Young saul
Member
- Feb 5, 2018
- 15
- 19
Habari zenu wadau!!
Nianze kabisa kwa kuelezea huu mlolongo wa matukio ambayo nimekua nafikiria kuhusu huyu baba yangu mzazi, mimi ni kijana ambae niseme kuwa ndio naanza kuingia huko kwani umri wangu bado ni mdogo almost 21 years,
mzee wangu alimpa ujauzito mama yangu kijiji flani huko kusini mwa tanzania wakati mzee ndio ameenda kuanza kazi kama askari polisi ila baada ya mda mzee akaamishwa kituo cha kazi na kupelekwa wilayani hvyo wakaama wote lakini baada ya kufika kule maisha yaka change.
mzee inshort akamtimua mother akiwa na ujauzito wangu sikujua sababu ni nini Kwan mama mpaka leo hakuwai kuniambia basi mama akarudi kijijini kwao akawa amenizaa mimi nikawa nimeanza shule pale kijijini nakumbuka bibi yangu alikua karani wa gulio kiufupi alinijari sana nakumbuka alinifundisha kusoma kabla hata sijaanza shule basi nikaanza shule ya msingi nikiwa na umri wa miaka 5 kujua kusoma ndio ilikua sababu kupelekwa shule nikiwa na umri huo, mawasiliano na mzee hatukua nayo kwani tulikua kijijini simu pia ilikua changamoto mpaka nilipofika darasa la 4 ndipo tulipopata namba ya mzee, basi ikawa ananisaidia hivyo hivyo ila mpaka nikiitaji kitu lakini yeye mwenyewe hakuwa anajali sana kuhusu mimi kwani kule alikua ameshaoa na alikua na mtoto basi nakumbuka wakati nipo Darasa la 7 mzee aka sema kuwa nikimaliza tu inabidi niende mjini kule wilayani niaanze tuition,
hapa mwenyewe nilishangaa kwani mzee hakua anajari sana kuhusu maendeleo yangu ya shule.
Kwanza mama akakataa maana ilitakiwa niende kuishi na yule mama mwingne hivyo mama akaogopa labda nitaenda kunyanyaswa kwani wakati huo mbaya zaidi mzee alikua pia kaamishwa kapelekwa wilaya nyingne lakini yule mke alikua bado yupo nae ila walikua wanaishi wilaya tofauti.basi mzee baada ya kumshawishi sana mother wangu akawa amekubali, nikaenda kuanza masomo ya pre form 1 kiukweli yule mother wa kambo hakua na shida yeyote lie kwani alinijali kama mwanae wa kunizaa.
Basi matokeo ya Darasa la 7 yalipotoka nikawa nimepangiwa shule ya kata ya kule kijijini kwetu mzee alitakata kuniamisha ila sijui ni nini kilimkwamisha basi ikabidi nianze o level nikawa nakomaa kule kila ikifika likizo naenda kule wilayani kupiga tuition hapa kiukweli mzee alikua ananijali sana mpaka mwenyewe nikawa nashangaa maana ilikua tofauti basi nikamaliza o level nikaenda kusikilizia result kwa mzee matokeo yakatoka nikawa nimefahulu sikuamini kwani ile shule inamatokeo mabaya mpaka leo hii nilipigiwa simu nyingi sana ile siku kutoka kijijini na waalimu wangu, selection za kwenda advance zikatoka nikachaguliwa huko mkoani kigoma.
mzee alikua traffic sasa hela ikawa sio ishu basi nikaanza form 5 wakati yule mdogo wangu wa mother mwingne anasoma tusiime ni shule ambayo kiufupi ada yao ni kubwa maisha yakaenda vizuri tu sasa changamoto na kiini cha tatizo ni pale nilipoanza tu kidato cha 6 aisee kwanza baada ya jamaa kuingia madarakani mzee akaamishwa kitengo sijui alifanya mishe gani basi kitengo chap traffic akatolewa na kuamishwa kituo cha kazi hapo ndipo mimi na yule dogo tu kanza kuonja joto la jiwe ikawa dogo kule hatumiwi ada ikafika hatua mother mwenyewe inabidi apambane na wakati huo mimi nishamaliza advance na nishapangiwa chuo sasa ikafika wakati wa kwenda kureport chuo mzee anarudi tungi kalewa nikimuulizia maswala ya mimi kwenda chuo hajali pombe na yeye yeye na pombe basi ikafika wakati ambao naitajika chuo na mimi nikawa kama nishakata Tamaaa ya kwenda chuo yule dogo kule akarudishwa shule kisa ada sasa tuna baba yetu mdogo ambae ni mdogo wake na baba yangu akawa amepata zile taarifa akaamua achukue hela akaenda kulipa kule shule ili mdogo wangu arudi shule basi na mimi akanitumia nauli ili niende kwake mimi nikaondoka nakumbuka niliondoka asubuhi sana mzee akawa bado kalala huku bado pombe haijamtoka nilimuaga hivyo hivyo nikabeba bag langu mpaka kwa baba mdogo kiufupi huyu anamoyo moyo sana na pia yeye hela kwake sio tatizo kwani ni mtu mkubwa tu serikalini. Akanilipia kila kitu mimi nikaanza chuo, nakumbuka mzee was hakukisumbua kunitafuta basi ikapita kama miezi 3 akanambia kuwa anaondoka ameitwa kikazi kigoma, sasa kumbe hakuna mtu alieye kamwambia zaidi yangu hata mama yake pia hakumwambia,
sasa siku Zika pita hakawa hapitikani wakaniuliza me nilishangaa kwani bilingual kuwa ndugu zake kawapa taarifa. Basi hakupatikan tena mpaka mimi nikawa naenda kulizia kule kituoni kwao wakanambia kuwa nisijali kuwa yeye anaendelea vizuri sasa dogo kule shule akawa anasoma katika mazingira magumu father mdogo akawa anaclear kila kitu kuhusu ada mzee yeye ikiwa nikimpigia cm hapokei mpaka mda mwingne anaamua kufunga akiona namba, na walipangiwa huko mwaka mzima sasa kuna askari ambae nafamiana nae week nikawa nime mtafuta ili mijue kuhusu mzee kama atakua karudi kwanza yeye mwenyewe akanshangaa akaniuuliza kwani hajakutafuta.
ndio astaajabu sana aka sema yeye mbona karudi na mwezi sasa unapita toka arudi daaah hapa ndio nilichoka kabisa, nikawaza inamaana mzee hajali kuhus familia yake maana yule mother wa kule bado yeye karudi hajataka kujua aliowaacha wanendeleaje kakaa tu kimya hata mama yake(nini yangu) ananiuliza kumbe pia hajamtafuta kiufupi kabadilisha na namba hatki usumbufu, mwaka mzima kama mzazi hujui watoto wanaendeleje umerudi safari zako bado pia hutaki kujua taarifa zao naona kabisa mzee anaanza kutumezesha sumu polepole ya Kuanza kuto kumpenda, mimi hapa nilipo sina shida sna na hela kwani hela napata japo na umri mdogo kiufupi naishi maisha yangu mwenyewe ila nasiktika napoona mzee kama hajali kuhusu sisi pamoja na ndugu zake ushauri wangu jamani nyie baba zetu hata kama hamna chochote mkituonesha upendo sisi watoto wenu na sisi tunakua tunafuraha na tunajiamini kuwa baba yupo. Kama unachochote cha kunishauri ili baba yangu arudi kama mwanzo karbu kwani hilo ndio lengo kuu siitaji baba yangu apotee.