Naomba maoni yenu juu ya wazo hili - ushauri wa afya

Impatient Pessimist

New Member
Aug 17, 2016
3
0
Naomba mawazo yenu katika tafiti hii ninayoifanya kuelewa tatizo au kero katika upatikanaji wa elimu, ushauri, na habari za kiafya. Mimi ni mfanyakazi wa afya ya jamii. Katika kazi zangu, nimejifunza kwamba kikwazo kikubwa cha watu kutoweza kuwajibika juu ya afya zao ni ufahamu mdogo, imani na dhana potofu katika jamii. Nina wazo la kubadilisha hili, ila nahitaji mawazo yenu ili kuhakikisha ufumbuzi husika unapatikana.

Naomba ujibu maswali 3-4 hapo chini. Jibu tu mfano 1) A, 2) C, 3) D, 4) B. Tafadhali chagua jibu moja tu linalokuhusu zaidi. ASANTE SANA!

1. Je, hili ni tatizo kwako? Jibu [A] kama NDIO, kama HAPANA. Upatikanaji wa ushauri au habari za kiafya ambazo ni hakiki na za kuaminika, katika muda muafaka kwako.


2. Kama hili NI tatizo kwako, sababu kuu ni nini hasa: Jibu [A] kama hujui mtu wa kumuuliza au sehemu ya kuuliza, huna muda wa kwenda kwenye kituo cha afya kuuliza, [C] huamini jibu utalopata , [D] sababu nyingine (tafadhali taja sababu, kwa mfano D sina hela ya kwenda kituo cha afya )


3. Je, kwa sasa, ukiwa na shida ya ushauri au kupata jibu la maswali yako ya kiafya, unafanyaje? Jibu [A] naenda kituo cha afya, nawasiliana na daktari ninayemfahamu, [C] nina-google, [D] namuuliza ndugu, rafiki, jamaa, [E] Napata kivingine (tafadhali taja jinsi unavyopata huduma)


4. Kama ungepewa fursa kuchagua jinsi ya kupata ushauri au majibu ya maswali yako ya kiafya (sio tiba), wakati muafaka kwako, ungependa upate huduma hii kwa njia ngani? Jibu [A] kama ungependa kwenda kituo cha afya, ungependa mhudumu akutembelee kwako, [C] ungependa kusearch mwenyewe mtandaoni (google), [D] ungependa kuwasilana na daktari mtandaoni, ikiwemo App, [E] ungependa kumpigia au kutext na daktari kwenye simu
 
Back
Top Bottom