mwendapole12
Member
- Apr 2, 2022
- 21
- 26
Mmmh.Wewe nunua tu, hayo unayoyatilia shaka ndio yakague uthibitishe ndipo utoe pesa
By the way unabajeti ya shiling ngapi na umeitoa wapi
MAliza mtihan wako wa kidato chaUkitulia ukaweka pupa pembeni ,,basi nakubashiria utapata gari nzuri na utakaa nayo sana ,, mimi nakumbuka wakat naingia kwa mara ya kwanza ulimwengu wa magari ,nilinunua Toyota sienta ,,kwa mzee mmoja wa kichaga,,aisee nilijuta kwann nilinunua gari ,maana sikumbuka kama nishawahi kupata furaha wakati nipo na gari lile ,,kwanza ilikuw na ugonjwa wa kupoteza nguvu ukipanda mlima ,,alaf punde likawa linaleta taa ya check ingine...basi sikukaa nalo sana nikamrudishia mwenyew gari lake nikamwambia natak pesa zangu ,, ilikuwa kuna mvutano kwenye kurudisha pesa ila kilichonisaidia nina mkoba wa uganga wa bi.mkubwa ,,basi nilimpa mwezi mmoja yule mzee atafute pesa aniletee ,,nilichokifanya nikaenda mzimuni kushtakia ,,ebwana yule mzee aliandamwa na mabalaa ,anajua yeye na mungu wake ,,mwisho wa siku akanipigia akanambia kijana nakulipa pesa zako ..basi nikampa account numbee yangu akaingiza mpunga wangu wote ,,, Hapo akili ikanikaa sawa ,,ikabidi nivute pumzi ,,nikaanza kutafuta gari taratibu hadi nikapata Gari nzuri aina ya toyota Alphard Ambayo mpaka sasa nipo nayo na nashkuru Haijawahi kunisumbua ..
Aisee! Unataka kufahamu mpaka alikoitoa?🤣🤣🤣Wewe nunua tu, hayo unayoyatilia shaka ndio yakague uthibitishe ndipo utoe pesa
By the way unabajeti ya shiling ngapi na umeitoa wapi
Pesa ngumu mkuu atuambie tuzifuate hukoAisee! Unataka kufahamu mpaka alikoitoa?🤣🤣🤣
Nimejikuta nimecheka japo sijui kama nilipaswa kucheka.Pesa ngumu mkuu atuambie tuzifuate huko
Ukishlipenda gari kupitia dalali nenda na mmiliki TRA ukajue ABC zake kuanzia umiliki halali, umiliki mara ngapi na mikopo kwenye taasisi za fedha pamoja na uhalali wa nyarakaWakuu habari zane nimeleta uzi huu mnifumbue macho kwa hili nisije kuingia mkenge,
Nataka kununua gari maana nimeendesha pikipiki kwa muda mrefu sasa imetosha bwana naomba.
Ninatazamia kununua gari IST au Vitz mkononi ila changamoto inayokuja nakosa amani na madalali kwani wao wengi unakuta tayari wana document ila la kipengele mawasiliano ya mmiliki wa kwenye kadi hawana.
Nami napata ofu nadhani mtu anaweza kuweka gari bondi akakopa mwisho wasiku akachelewa kulipa fari ikauzwa au mtu akachukua doc za nduguye akaamua kuuza.
Gari sasa nifanyeje ili niweze kununua gari kwa dalali maana magari ni mengi.
Je hayo magari yote yanayouzwa na mdarali wanaoenda kuyatumia wanafanyeje ikifika wakati wa kufanya transfer ofu ownership?
Hapa si TRA wataleta pua zao kutaka Kodi.Kwenye ownership transfer lazima uwe na kopi ya NIDA ya mmliki (jina kama linavyooneshwa kwenye kadi) picha yake passport size na pia lazima Ofisa wa TRA atampigia simu mmiliki wa gari kupata ridhaa yake ya kubadilisha umiliki.
Lazima ulipe 50K ya transfer kwa gari ndogo,ukiwa na mkataba wa mauziano wa mwanasheria wenye EFD risiti hawana cha zaidi.Hapa si TRA wataleta pua zao kutaka Kodi.