Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Hakuwezi kuwa na uhusiano kati ya kikohozi cha sasa akiwa na miaka 6 na kupaliwa maji ya sabuni miaka mi5 iliyopita. Huwa mnampeleka hospitali? Ameshaonwa na Paediatrician (daktari bingwa wa watoto)? Nadhani kuna umuhimu wa mtoto huyo kuonwa na Paediatrician akamsikiliza vizuri kifua kwa kutumia stethoscope na pia kumfanyia X-ray ya kifua. Kuna magonjwa mawili ambayo huwa mara nyingi dalili yake ni kikohozi cha mara kwa mara kwa watoto, nayo ni Pumu (Asthma) na magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital Heart Diseases). Haya magonjwa daktari anaweza akayahisi kirahisi tu kwa kusikiliza kifua kwa umakini na/au kufanya X-ray.
Nina mtoto wa miezi tisa ila ana mafua nimpe dawa gani ili apone? Msaada please!
Unge weka umri wa mtoto inge saidia sana wataalam binafsi mimi huwa nachemsha maji halafu una weka chumvi kidogo halafu unamdondoshe matone mawiwili kila pua.Za leo wandugu,
Mtoto wangu anasumbuliwa sana na mafua, yanamfanya kushindwa kupumua na kukosa raha kabisa hata ya kula. Nimejaribu dawa za hospitali za kuzibua naona hazimsaidii. Nini nitumie mbadala kinakachoweza kuzibua hizo pua!.
Asanteni.:embarassed2:
Unge weka umri wa mtoto inge saidia sana wataalam....binafsi mimi huwa nachemsha maji halafu una weka chumvi kidogo halafu unamdondoshe matone mawiwili kila pua...
Asante ndugu yangu,Mpeleke kwa ENT surgeon haraka anaweza kuwa na adenohypertrophy au nasal polypsy kama hana allergy.
kumfukiza pia inasaidia! weka maji ya moto kwenye beseni katia limao likiwa ha maganda yake changanya na chumvi kidogo.kaa nae kisha mjifunike na shuka safi. avute mvuke 2mnts on and 5 mnts off hadi maji yapoe. inakuwa kama steam bath. imemsaidia kweli mwanangu who is two years now!
Kuwa makini na dawa zinazopendekezwa. Miezi miwili iliyopita niliugua mafua na pua kuziba. Nilipowaona Hospitali nikaandikiwa dawa fulani hivi ya matone. Kweli ukiweka tone moja tu pua mwaaaaa zinazibuka . Lakini amini toka wakati huo sisikii/sinusi harufu yeyote. Nimepoteza uwezo wangu wa kunusa. Kabla nilikuwa sensitive sana kwa harufu lakini sasa hata harufu ipi siinusi!