Rafki yangu, msaada wa kisheria bure bure hutaupata kwani sisi wanasheria truly speaking, we're after money japo maadili ya kazi yanasema kumuhudumia mteja sharti kuwe kwa moyo na jitihada zote kumtetea na kuthibitisha kuwa ana haki au haki yake inanyimwa (denied), haya yote ni baada ya kumlipa mwanasheria. Kwa shauri lako ningependa kukupa ushauri mdogo tu, jaribu kupitia family law, halafu na kwa maelezo yako kila dai sharti litambuliwe na sheria iliyopo (law in force), hivyo matusi yote aliyokutukana ulipaswa kuyaweka hapa bila kupunguza au kuongeza neno lolote kwani wenda matusi unayosema si matusi kisheria na shauri lako kwa mantiki hiyo likawekewa pingamizi la awali (preliminary objection) au kusiwe na shitaka la kujibu kwa mtuhumiwa. "Unapoteza muda wako kwa kunisema kwa mkwe wangu" si tusi kisheria, hivyo kama unanuwia kumshitaki jua sheria ya ushahidi (Law of Evidence Act) kifungu cha 112 kinahitaji yeyote anayedai sharti athibitishe (He who alleges must prove), sasa tunza hizo sms kuwa ushaidi. Huu ndio msaada wangu kwako lakini ukitaka msaada kabisa tafuta mwanasheriaam au nenda moja kwa moja mahakamani. Kazi njema