Naomba ushauri toyota IST vs VW GOLF

Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,823
2,000
Wakuu naomba mnisaidie ushauri kuhusu gari ist na golf zote za 2005 ili kukwepa dumping fees, naipenda golf kwa muonekano wako lakini je ni gari ambayo nikitaka kuja kuuza itauzika? Na upatikanaji wake wa spare upo?

Toyota ist je ni gari sumbufu? Kama tukiweka golf vs ist huku kichwani tukiwaza uuzikaji, upatikanaji wa spare, muonekano, ubora wa gari je ipi itaibuka mshindi? Natanguliza shukrani Wakuu.
 

mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
Kaka, VW Golf ni gari aina kama Benzi na mtengenezaji ni mmoja. Spea za Golf zinatofautiana kidogo sana na benz kwenye bei. Ukiwa nayo hakikisha unaisukuma kabla haijaanza kusumbua, maana mwisho wake huwa ndoa ya kikatoliki. Kama ni gari yako ya kwanza sikushauri
 

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,399
2,000
Mkuu Vwa kwanza nzito,muda unavyozidi kwenda au muda mfupi tu mlio wa Engine utausikia unabadilika,nchi zetu za joto ni sheeda.
Kuuzika labda uuze milioni moja,hizi gari hakuna mwenye shobo nazo,utauza kwa hasara.
IST mpango mzima,zinauzika na zipo vizuri.
 

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,658
2,000
Kwa jinsi uanvyoongea, hii inaonesha ni gari yako ya kwanza. Na ni vizuri gari ya kwanza ikawa ni gari ya Toyoto. Coz mpaka uje ujue kuendesha vizuri, utakuwa ushabadilisha indiketa, site mirror na kunyosha nyosha sana. Kwa mtu mzoefu wa magari Ki gofl kiko poa. Kwa ujumla me napenda magari unique... Hayatoki kwenye fashion mapema.
 

Kijuso

Senior Member
Jun 23, 2009
161
195
kaka Mwanafyale kuna maneno hapo umeniacha njia panda "ndoa ya kikatoliki" na ''magari ya mafuriko'' naomba kidogo ufafanuzi kidogo hata nami ikifika wakati wa kununua gari nipate kuelewa

Ahsante
 

mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
Magari ya mafuriko ndio yapi? Na je ni sawa ist(2005) ambayo ndio imetoka bandarini haijaendeshwa bongo kuuziwa mil 12?
Kaka, umesahau hv juzi kati Japan ilikumbwa na mafuriko makubwa na kufanya majengo na viwanda na yard zao kusombwa na mafuriko hayo. Sasa magar yaliyokumbwa na mafuriko hayo yalikarabatiwa na kuuzwa mpaka dola 450, bongo magari hayo yamejaa tele kwenye yard. IST kuuzwa 5m, 9m, 12m au hata 20m hiyo ni biashara, ukifika bei unachukua, ukiwa mjanja utahoji. IST mkononi hadi 5m unapata
 

mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
kaka Mwanafyale kuna maneno hapo umeniacha njia panda "ndoa ya kikatoliki" na ''magari ya mafuriko'' naomba kidogo ufafanuzi kidogo hata nami ikifika wakati wa kununua gari nipate kuelewa

Ahsante
Ndoa ya kikatoliki haifunguki/haivunjiki. Kuna magari ukishanunua haliuziki tena, utakufa nalo
 

KINGSLEE

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
650
1,000
Wakuu naomba mnisaidie ushauri kuhusu gari ist na golf zote za 2005 ili kukwepa dumping fees, naipenda golf kwa muonekano wako lakini je ni gari ambayo nikitaka kuja kuuza itauzika? Na upatikanaji wake wa spare upo?

Toyota ist je ni gari sumbufu? Kama tukiweka golf vs ist huku kichwani tukiwaza uuzikaji, upatikanaji wa spare, muonekano, ubora wa gari je ipi itaibuka mshindi? Natanguliza shukrani Wakuu.Golf habar ya mjini kitu speed hadi 260/hr sasa huyi IST atakupata wapi ukienda kwenye mkutano, sherehe like harus e.Tc kitu unique ni kizuri sana
 

Attachments

  • Screenshot_20200904-114621.png
    File size
    766.6 KB
    Views
    0

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom