Naomba ushauri: Mwalimu ana TGS E ashushwe awe na TGS D ili afanyiwe recategorization kuwa mchumi au aazimwe aendele na cheo chake cha awali?

Kama umri unaruhusu,akafanyiwe recategorization kwani hiyo F ataifikia mapema na kuipita vizuri tu.E kurudi D wala sio mbali,ni hatua moja.

Kuna mwanangu aliajiririwa kama Afisa mifugo akaenda Mazingira na alifika mbali F huko ila akachungulia alivyoona umri unaruhusu akafumba macho akarudi nyuma,sasa hv anapiga show za kibabe tu.

Fanya maamuzi mapema acha kumbwelambwela
 
kwa sheria za utumishi mshahara wa utumishi unaweza kushushwa kweli unapopandishwa? Maana kupanda kwa daraja ndo kupanda kwa mshahara.

Hilo nadhani halipo,ngoja waje wajuvi zaidi,nadhani atafanyiwa recategorization bila kuathiri mshahara otherwise upande ila si kushuka
Yes unashushwa unaanza moja. Ni wajinga tu wanadhani eti kuwa mchumi ndiyo maisha unayalenga. Kuna vikaragosi kibao vinadhani wachumi wana hela na wakishafanyiwa recat wakiingia ofisini wananjaa utadhani ofisi ya mchumi ina hela. Kwa ufupi mwenye mtindo wa ubongo ndiyo anaweza kukubali ujinga wa kuacha kazi ya heshima ya ualimu na kwenda kufanya kazi ya majungu na haina hela kama ya mchumi.
 
Wanaishi longer wapi, wanakuwa hawana hela ya kugharamia supu na mishikaki ya samaki; ukiwauliza mara ya mwisho kutumia wine ni lini, watakujibu miaka 10 iliyopita.
Siku za mishahara zikifika ikichelewa kutoka utawaonea huruma jinsi wanavyoulizia ulizia humu.

Mei Mosi Mama Samia awafikirie kuwaongezea chochote ktk mishahara yaokwa kweli watasusa kutufundishia watoto wetu bureeeeeee
 
Wengi huwa wanaomba recategorization; wapo waliokuwa waalimu sasa hivi ni maafisa, hatima ya maisha yako, yako mikononi mwako, kama hujihurumii hakuna atakayekuhurumia.
 
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.

kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)/

Hivyo anaomba ushauri.

Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
Mwambie aache ujinga akimbie haraka tena bila kuangalia nyuma aende halmashauri akawe mchumi atanishukuru baadae. Pumbavu huyo dogo
 
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.

kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)/

Hivyo anaomba ushauri.

Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
Angalie maslah ,huenda mshahara utashuka lkn inawezekana Kuna marupurupu kibao kwenye kuwa mchumi
 
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.

kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)/

Hivyo anaomba ushauri.

Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
Nashauri wamuazime tu...huku akiendlea kutafakar asichukue maamuz Kwa haraka. Ualimu Bado sio mbaya.
 
Wanaishi longer wapi, wanakuwa hawana hela ya kugharamia supu na mishikaki ya samaki; ukiwauliza mara ya mwisho kutumia wine ni lini, watakujibu miaka 10 iliyopita.
Hapo umeongopa wapo walimu wengi tuu wanaweza hata kukuajiri wewe na wakakulipa kama kuchoka makundi yaliyo choka yapo kada zote za ajira za chini kuanzia elimu, afya , mambo ya ndani nk.
 
Kuna muda lazima tukubali kubadirika kifikra,dunia inakwenda kasi sana mkuu,heshima ya mtu inategemeana na utendaji kazi wa mtu na sio kazi ya mtu,kila kazi ukiifanya vyema itakupa heshima,labda kama kuna tafsiri nyingine ya heshima
Upo sahihi lakini mtazamo huo ni tofauti na mtazamo wa wengine. Fanya utafiti kwenye jamii au hata halmshauri kwenyewe walimu hawapew heshima wanayostahili
 
Back
Top Bottom