Naomba ushauri/maoni juu ya jambo hili

Premij canoon

JF-Expert Member
May 27, 2018
1,115
2,490
Salaams wanajamii, poleni na majukimu.

Moja kwa moja niende kwenye jambo lililonifanya hasa nije hapa.

Kuna biashara nilifanya na mtu ambae alikuja ofisini kwangu kununua huduma, tukakubaliana bei lakini akadai hana cash mfukoni hivyo analipa kwa mobile money (Airtel momey), Tukakubaliana nikampa namba ya malipo na akafanya malipo, nikampa huduma yake tukamalizana.

Siku hiyohiyo muda mfupi baadae naona txt ya AIRTEL MONEY ikisema :-

"Mteja xxxxx ameomba kurudisha muamala PP210131.xxx.B10863 wa Kiasi cha Tsh xxx.00.Pesa hii imezuiliwa, Piga *150*60# ili kuhakiki kurudisha muamala huu"

Na txt nyingine ikasema :-

"Ombi lako la kurejeshwa kwa muamala PP210131.0444.B10863 uliokosewa limetumwa Airtel"

Na nyengine pia ikasema:-

"Kitambulisho rejea TC2xxxz.0505.D15479 muamala uliopokea kwa makosa umetolewa kwenye akaunti yako. Salio jipya ni xxx Tshs."

Nikapatwa na mshangao sana, nikajua tayari hapa jamaa kanitapeli kwa uzembe wa Airtel, sikufanya chochote nikaendelea na mishe zangu ili siku inayofuata niende ofisi za airtel kuiloza na wanipe ufafanuzi ni kigezo gani kimetumila kuhakiki kama jamaa kakosea muamala, na kwanini hawajanishirikisha!

Kwenye Airtel Money kuna huduma walioiweka siku za hivi karibuni kwamba utaweza kurudisha muamala uliokosea kutumwa.

JF ni jukwaa pana. Nimewasilisha hapa kuomba ufafanuzi wa kisheria nitakaoweza kuchukua dhidi ya mwizi na Airtel kwa uzembe wao uliofanikisha mimi kuibiwa.

Nawasilisha.
 
Airtel wao hawahusiki na huo wizi ,hyo huduma waloweka inamaana mteja kama kafanya muamala kimakosa anaruhusiwa kurudisha muamala huo,kwa hyo bondi ipo kati ya airtel na hyo alofanya muamala na sio wewe,kiufupi deal na alokutapeli airtel wao hawahusiki na wizi huo
 
Nadhani Airtel walipaswa kujumuisha pande zote mbili, sio upande mmoja. Hivi huoni huu utaratibu unaleta mwanya kwa matapeli kufanikisha utapeli kwa urahisi mkuu?
 
(Jenga picha) upo dukani kwako, anakuja mteja anakwambia nataka hio jeans. Unamwambia bei yake 25,000/, anasema sawa nalipia kwa airtel money naomba namba nilipie. Unampa namba analipia kisha unampa mzigo wake, huyoo anaishia.

Baada ya nusu saa kuondoka unapokea txt kutoka airtel money... "Muamala uliotumwa kwako kimakosa umerudishwa kwa namba xxxx"

Airtel hawajakushirikisha wala nini, wao wamesikiliza upande mmoja tu. Sasa huoni hii kama udhaifu kwa airtel, na kisheria wamehusika kwa huo utapeli.
 
Hapo uko sahihi,ila changamoto watamwamini nani mteja au wewe ulopokea hyo hela,
 
Salaams wanajamii, poleni na majukimu.

Moja kwa moja niende kwenye jambo lililonifanya hasa nije hapa.

Kuna biashara nilifanya na mtu ambae alikuja ofisini kwangu kununua huduma, tukakubaliana bei lakini akadai hana cash mfukoni hivyo analipa kwa mobile money (Airtel momey), Tukakubaliana nikampa namba ya malipo na akafanya malipo, nikampa huduma yake tukamalizana.

Siku hiyohiyo muda mfupi baadae naona txt ya AIRTEL MONEY ikisema :-

"Mteja xxxxx ameomba kurudisha muamala PP210131.xxx.B10863 wa Kiasi cha Tsh xxx.00.Pesa hii imezuiliwa, Piga *150*60# ili kuhakiki kurudisha muamala huu"

Na txt nyingine ikasema :-

"Ombi lako la kurejeshwa kwa muamala PP210131.0444.B10863 uliokosewa limetumwa Airtel"

Na nyengine pia ikasema:-

"Kitambulisho rejea TC2xxxz.0505.D15479 muamala uliopokea kwa makosa umetolewa kwenye akaunti yako. Salio jipya ni xxx Tshs."

Nikapatwa na mshangao sana, nikajua tayari hapa jamaa kanitapeli kwa uzembe wa Airtel, sikufanya chochote nikaendelea na mishe zangu ili siku inayofuata niende ofisi za airtel kuiloza na wanipe ufafanuzi ni kigezo gani kimetumila kuhakiki kama jamaa kakosea muamala, na kwanini hawajanishirikisha!

Kwenye Airtel Money kuna huduma walioiweka siku za hivi karibuni kwamba utaweza kurudisha muamala uliokosea kutumwa.

JF ni jukwaa pana. Nimewasilisha hapa kuomba ufafanuzi wa kisheria nitakaoweza kuchukua dhidi ya mwizi na Airtel kwa uzembe wao uliofanikisha mimi kuibiwa.

Nawasilisha.
Hio ni loophole ya hudumu za mtandao, hawakuangalia hilo wakati wa kuanzisha hudumu, ni vywema ukaenda Mwenyekiti office Zao na baada ya hapo nenda police kuna kitengo cha kufuatilia wiza wa mitandao na wanaweza kumkamata
 
Airtel wao hawahusiki na huo wizi ,hyo huduma waloweka inamaana mteja kama kafanya muamala kimakosa anaruhusiwa kurudisha muamala huo,kwa hyo bondi ipo kati ya airtel na hyo alofanya muamala na sio wewe,kiufupi deal na alokutapeli airtel wao hawahusiki na wizi huo
Huoni kama Airtel wametoa mwanya kwa watu kufanya utapeli?! Kwanini wasiweke option ya kuhakiki kwa alietumiwa hela?!
 
Nadhani Airtel walipaswa kujumuisha pande zote mbili, sio upande mmoja. Hivi huoni huu utaratibu unaleta mwanya kwa matapeli kufanikisha utapeli kwa urahisi mkuu?
Huyo anajibu kirahisi kwasababu hayajamkuta
 
Simple wakati mwingine unajiongeza tu....
unahamisha mzigo instantly......
sio kulaumu laumu tu,
 
Hapo uko sahihi,ila changamoto watamwamini nani mteja au wewe ulopokea hyo hela,
Wakiona tarifa zinakinzana c inabidi wasimamishe au waugandishe muamala, yan usiende kwa A au B, na wawatake wafike ofs za Airtel money na ushaidi ili kujiridhisha
 
Nadhani Airtel walipaswa kujumuisha pande zote mbili, sio upande mmoja. Hivi huoni huu utaratibu unaleta mwanya kwa matapeli kufanikisha utapeli kwa urahisi mkuu?
Kwenye hii case yako wala usipoteze muda wako kung'ang'anizana na Airtel mtafute huyo aliyekupiga,mitandao ya simu huduma nyingi huwa wanaziweka randomly kila mteja ajichagulie anachokitaka so kama wewe ulitaka line yako iwe ya kibiashara ungeenda mapema kuna form unajaza ikihitaji TIN # na aina ya baishara hiyo line inasajiliwa na ikishakuwa active mtu akiingiza hela kimakosa haiwezi kurudi kwake mpaka pande mbili muulizwe.
 
Hapo ndugu ushapigwa cha msingi tulia tu maana hata ukienda polisi utapoteza nyingi zaidi mwishowe hakuna utakaloambulia. Wengi hawatakagi kabisa kupokea hela kwa nhia ya simu unless utumie njia ya kutuma account ya benki maana huko hawezi kurudisha muamala.
 
Wao pia waliliona hilo kabla ndio maana kwa matumizi ya kibiashara wakaweka line maalum unazoweza kusajili kwa ajili ya kupokea fedha za biashara zile "lipa kwa M-pesa" au "lipa kwa tigopesa" sidhani kama miamala yake inaweza kurudi kirahisi namna hiyo.
Kwa kesi yako nadhani ni vyema ukadeal na mteja wako kama unamfahamu na ujifunze kupitia kadhia hiyo.
 
Nenda Airtel mkuu...wakakulipe pesa zako ikiwezekana nenda mahakamani...
 
System nzima ni kosa pole kwa hasara ......ndo maana mitandao ilikuja na lipa no kwaajili ya wafanya biashara umejifunza badilisha mfumo sidhani kama kuna kitu unachoweza fanya pesa irudi sababu airtel hawafaham makubaliano yeyote kati yenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom