Naomba ushauri: Mke wangu mgonjwa

Vuta subira Mkuu na kila la heri katika ujauzito wenu wa kwanza.
 
ni mara ya kwanza mkuu

Pamoja na ushauri wa kusubiri kwa muda zaidi, ni vema pia kuangalia kama hana matatizo mengine yanayoleta dalili kama hizo za ujauzito (kutopata hedhi kwa wakati etc) hasa hasa kwa sababu ni ndio mara ya kwanza kuna uwezekano mkubwa 'dalili' anzozihisi ni psychological zaidi na pengine zinatokana na mapokeo tu (zaidi kwa sababu pengine anakosa uzoefu wa jinsi hasa mimba inavyokuwa, zaidi ya kusimuliwa ama kusoma).

Lingine, ambalo ni muhimu kuligusia (ingawa pengine si hivyo kwako) ni social pressure. Hili ni lazima muwe nalo macho sana, otherwise litawaletea shida na hasa wewe mwanaume ni vema mara zote ukasimama upande wa mkeo ili asiathirike zaidi na 'unyanyapaa' kama upo hasa kutoka kwa ndugu zako. Social pressure zikizidi, wanawake wanaweza hata kufikia kufake ujauzito na hata mara nyingine wanafanikiwa kufikia kupata mtoto kwa njia zisizo halali (eg kuiba watoto wachanga hospitalini) ili tu kumridhisha mumewe.
 
mpe mama likizo akapuzike kwao alilaks ,mie ishanitokea alipgwa u/s akaambiwa anauvimbe baadaye ikaonekana halafu kama ashapata mtoto akaa muda mrefu kujifungua mtoto m/ne .je mnamtoto?
 
Pole sana mwanangu,

Inaonekana mna hamu kubwa ya kutupatia kajukuu. Kama walivyokushauri ndugu zako, kuwa mvumilivu. Endelea kujaribu. Usikate tamaa. Muonyeshe bi mdogo mapenzi ya hali ya juu kumjenga kisaikolojia. Msongo wa mawazo huaribu mimba pia. Ukianza kuonyesha wasiwasi hata mamaa utampa taabu sana kiasi cha kuathiri kiumbe kilichopo. Vipimo inategemea umepima wapi. Tatizo la kutoonekana mimba kwenye vipimo lilinitokea kwa mtoto wangu wa kwanza. Nilihisi mambo tayari lakini nilipokwanda hospitali nikiwa na wiki 5 nikaambia hakuna kitu. Sikuamini, na wala sikumtaarifu mwenzangu majibu hayo. Nikaenda hospitali nyingine nikaambiwa ina wiki 7. Nilifurahi lakini nikaona tatizo kwani ujauzito hule kwa mahesabu yote ulikuwa ni wa wiki 5 na siyo 7. Nikabanisha tu nikaenda hospitali ya tatu, vipimo vikakubaliana na hesabu zangu.

Baba nanii tafadhali mezea, baada ya kupata majibu niliyokuwa na uhakika nayo ndiyo nikamwambia. Naye akasema alihisi hivyo kwa kuwa aliona nimebadilika sana. Siri ya vipimo vya awali nilimpa baada ya kuzaliwa mtoto. Nilihofia kuleta mtafaruku ndani ya familia. Kwa hakika vipimo vya daktari wa mwisho vilikuwa sahihi kabisa. Baada ya kuwaeleza ukweli, wanafamilia wote walinishukuru na kunipongeza kwani vipimo vile vingejulikana bila kupata usahihi hata ndoa ingeweza kuvunjika ama kutetereka.

Mwanangu, ukiona nyani mzee kakwepa mishale mingi. Hiyo ndiyo baadhi ya mishale yenyewe ya maisha. Kuwa mvumilivu. Mpe support mwenza wako. Mtafanikiwa kwa mapenzi ya Bwana.
 
Bado ni mapema sana kuhofu kuhusu mimba. Subirini mimba iwe na wiki kumi na mbili na kuendelea. Pia hebu jaribuni Pregnancy Urine test, kwa miezi miwili utapata majibu kama autapima sawa sawa. It is cheaper than UIltra-Sound. Pharmacy watakuelekeza namna ya kutumia kama hufahamu, pia maelezo yapo kwenye kipimo chenyewe, simple, short and clear.
 
Edson pole sana...

Ngoja nijaribu, if possible jaribuni kwanza kuacha mawazo ya hiyo mimba mpumzike ili afya ya mama ikae vizuri, stress can cause alot of problems. then tafuteni Dr. Mzuri awape ushauri wa namna ya kuendelea na uchunguzi na pia care ya mama.

Kuna wakati inatokea mtu unakua umepania sana kitu, au uko obsessed etc. kiasi kwamba ukaamini kcihwa kinauma au macho hayaoni, and this may even need clinical attention

KWA SASA JARIBUNI SANA KU-FOCUS KWENYE RECOVERY NA SIO MTOTO, HIYO STRESS ITAWASUMBUA SANA

ushauri wako mgumu
 
..Pole sana mkuu, kwa maelezo yako inaonekana mmekuwa mkitafuta mtoto kwa muda sasa bila mafanikio, na hali hiyo imeanza kumsononesha mkeo (hili ni kawaida kutokea kwa kina mama). Kufikia hatua ya kutegeshea siku ya ovulation ndio mkutane kimwili ndio inanifanya nifikiri hivi.

Sasa kisaikolojia anaweza kuwa amejiandaa MNO kuwa mjamzito na hii ikaathiri akili yake kwa kiwango cha kutookuona/kukata hedhi. Usidharau nguvu kubwa ya vile tunavyofikiria; zipo simulizi za watu waliopooza mkono siku ya mtihani sababu tu waliamini hawawezi kufanya mtihani huo!

kama niko sahihi kuwa mnahangaika kwa muda sasa kupata mtoto; nakushauri yafuatayo:-

  • take it easy, go slow. Hofu huharibu mambo zaidi, na hata kuvuruga ovulatory cycle(mzunguko wa hedhi)
  • Fikirieni kufanya infertility work up....vipimo kadhaa vya kubaini tatizo (muhimu: wote mshiriki sio kusema mwenye tatizo ni mke/ au mume tu)
  • Ondoeni hiyo ratiba ya kukutana siku ya ovulation; afterall mmefanya utafiti kuibaini hiyo siku exactly ni ipi? achaneni na theory za barabarani za siku ya 14 it do vary sometimes
  • Furahieni ndoa yenu
  • Unaweza ukani PM pia.....

Hili ndilo jibu sahihi, hana ujauzito. vumilia tu atapata hedhi.
 
Mmmmmmmh,mungu mkubwa atakusaidia,jitahidi sana lakini ulivyoanza nakupongeza sisi wenye imani haba saa hizi tungekuwa mbali. Mungu atakuepusha na haya majaribu. :hug:
 
Mkuu hiyo imeshawapata wengi, wako ambao baada ya muda vipimo vilionyesha ujauzito na wengine walirejea hali ya kawaida hakuna mimba. Kuna case mama anashika mimba bila kujijua anashtukia uchungu, hivyo haya yote yapo. Kama walivyokwisha changia wengine, vuta subira miezi miwili ni muda mfupi sana kwa wanaotafuta mtoto, hata ukienda hospitali dr. hatafanya chochote unless mkeo yuko over 35, sana sana atawaambia mrudi baada ya miezi sita.

Mama anayejiandaa kubeba mimba anashauriwa pamoja na mambo mengine kutumia prenatal multi vitamin, kabla ya kubeba mimba na aendelee mpaka atakpojifungua. All the best and take it easy!
 
habari wana jf:

naomba kusaidiwa juu ya tatizo alilo nalo mke wangu.....mda ulipowadia wa kushika mimba mimi na mke wangu tulikutana kimwili......baada ya mda dalili zote za kuonyesha kuwa ni mjamzito zilianza kujitokeza ikiwa ni pamoja na hedhi kutoweka nk....yaani dalili zote za kuonyesha kuwa yu mjamzito zilijitokeza.
sasa alipokwenda hospitali kupima mimba haikuonekana.....dokta akashauri arudi baada ya wiki moja....amerudi hosp akapimwa tena pia ikaonekana mimba hakuna.....akapimwa kwa ultra sound..pia mimba haikuonekana. mpka sasa mke wangu hara raha na mimi pia najiuliza kuna nini kimetokea..vipimo vya hosp vinaonyesha hakuna mimba lakini yeye anahisi ana mimba maana dalili zote za kuwa yu mjamzito anazipata......ndugu zangu hili tatizo linaweza kutokana na nini?
naombeni ushauri kwa wale wataalam wa magonjwa ya wanawake au mwenye uelewa juu ya hili swala
Ili kuwasaidia wenye nia ya kukupa ushauri wa kitaalam eleza mmeishi pamoja kwa muda gani, mmeshazaa watoto wangapi na hiyo ni mimba ya ngapi, bila kusahau umri wako na wa mkeo. Vinginevyo utaishia kupata ushauri wa kijamii zaidi kama inavyoelekea.
 
oh kaka i had this hali wakati fulani after my first born. nilidhani nimeconceice na nikawa hadi napata kichefuchefu na hedhi kutoweka kwa miezi 2, nilipima hosp ila wakasema hakuna. hofu na mashaki vilijenga hali ya kujua ni mjamzito hadi nilipoanza kurelax hali ikarudi kuwa normal.

my ushauri.
huenda mna shinikizo sana nafsini mwenu la kupata mtoto. kwa vili mliamini kuwa mkikutana wakati wa siku hizo mtapata mtoto mawazo ya mkeo yamekua hivo kua anajua ni mjamzito na ndio maana pengine mlienda kucheki haraka. yamkini ni fikra tuu. hivo u n my wii have to take it easy. na pia ikiwa ipo ipo tu ndugu. msianze kujipa hofu nyingine za kiimani, hiyo itaongeza tension na itakua worse. akitimiza miezi mitatu nendeni tena hosp.

Regency hosp kuna daktari mama moja anaitwa ana pruna ni mzuri sana kwa masuala ya kina mama kama vipi mmwone.
 
Pole subiri baada ya miezi mkacheki tena.Pia anahitaji kutoliwazia sana jambo hilo.

Edson
Wewe na mke hamtakiwi kuliewazia sana hili jambo, najua kuna familia huwa wanatoa pressure kubwa kwa wanandoa, ni jukumu lako wewe kumkinga mkeo na hali hii, swala la kupata mtoto litakuja tu, akapime after three to four months. Hata kama haitakuwepo si tatizo, jipangeni upya na kwa uwezo wa mwenyezi mungu, mwingi wa rehema mtapata tu mtoto madhali afya zenu zinaruhusu.
Naongea kwa experience.
 
habari wana jf:

naomba kusaidiwa juu ya tatizo alilo nalo mke wangu.....mda ulipowadia wa kushika mimba mimi na mke wangu tulikutana kimwili......baada ya mda dalili zote za kuonyesha kuwa ni mjamzito zilianza kujitokeza ikiwa ni pamoja na hedhi kutoweka nk....yaani dalili zote za kuonyesha kuwa yu mjamzito zilijitokeza.
sasa alipokwenda hospitali kupima mimba haikuonekana.....dokta akashauri arudi baada ya wiki moja....amerudi hosp akapimwa tena pia ikaonekana mimba hakuna.....akapimwa kwa ultra sound..pia mimba haikuonekana. mpka sasa mke wangu hara raha na mimi pia najiuliza kuna nini kimetokea..vipimo vya hosp vinaonyesha hakuna mimba lakini yeye anahisi ana mimba maana dalili zote za kuwa yu mjamzito anazipata......ndugu zangu hili tatizo linaweza kutokana na nini?
naombeni ushauri kwa wale wataalam wa magonjwa ya wanawake au mwenye uelewa juu ya hili swala
Nakushauri mkeo akaonane na dk na aombe kupima Hormon balance,HVS.
Hali hiyo hutokea ila elewa kuwa kutopata hedhi sio dalili kuu ya kuwa mjamzito.Hata mimi iliwahi kunitokea hali hiyo.Sikupata hedhi kwa takribani miezi 9.Nilipokwenda pima kliniki ninaonesha kuwa nina UJAUZITO, tumbo linakua kubwa liliongezeka kila mwezi nilipo pimwa kimo cha mimba.Mapigo ya mtoto hayapo lakini nikawa nahisi mtoto kucheza hata lilipofikisha miezi 9.Niligutuka na kupima PLANO(preg test)kwa kipimo cha U.P.T.mimba haikuonekana!Mwisho wa yote tumbo likanywea.
 
mke wako ana tatizo linaloitwa pseudocyesis...hii ni false belief ya kua pregnancy ambayo inaassociate na dalili zote za ujauzito. ni tatizo la kisaikolojia lipo katika kundi linaitwa somatoform Disorder not otherwise specified na mfano wa hili kundi ndio pseudocyesis ambalo mkeo analo. tafuta kwa google au wasialiana na wataalam kupitia psychologicalsupport@hotmail.com
 
mkuu huwa tunakutana kimwili na mwenzangu kama kawaida ila tulikuwa makini katika siku zile za hatari.....sasa mda umefika tukasema sasa na tupate mtoto ndo tukakutana kimwili nza mwenzangu katika siku hizo........nabaada ya hapo ndo kama nilivyoeleza hapo juu

KwA hiyo mlitiana sio?
 
KwA hiyo mlitiana sio?
Mkuu mada ya 2011 umeiibua leo wakati nahisi hawa kama Mungu aliwabariki uzao sasa wanakaribia kulea mjukuu!!

Naona bado yupo active hapa jukwaani tumsubiri aje atupe mrejesho.
 
habari wana jf:

naomba kusaidiwa juu ya tatizo alilo nalo mke wangu.....mda ulipowadia wa kushika mimba mimi na mke wangu tulikutana kimwili......baada ya mda dalili zote za kuonyesha kuwa ni mjamzito zilianza kujitokeza ikiwa ni pamoja na hedhi kutoweka nk....yaani dalili zote za kuonyesha kuwa yu mjamzito zilijitokeza.
sasa alipokwenda hospitali kupima mimba haikuonekana.....dokta akashauri arudi baada ya wiki moja....amerudi hosp akapimwa tena pia ikaonekana mimba hakuna.....akapimwa kwa ultra sound..pia mimba haikuonekana. mpka sasa mke wangu hara raha na mimi pia najiuliza kuna nini kimetokea..vipimo vya hosp vinaonyesha hakuna mimba lakini yeye anahisi ana mimba maana dalili zote za kuwa yu mjamzito anazipata......ndugu zangu hili tatizo linaweza kutokana na nini?
naombeni ushauri kwa wale wataalam wa magonjwa ya wanawake au mwenye uelewa juu ya hili swala
Ukipata muda njoo pm nikuulize mambo mawili matatu kwanza
 
Back
Top Bottom