Ndugu zangu wana JF nina mdogo wangu alipata shida ya meningitis pindi alipokua mdogo lakini inaonekana kua ugonjwa huu ulihathiri mfumo wake wa uongeaji akiongea maneno yake ni kama hayaelewiki kwa wepesi.
Kwa kulitambua hilo tuliamua kumpeleka shule ya mahitaji maalum lakini cha ajabu mpaka sasa yupo la saba na bado hajui kusoma vizuri lakini sign language anaweza vizuri na kizuri yeye anasikia vizuri tu tatizo ni hapo kweny kusoma sasa nimekuja hapa mnisaidie kwenye ushauri nifanyeje make nahitaji asiwe tegemezi hata kidogo kazi kama za nyumbani anajua tatizo ni hili kuongea vizuri na kusoma sasa nilikua naomba mnishauri.
Ni wa kike......akili yake yani yuko normal na uelewa wake wa mqmbo ya kawaida iko vizuri tatizo lipo kweny masomo tu labda nifanye evaluation ya kipaji chake