Naomba ushauri kuhusu muonekano huu wa Nyanya

wa hapa hapa

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
281
150
Habari za zenu wadau. Nina Bustani yangu ya Nyanya ambayo sasa hivi miche ishaanza kutoa matunda lakini tatizo nililokutana nalo ni kwa baadhi ya matunda kuwa na hali kama ya kuoza au kuungua chini ya Tunda.

Swali ni kwamba ni kitu gani husababisha hali hiyo kutokea na nini Tiba yake

IMG_20211017_085140_961.jpg
 
View attachment 1978208
Zipatie maji ya kutosha mkuu. Mara nyingine upungufu wa maji husababisha hiyo Hali.
 
Kama ni kwenye kitako Cha nyanya Basi tambua kuwa unamwagilia maji Wakati ardhi Ni ya Moto,sasa ukimwaga Yale maji hutoa mvuke wenye joto ambao huunguza nyanya kwenye kitako chake.

Ushauri,jaribu kutandaza nyasi shambani ili kutunza unyevu nyevu lakini pia zitasaidia ardhi usipate joto kupita kiasi.

Kitu kingine jaribu kumwagilia maji Wakati ambao ardhi itakuwa imepoa ili kupunguza mvuke ambao huwa na joto.
 
Ugonjwa huu unaitwa “Blossom-end Rot” ni ugonjwa ambao tunaiweka katika kundi la fiziolojia ambapo husababishwa na kutokuwa na uwiano sawa wa madini ya calcium na nitrogen katika udongo ambapo mara nyingi hutokea kwenye udongo ambao hauna unyevu-unyevu wa kutosha.

Kuondoa tatizo hilo jaribu kufanya mambo yafuatayo;

- Hakikisha udongo wako unapata maji ya kutosha pale tunda linapoanza kutengenezwa

- Nyunyizia mmea kirutubisho aina cha calcium chloride

- Ipate mimea yako ya nyanya mbolea ya maji mfano “ EASY-GRO CALCI” na hali hiyo haitotokea tena.
 
Hiyo inaitwa Blossom End Rot au kuoza kwa kitako hii husababishwa na umwangiliaji wa maji usio na mpangilio mzuri au ukosefu wa madina ya calcium kwenye udongo suluhisho uwe na mpangilio mzuri wa umwangiliaji maji pia tumia mbolea zenye calcium
Mtaalamu wa kilimo thumb up 🤞🏾
 
Nashukuru sana kiongozi japo nimechelewa kuutambua mchango wako.
Be blessed mkuu.
 
Hiyo inaitwa Blossom End Rot au kuoza kwa kitako hii husababishwa na umwangiliaji wa maji usio na mpangilio mzuri au ukosefu wa madina ya calcium kwenye udongo suluhisho uwe na mpangilio mzuri wa umwangiliaji maji pia tumia mbolea zenye calcium
Samahani mkuu, mpangilio bora wa Maji ukoje coz namwagilia mara 2 kwa wiki na unyevu upo wa kutosha.
NB:Hii ni mara yangu ya Kwanza kulima Nyanya, napenda kupata uzoefu kutoka kwa wenye uzoefu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom