Naomba ushauri, mke kanitoroka

Naomba ushauri, mke kanitoroka

Habari wana Jamiiforums

Nilisafiri kwa muda wa siku kama 35 nikaenda Morogoro kufanya kazi, baada ya kukaa siku kama 30 nilirudi nyumbani ghafla kwenda kumsurprise mke wangu maana nilikuwa nimemmiss, nilipofika nilipigwa na butwaa baada ya kugundua kahamisha nguo zake, viatu, vyombo na kila kitu alichonunua yeye pale ndani na kabakiza vitu vichache sana.

Basi baada ya kumuuliza vitu vyake viko wapi amesema amevipeleka kwa rafiki yake ambae mim simjui. Baada ya kukosa maelezo ya kutosha niliondoka nyumbani na kurudi jioni nikakuta kabeba kila kitu kaondoka. Baada ya kufuatilia nikajua ameenda kanisani kwenye semina.

Hakurejea kabisa nyumbani na kwa muda wa siku 3 hapatikani kwenye simu na wala sikujua yuko wapi, hata wazazi wake pia hawajui.

Baada ya siku tatu akaanza kupatikana kwenye simu yake ndio akaitwa kwa wazazi akaenda na kusema ameamua tu kuondoka maana ameona hatujafunga ndoa na tumekaa miaka 2 hivyo amechoka kuzini anataka amrudie Mungu wake.

Ni kweli ndoa hatujafunga lakini taratibu za kiafrika zimefuatwa. Sina shaka sana na kuchepuka kwa kuwa hana tabia kama hiyo. Kiukweli nimepata stress sana.

Mpaka sasa sielewi nini cha kufanya.

Naombeni ushauri
Pole, ila unapate ujasiri wa kumuita mtu amambaye hujafunga nae ndoa kua ni MKE wako,
Sasa ni wakati Sasa wa wewe kwenda kufunga nae ndoa maana yeye kachoka kuzini
 
Kichwa cha Uzi "mke kakutoroka na unaomba ushauri!" Content "ahsanteni".
So unatushukuru kwa kumtorosha huyo mkeo ila Kuna Jambo baya litamkuta mtoroshaji au..?
Maana kwasie tulioendelea tumesoma kama Kuna kisasi fulani hivi ambacho kitalipizwa kwa njia ya mizimu au majini...😂
 
Kichwa cha Uzi "mke kakutoroka na unaomba ushauri!" Content "ahsanteni".
So unatushukuru kwa kumtorosha huyo mkeo ila Kuna Jambo baya litamkuta mtoroshaji au..?
Maana kwasie tulioendelea tumesoma kama Kuna kisasi fulani hivi ambacho kitalipizwa kwa njia ya mizimu au majini...😂
Pole kwa kuchelewa kusoma uzi, ushauri umeshatosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom