. Fanya hivyo sasa ili kuepuka usumbufu baadae
2. Fanya hivyo sasa ili kudhibiti/kuzuia mtu mwingine asitumie jina, nembo, ishara au kaulimbiu (slogan) yako.
 
Hakikisha unaisajili logo/nembo yako au jina lako la biashara pale brela. Kwa kufanya hivyo utakuwa unailinda project yako dhidi ya mafisadi ambao wanaweza kutumia trademark yako kwa faida zao binafsi. Gharama ni 135,000/- tu. Malipo haya unaweza kuyagawa na kuyafanya ktk awamu 3. Kimsingi pale brela hakuna usumbufu. Zoezi zima la usajili Wa trademark hadi kukamilika uchukua muda wa takriban miezi 4.
 
Kwa wale wanaohitaji nembo (logo) au product label tafadhali wasiliana nami tuyajenge.

Aidha ili kujiridhisha juu uwezo wangu, unaweza kuangalia baadhi ya kazi zangu ktk album yangu hapa hapa JF au
Cheki baadhi ya kazi zangu hapa:
LOGO DESIGNER
Logoriddim - LOGO Designer

Email: logoriddim@yahoo.com

Contact: (mobile/whatsapp): +255 688 999006

Karibuni sana.
Nimeiona kazi yako. Kwa hakika ni bomba kabisa. Nitawasiliana nawe wakati muafaka ukifika.
 
Back
Top Bottom