Naomba ushauri: Toyota CAMI vs Toyota Vitz

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
811
Habari zenu wadau. Nahitaji kununua gari, na Katika Uchunguzi wangu nimeweza kushortlist gari tatu ambazo ni Toyota CAMI, Vitz na Suzuki Swift sababu kuu ya kushortlist ni kwamba zote zinalingana kiu-uwezo kwa CC zake(1300) na hivyo nitaweza kuzimudu kwa uendeshaji wake(Mafuta). Katika Hizo, kuna baadhi ya watu walinishauri niachane na gari za suzuki na kusema ni heri niwe na toyota kwani upatikanaji wa spea ni mkubwa.

Sasa Wadau naomba kwa wenye Uelewa Mzuri na Haya magari juu ya uimara wa magari husika, upatikanaji wa spea zake, uendeshaji na bei zake. Ikiwezekana naomba pia directives za showrooms ambazo ziko cheaper in town.

Natanguliza Shukurani
 
CAMI na VITZ bei zake ni tofauti. CAMI iko juu kwani hii ni SUV kwamba unaweza kuitumia hata kwenye barabara zetu za kibongo zenye mahandaki tofauti na VITZ.
Mimi ningekushauri kama budget yako inakurusuhu chaguo lako liwe CAMI, ukipata CAMi ambayo ni 4wd its well and good. otherwise spares zipo mitaani zinapatikana bila usumbufu.
Kwa show room za kibongo sijui ni wapi lakini kama unasubira ni vema kuagiza moja kwa moja japan. itachukua muda lakini utasave angalau mil hata 2 tofauti na ungenunua hapa bongo.
 
Siku hizi spea za magari kama Suzuki na Nissan sio shida tena kama ilivyo kuwa zamani kwamba mpaka uagize Nairobi. Cami ni 4WD na spea zipo lakini sio imara maana nyingi zinachakachuliwa kwa kuwa zinaingilina na aina nyingine za Toyota nyingine. Suzuki Swift nazo zipo 4WD ingawa sio nyingi, spea zipo lakini bei juu, ila ni imara unadumu nayo. Mimi nina Swift nadunda kama kawaida. Ujue kwamba watu wanapenda magari ya Toyota kwa sababu spea zake ni bei rahisi lakini ni zinachakachuliwa na ni feki na ndio maana utaona kwamba zinaingiliana, kwa mfano Oil ceal ya Toyota unaweza pata kwa 5,000/= unakaa nayo wiki moja, tofauti na Nissan au Suzuki ambayo ni 35,000/= lakini unasahau. Chagua baina ya Toyota Cam na Suzuki Swif, achana na Vitz.
 
Mkuu Toyota Cami = Daihatsu Terios kwahiyo spea zake haziingiliani kabisa na Toyota zingine na ni ghali ila kama alivyosema mdau hapo juu ubora wake ni wa juu zaidi ukinunua unasahau. Pia ni 4WD ba bei yake ni kubwa. Hata mimi sikushauri kununua Bongo ni wachakachuaji sana wa bei na ubora pia. Ni bora ukaagiza mwenyewe utapata kwa bei nafuu na ubora wa juu pia.
 
CAMI na VITZ bei zake ni tofauti. CAMI iko juu kwani hii ni SUV kwamba unaweza kuitumia hata kwenye barabara zetu za kibongo zenye mahandaki tofauti na VITZ.
Mimi ningekushauri kama budget yako inakurusuhu chaguo lako liwe CAMI, ukipata CAMi ambayo ni 4wd its well and good. otherwise spares zipo mitaani zinapatikana bila usumbufu.
Kwa show room za kibongo sijui ni wapi lakini kama unasubira ni vema kuagiza moja kwa moja japan. itachukua muda lakini utasave angalau mil hata 2 tofauti na ungenunua hapa bongo.
Asante sana mkuu. Umenitoa tongotongo kwa utofauti huu.
 
Siku hizi spea za magari kama Suzuki na Nissan sio shida tena kama ilivyo kuwa zamani kwamba mpaka uagize Nairobi. Cami ni 4WD na spea zipo lakini sio imara maana nyingi zinachakachuliwa kwa kuwa zinaingilina na aina nyingine za Toyota nyingine. Suzuki Swift nazo zipo 4WD ingawa sio nyingi, spea zipo lakini bei juu, ila ni imara unadumu nayo. Mimi nina Swift nadunda kama kawaida. Ujue kwamba watu wanapenda magari ya Toyota kwa sababu spea zake ni bei rahisi lakini ni zinachakachuliwa na ni feki na ndio maana utaona kwamba zinaingiliana, kwa mfano Oil ceal ya Toyota unaweza pata kwa 5,000/= unakaa nayo wiki moja, tofauti na Nissan au Suzuki ambayo ni 35,000/= lakini unasahau. Chagua baina ya Toyota Cam na Suzuki Swif, achana na Vitz.

asante swabaho..nimekuwa discouraged sana na magari ya suzuki na jamaa kadhaa niliowauliza. Nachukua ushauri wako katika kufanya maamuzi yangu. Shukrani
 
asante swabaho..nimekuwa discouraged sana na magari ya suzuki na jamaa kadhaa niliowauliza. Nachukua ushauri wako katika kufanya maamuzi yangu. Shukrani

Asante kushukuru, Mkuu. Kama hutojali waweza ni PM ili nikuunganishe na Kampuni ambayo niliagiza Suzuki Swift ya mwaka 2003, niliipata bila shida tena kwa bei nzuri iko katika hali nzuri sana. Nimeipata Oktoba, 2010 lakini mpaka sasa sijatembelea gereji yoyote, tofauiti na kuingia petrol station kuongeza wese au kufanya service ya kawaida.
 
mkuu kweli ushauri huu unalingana na hitaji lake kweli? mtu anauliza ushauri wa kununua vitz au cami tayari umeshajua huyu mtu budget yake kiasi gani...sasa ukimshauri kununua v8 si ni ndoto hizo mkuu...v8 au prado ushuru wake sidhani hata hiyo budget yake ya vitz itatosha hata kuikomboa hiyo gari mikononi kwa serikali. mpe ushauri kuendana na alivyojieleza otherwise utakuwa unamkatisha tamaa mkuu

chukua prado wewe achana na vigari vya watoto ivo...au kamata v8
 
chukua prado wewe achana na vigari vya watoto ivo...au kamata v8

We hata baiskeli unayo kweli? watu wengi wanaopenda kujishow off ni empty kabisa...kakuambia nani kuwa ukipenda wewe prado basi kila mtu anapenda kila mtu ana choice yake mkuu acha hizoo
 
Back
Top Bottom