Naomba ushauri kuhusu tatizo la ini kuwa na mafuta

Habar wanajamvi,

Nina mzee wangu kaenda kufanyiwa vipimo hospitali kakutwa na tatizo Hilo, vipi, mwenye ushaur zaidi ya jinsi ya kuzuia,kukabili na kumaliza tatizo hili tusaidiane

Ili kutatua tatizo la ini kuwa na mafuta mengi, ni vyema kutambua sababu:

Hali hii hujitokeza pale ambapo uchukuaji wa vyakula vyenye nguvu/wanga kuwa mkubwa kuliko matumizi ya nguvu ya mhusika.

Hivyo, kulingana na hali ya mhusika ni vyema kuzingatia hilo wakati wa tiba.

Pia matumizi sahihi ya dawa mbalimbali atakazoandikiwa.

Mambo mengine ni kuhakikisha mhusika hana tatizo lolote linalohusiana na:

1: Ugonjwa wa Kisukari
2: Homa ya ini
3: Matumizi ya pombe
4: Uzito uliopitiliza
5: Kiasi cha mafuta mabaya vs mazuri mwilini.
6: Kuangalia kiasi cha vimeng'enyo vinavyotolewa na ini ili kuangalia utendaji kazi wa ini.
 
mnunulie unga wa mlonge pamoja na unga wa artemisia, changanya ujazo wa kijiko kimoja kimoja kidogo cha chai unga wa mlonge + artemisia kwenye maji ya vugu vugu nusu lita mpe mgonjwa asubuhi na usiku wakati wa kulala kwa muda wa wiki2 mpaka mwezi 1. tiba mbadala hii itamsaidia sana kama ilivyo nisaidia mimi mwenyewe, nadhani mzee atakuwa na tatizo la kisukari cha pili??

kwenye hili jukwaa zamani tulikuwa tuna share tiba za matatizo mbali mbali kama haya openly, inasikiila siku hizi matatizo yetu watuwamefanya fursa kwao ku share tiba na imekuwa nadraa sana ???
 
Na je mtu mwenye tatizo la ini stage three tiba yake ni nini?
nenda hospital kwanza wakwambie kiini cha tatizo nini, kuna baadhi ya matatizo ya ini yanatibika kirahisi sana kwa matibabu ya kwaida ya hospital ( allopathic treatment ) kuliko kule kwingine……...
 
Habar wanajamvi,

Nina mzee wangu kaenda kufanyiwa vipimo hospitali kakutwa na tatizo Hilo, vipi, mwenye ushaur zaidi ya jinsi ya kuzuia,kukabili na kumaliza tatizo hili tusaidiane
Mkuu pole sana je Mzee wako ameshapona amradhi yako?Kama hajapona nitafute kwa wakati wako ili nipate kumtibia mzee wako .
 
Hana dawa Mimi mwenyewe Nina tatizo kama Hilo anasema nimpe milioni 2 nimpelekee mtu kigamboni. Kiufupi mazingira yalikuwa ni utapeli mtupu.
Kula mboga mboga chungu zilipokwa kiasi sio sana, matunda jamii ya ndimu. Punguza wanga, pombe, sigara, sukari. Fanya mazoezi au kazi ngumu
 
Kitu pekee ninachofahamu huyu ni tapeli, simjui na wala hanijui ninachohadithia ni kitu ambacho kilichotaka nitokea.
Kuna siku nilijichanganya akasema ana dawa ya kukuza mashine. Nikalipa laki mbili na nusu, dawa zikafika chupa zilikuwa mbili, zimetolewa zile karatasi za nje, ila kwa kuzitazama ni kama mafuta ya mzeituni. Pia kulikuwa kuna unga flan kama vile wa karafuu au kitu kingine kinachonukia vile. Utaratibu wa kutumia dawa ni kutoa mafuta kidogo unapasha afu unachua na kiasi flan cha ule unga. Nikatumia hii dawa kwa siku tatu hivi, mashine ikawa viupele vingi hatari, nikamjulisha kuwa hii dawa badala ya kukuza inaleta viupele.

Akasema dawa zipo nyingi hivyo anabadili dozi. Akasema niwe nakata vitunguu maji nichanganye na kiasi flan cha yale mafuta nipashe afu nitumie hayo mafuta kuchua.

Nikatumia siku kama 7 hivi nikaona ujinga, nikaona mambo ya kunikia pilau asubuhi hayana tija.

Baada ya hapo wala hakuulizia chochote kile, nikaona hapa nimepigwa mchana kweupe. Alipa wasiwasi zaidi aliposema anatibu hata ngoma na mtu anapona.

Inawezekana kuna baadhi ya magonjwa anatibu vizuri, ila mengine anaingia tamaa ya pesa kusema anaweza kuyatibu ilihali hana uwezo huo.
 
Niamini Mimi hatibu chochote ni tapeli tu
 
Back
Top Bottom