Naomba Ushauri: Mpenzi wangu anachumbiwa na watu wengi, mimi mambo sio mazuri kabisa, nifanyeje?

Kuna beberu mmoja mwenye busara alishawahi sema;
"Before you cum, make sure you have an income."
Kwa hiyo kijana achana na mke wa mtu. Maliza chuo tafuta hela. Wewe mke wako kwa haraka haraka ndo anamaliza Form II. Hadi uje kuwa sawa kiuchumi mke wako atakuwa kafika Chuo
 
Huyo ni mjanja mjanja analiwa kiakili tena hawa mabint wa hospitalini woiiii anakutumia charting za huyo bwege mwingine ili uone yeye ni most wanted upuuzi mtupu mwanamke anaejielewa hawez kukutmia charting z watu wanaomtongoza piga chini kimyakimy hiyo takataka piga kitabu mzee panga life lako la kesho....
 
Kwahio kakuonesha charting za engineer, halafu anakwambia watu wanaomtongoza, marafiki zake pia wwnakwambia watu wanaomtongoza, halafu kakuzidi miaka 2 (ana miaka 24 wewe miaka 22), halafu yeye kamaliza chuo, wewe bado unapambana chuo.

Dogo hapo unaandaliwa kisaikolojia tu, utakuja kupigwa tukio hautaamini macho yako. Kifupi hapo anataka GO AHEAD umruhusu aolewe (atajifanya kama kusikitika ila atakubali), sasa ww ukichelewa ukakaza fuvu utakuja kustukia unatumiwa picha za harusi.

Uyo dem level zake ndio hao ma engineer wanaomtaka, ww mshika pembe tu, mwache aolewe mdada wa watu.

Wewe mkeo yuko form three huko, mpaka ukiwa stable kiuchumi atakua anamaliza chuo. (Wakati huo ka boyfriend kake ka chuo kataachwa ili demu aolewe na wewe). Historia huwa inajirudia tushapitia huko kijana.
 
Mwambie ukweli aolewe,
Wewe bado sana, kwanza inabidi umalize chuo baada ya hapo bado unamiaka kama 5 hivi yakupigika na kupambana ili angalau ukae Sawa,
utampotezea muda mke wako yupo form 1 sahivi siyo huyo.
 
Kama kijana wa 2001 unaweza kupangilia maandishi hivi basi ni imani yangu kubwa una uelewa mzuri na hiki nachotaka kukwambia utakishika na kukielewa. Kwa sasa hivi kinachokusumbua ni mindset yako ukiamini unapendwa lakini kiuhalisia huyo tayari ni mke wa mtu kilichobaki ni kuhalalishwa tu. Hata usipomwambia leo aolewe nakuhakikishia hautazidi mwaka utaanza kuziona rangi huzielewi.

Sasa unachotakiwa kufanya punguza mazoea ikiwezekana hata mbususu usiiguse kama utaweza mwambie akaolewe na Eng, nakuhakikishia baada ya kumwambia ivyo atakulilia machozi na kuja na zile kauli za wanaume ni mbwa usitetereke umefanya jambo zuri kwa ajili yenu wote. Sasa katika hiki kipindi hiki ndio utajua mwanamke ni mtu wa namna gani. Hakikisha haumgusi au kuwa karibu naye utajiepusha na mengi sana.

Naomba niishie hapo naamini umenielewa. Mke wa mtu sumu
 
Wewe na huyo binti akili zenu ni ndogo ila wewe kwakuwa amekuzidi akili that's why unamwona bonge la genius.
Yaani achati huko then akutumie chatting 😝😝😝😝
Kwa mwendo huo unaweza kujinyonga kwa mambo ya kitoto.
 
Sikia dogo mwambie aolewe. Wewe piga kitabu. Kusema utamuoa sasa hivi uongo, labla miaka 5/6 ijayo.
 
Wakuu nipeni ushauri mdogo wenu.

Nipo kwenye mahusiano na huyu binti kimsingi tulianza mahusiano kipindi nipo mwaka wa kwanza chuoni (hivi sasa nipo mwaka wa pili), lakini yeye tayari hivi sasa kamaliza masomo na yupo nyumbani (amesoma Diploma ya clinical medicine).

Lengo la mahusiano yetu ni badae tuanzishe familia kwa pamoja (kufunga ndoa).

Umri wake ni mkubwa kwangu, ananizidi miaka miwili mimi ni wa 2001

Ni zaidi ya mara nne sasa huyu binti ananambia kuna wanaume ambao wana muapproach kwaajili ya kumuoa, hata rafiki zake wa kike mara nyingi huniambia kuwa huyu binti ana windwa na wanaume wengi tena ambao wapo seriously na wenye maisha yao.

Ofcourse hata mimi naweza ku confirm hicho kitu, maana she is beautiful pia ana akili na ufahamu mzuri, she is completely a wife material.

Jana usiku amenitumia screenshot za chating za jamaa ambae ni engineer, jamaa anamwambia kabisa anataka kumuoa mwakani na yupo serious.

Ugumu unakuja hapa, mimi bado nipo chuo tena maisha yangu ni kawaida sana, na nyumbani kwetu hali si nzuri hata kidogo, kiufupi bado nina safari ndefu sana ya kujitafuta kimaisha.

Naona kabisa huyu binti nitamchelesha kwenye maisha anayotaka, na yeye anajua hali yangu hiyo. Natamani kumwambia akubali hao wanaomchumbia lakini sijui atapokea vipi, mana tunapendana, na mimi ninapotazama safari ya maisha yangu bado naona ukungu na giza kubwa sana.

Sitaki kumzibia riziki huyu binti, najua ananipenda na mimi pia nampenda sana.

Hapa nipo njia panda, sijui nifanye maamuzi gani kwa manufaa ya kila upande.
Mwanamke kakuzidi umri unahangaikaje naye, huyo siyo level yako, maliza chuo, tafuta pesa. Mwanaume unaoaje demu aliyekuzidi umri
 
Mwanamke kakuzidi umri unahangaikaje naye, huyo siyo level yako, maliza chuo, tafuta pesa. Mwanaume unaoaje demu aliyekuzidi umri
Piga chini, tafuta aliye form four kwa sasa, ndo saizi yako. Siyo mke kakuzidi umri, anazeeka kabla yako, kisha baadae uanze kukodolea macho vibinti vibichi.
 
Kwamba anajisifia kuwindwa hiyo ni ishara tosha uhusiano wenu hauendi popote, maana hata kama ukiishia kumuoa utapata tabu sana kwa vile atakua anakukumbusha waliokua wanamchumbia.
Wewe pambana na maisha kwanza, jichimbie kisha utapata mnaye endana.
Mi ninavyoelewa, akikwambia kuwa anatongozwa sana, anamaanisha ukaze bidii umuopoe kabla hajawahiwa.
 
Katika kitu nimejifunza kwenye maisha ni kuwa swala la mapenzi, ndoa na maisha huwa lina athiriwa na namna unapanga vitu vyako na unakutana na nani.

Eneo la mapenzi unahitaji kukutana na mtu anayekuelewa wewe kama wewe bila ya kutamani kingine chochote kuhusu wewe mfano pesa, mali, status yako na familia yako etc.

Kama huyu binti anajua hali yenu huko kwenu na hali yako na still anataka kuwa na wewe then likely anakupenda wewe kama wewe. Hapa kuna point muhimu unatotakiwa kubeba.

Eneo la ndoa unahitaji kukutana na mtu anayejua wajibu wake kama mwanamke (in this case),anajua thamani yako kwake kama mwanaume, na la muhimu zaidi atambue ushirika wenu unalenga kutengeneza future ya aina gani ili aweze kujicommit na hata pale unapokwama aweze kukusaidia kunyanyuka. Sijajua huyu binti upande wake umemuonaje eneo hilo.

Maisha ni swala la utafutaji wa pesa na mali ili kuweza kujua utaishi vipi kwenye mazingira yako. Kwasasa upo chuo bwana mdogo, binti amekuzidi umri na yupo kitaa, sasa unahisi unaweza kushirikiana nae kumpa maisha mazuri not necessarily maisha ya gharama.

Nadhani ni muda ujitambue. Hizi sababu umetoa hapa ni visingizio vya kuficha ukweli kuwa haupo tayari kuprove upendo wako kwa huyo binti unasubiria makusudi yake itokee uje kulalamika hapa kuwa wanawake sio watu.

Kuwa chuo sio ulemavu kusema unashindwa kutafuta mishe za kukuingizia hata 20,000/- per day. Kama unampenda huyo binti, utafanya jitihada kwa kushirikiana nae mpate pesa kidogo ya msingi wa kuanzia maisha then utaanza nae hata kwenye nyumba ya chumba na sebule huku wewe ukimalizia shule yeye akijitafuta na kazi ya kusapoti familia yenu changa.

Ila kama wewe unajua hauna mapenzi ya kweli na huyo dada ulikuwa tu ni ujana then why unahangaika kujua ni nini cha kufanya?
 
huyo muache aende we songa mbele jitafute kwanza wazuri hawaishi wako wengi tu utapata mwingine tu acha kujipa stess.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom