Naomba ushauri, nina Kesi ya madai

otimbiotimbi

Senior Member
Dec 12, 2019
100
135
Habari za leo ndugu zangu,

Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Summons yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu, Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.

Je, nifanye nini kwa sasa?
 
Muone Wakili, na hapohapo kimbilia Takukuru haya Madeni yenye Riba hewa Waziri wa Fedha na Mipango Bw Mpango alishayakataa tangu Disemba 2019.

yupo jamaa Bukoba alikopa milioni 8 kwa Harusi ya kijana wake na akaaha Kadi ya Benki kila Mshahara ukiingia jamaa anakata rejesho na riba ikafika milioni 67.

akagangamala zimerudi zote kupitia Mkuu wa Mkoa Brigedia Gen Gaguti
 
Muone Wakili, na hapohapo kimbilia Takukuru
haya Madeni yenye Riba hewa Waziri wa Fedha na Mipango Bw Mpango alishayakataa tangu Disemba 2019
yupo jamaa Bukoba alikopa milioni 8 kwa Harusi ya kijana wake na akaaha Kadi ya Benki kila Mshahara ukiingia jamaa anakata rejesho na riba ikafika milioni 67
akagangamala zimerudi zote kupitia Mkuu wa Mkoa Brigedia Gen Gaguti
Hapa utampotosha na hizi siasa!
 
Habari za leo ndugu zangu,

Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Samansi yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu,Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.

Je, nifanye nini kwa sasa?
Wapi ?
 
Hapa utampotosha na hizi siasa!
Wakili ndio hataki pesa? Mawakili sio kwamba atashinda Kesi
utamsababishia apoteze mali zaidi kwa wakili na Hukumu
jamaa lazima ajichanganye atumie Wakili na ubabe atumie pia ndio maana yangu
 
Wakili ndio hataki pesa? Mawakili sio kwamba atashinda Kesi
utamsababishia apoteze mali zaidi kwa wakili na Hukumu
jamaa lazima ajichanganye atumie Wakili na ubabe atumie pia ndio maana yangu
Mhhh! Haya!
 
Mhhh! Haya!
wewe unamsaidiaje? mbona huweki bayana
naomba ufahamu hakuna wezi kama Mawakili na Mahakimu
sasa badala ya Kagera kwa Brigedia angalia hii ya Mh Katambi huko Dodoma juzi tu

otimbiotimbi Pambana Mkuu mvanie Mkuu wa Wilaya yoyote km una hakika mkopo wako una mushkeli na hasa Riba za kubambika, kwanza lazima walipe Kodi TRA hakuna biashara za kukopeshana kiholela kwa riba za 50% angalia dk ya 13:50 anazungumzia Mikopo aliyorudishs ya kitapeli
 
wewe unamsaidiaje? mbona huweki bayana
naomba ufahamu hakuna wezi kama Mawakili na Mahakimu
sasa badala ya Kagera kwa Brigedia angalia hii ya Mh Katambi huko Dodoma juzi tu

@otimbiotimbi Pambana Mkuu mvanie Mkuu wa Wilaya yoyote km una hakika mkopo wako una mushkeli na hasa Riba za kubambika, kwanza lazima walipe Kodi TRAhuu hakuna biashara za kukopeshana kiholela kwa riba za 50% angalia dk ya 13:50 anazungumzia Mikopo aliyorudishs ya kitapeli
Hao wanasiasa hawawezi kuwasaidia kitu. Zaidi sana watayachukua matatizo yenu kujitafutia ujiko.

Juhudi zao za kutatua migogoro ni nzuri lakini haziko katika mkondo sahihi.

Mkuu wa mkoa hawezi kuzuia mambo ya mahakama. Kuna procedures za kufuata, ambazo wakili atazifanya na kuiomba mahakama isimamishe proceedings au execution.

Huu ni ushauri tu kwa wale wanaopenda kukimbilia kwa wanasiasa!
 
Hao wanasiasa hawawezi kuwasaidia kitu. Zaidi sana watayachukua matatizo yenu kujitafutia ujiko.
Juhudi zao za kutatua migogoro ni nzuri lakini haziko katika mkondo sahihi.
Mkuu wa mkoa hawezi kuzuia mambo ya mahakama. Kuna procedures za kufuata, ambazo wakili atazifanya.
Huu ni ushauri tu kwa wale wanaopenda kukimbilia kwa wanasiasa!
naomba nikueleweshe Kesi zote za kukopeshana ki SACCOS /MITAANI hazipokelewi Mahakamani
Mshauri huo ushauri Mleta Mada km hakuuziwa mali zake, ndio atajua Wakili na Hakimu ni kitu kimoja, gharama za Wakila hana kuhonga Hakimu hana, Riba kapandishiwa makusudi wamuunganishe na Dalali wakauze mali wagawane, aende tu kwa Mkuu wa Wilaya ataingilia kati hiyo Kesi ana atapewa muda wa kulipa Principal tu Riba hakuna
Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Samansi yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu,Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.
 
Mimi naona hatujamuelewa, au huenda keshanadiwa mali zake tumsubiri arudi lkn naona Kesi yake ni kwamba kachukuwa pesa kwa mtu ya Riba sasa kachelewesha.

na hii Waziri Mpango alishaikataa hakuna kukopeshana Mitaani kwa aina yoyote na kujiwekea Riba au kutolipa Mapato TRA.

tumsubiri tusiandikie tusivyomuelewa mleta Mada
 
Habari za leo ndugu zangu,

Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Samansi yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu,Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.

Je, nifanye nini kwa sasa?

Kwanini hukulipa nawewe mpaka mtu aende Mahakamani?
Na ulivoona deni si halisi ungekata rufaa.

Anyway nenda kasikilize hiyo kukazia hukumu wewe sasa ndio ujipange kupangua utekelezaji wake..

Kukazia hukumu maana yake, unaulizwa kwanini wauze mali zako.

Ila Kama pia waona umeshindwa hilo badilisha umiliki wa hizo mali, wakija kuangalia majina wakute manyoya...japo si vizuri kwa watu Kama nyinyi msiolipa wenzenu kuwashauri hili, ilitakiwa ukamatiwe Mali zako Kwanza ndio ujifunze kulipa madeni.
 
Habari za leo ndugu zangu,

Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Samansi yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu,Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.

Je, nifanye nini kwa sasa?
Tii wito, nenda Mahakamani ukajue msingi wa madai ili ujue namna sahihi ya kuyajibu.
 
Ni uungwana kulipa madeni ya watu kwa wakati kama mlivyokubaliana ikitokea kuchelewa iwe kidogo tu na siyo kuacha kabisa halafu hata simu akikupigia hupokei au una m block.

Kukopa harusi kulipa matanga.
 
Habari za leo ndugu zangu,

Nimepigiwa simu kuwa mahakamani kuna Samansi yangu kwaajili ya kesi ya madai ambapo mdai wangu anakazia hukumu ili aweze kukamata mali zangu,Deni analodai si halisi kama lilivo katika documents ni kubwa sana.

Je, nifanye nini kwa sasa?

Anakazia? Ina maana hukumu ilishatoka?
 
@otimbiotimbi wewe umetuachia timbwili la nyani huku shambani
umeomba ushauri hata hukurudi kutupa mrejesho au ni Mada ya kutunga
salama mkuu?.Nilienda tarehe 28.05.2020 mahakamani ikapangwa kuwa tarehe 04.06.2020 natakiwa nipeleke majibu ya kwanini wasiuze mali zangu!
 
salama mkuu?.Nilienda tarehe 28.05.2020 mahakamani ikapangwa kuwa tarehe 04.06.2020 natakiwa nipeleke majibu ya kwanini wasiuze mali zangu!
ok na pole sana, hapo kimbilia kwa Wakili akuandikie hayo mapingamizi ni ndani ya siku 14 kam hutayapeleka kesho trh 04/June, kabla ya kuuza mali km nyumba utapewa siku 74, hapo jitahidi kulipa deni hilo kwani ni kubwa sana? na limechangiwa na Riba?

kama kuna uonevu wa kulipandisha likafikia kiwango cha kukutisha/kukukatisha tamaa fuata Viongozi wa Serikali wakakusimamishie riba ulipe taaaratibu upatapo.

kwa sasa hela ni ngumu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom