Naomba ushauri kuhusu mfuko wa kijamii wa kujiunga

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
661
Ndugu habari za leo? Mimi ni mzima wa afya, naomba mnishauri nijiunge na mfuko gani wa kijamii kwa manufaa ya baadae? Ninapata mkanganyiko maana kila mmoja anavutia kwake, na hivyo nimeona nije humu mnishauri kutokana na uzoefu wenu ili nifanye chaguo lililo bora zaidi.

Nisingependa wanaojihusisha na kutangazia mifuko hiyo (PSPF, LAPF, GEPF, NSSF etc) kuweka kampeni hapa, bali wale watumiaji wa mifuko hiyo pekee.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yangu ya baadae. Asanteni sana.
 
Wote siku hizi wanatumia formula moja kukokotoa mafao ila nawakubari PSPF maana kidogo sio wasumbufu sana kwenye kukupa mpunga wako
 
Ndugu habari za leo? Mimi ni mzima wa afya, naomba mnishauri nijiunge na mfuko gani wa kijamii kwa manufaa ya baadae? Ninapata mkanganyiko maana kila mmoja anavutia kwake, na hivyo nimeona nije humu mnishauri kutokana na uzoefu wenu ili nifanye chaguo lililo bora zaidi.

Nisingependa wanaojihusisha na kutangazia mifuko hiyo (PSPF, LAPF, GEPF, NSSF etc) kuweka kampeni hapa, bali wale watumiaji wa mifuko hiyo pekee.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yangu ya baadae. Asanteni sana.
Hakuna mwenye unafuu hapo wote wana tabia sawa sema wamejificha kwenye koti la majina tofautitofauti!
 
Dogo inaonekana umemaliza chuo mwaka jana na hii ni formal ajira yako ya kwanza.
Huna knowledge yoyote ya hii mifuko.

Chukua LAPF kijana. Hizo zingine hata usijaribu kuziwaza. Utajuta.

PPF utajuta.
NSSF wajinga tuu..
PSPF hamna kitu.
GEPF hamna tuu
..
Dogo kakataza madalali wa mfuko wowote kutoa ushauri au hujasoma vizuri?
 
Dogo inaonekana umemaliza chuo mwaka jana na hii ni formal ajira yako ya kwanza.
Huna knowledge yoyote ya hii mifuko.

Chukua LAPF kijana. Hizo zingine hata usijaribu kuziwaza. Utajuta.

PPF utajuta.
NSSF wajinga tuu..
PSPF hamna kitu.
GEPF hamna tuu
..
asante kwa ushauri wako, nadhani "Chukua LAPF kijana" ingetosha
 
LAPF ndo habari ya mjini. Ina faida nyingi... kuna mafao mpaka basi. Mwanzoni nilidhani utani... mwaka jana mke wangu kajifungua kapewa mpunga wa uzazi kama 1m hivi kimasiara naangalia.
Pia hawana longolongo kama wengine kwenye mafao.... kuna wengine wanahitaji nyaraka nyingi ukistaafu utadhani unaiba. Ni fasta
 
asante kwa ushauri
 
Ndugu habari za leo? Mimi ni mzima wa afya, naomba mnishauri nijiunge na mfuko gani wa kijamii kwa manufaa ya baadae? Ninapata mkanganyiko maana kila mmoja anavutia kwake, na hivyo nimeona nije humu mnishauri kutokana na uzoefu wenu ili nifanye chaguo lililo bora zaidi.

Nisingependa wanaojihusisha na kutangazia mifuko hiyo (PSPF, LAPF, GEPF, NSSF etc) kuweka kampeni hapa, bali wale watumiaji wa mifuko hiyo pekee.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yangu ya baadae. Asanteni sana.
LAPF, itakufaa
 
PSPF ni mfuko uliofilisika,ukistaafu leo unaweza kulipwa mafao baada ya miezi kumi na mbili mpaka mwaka na nusu,usidanganywe,usigeuke nyuma,nenda LAPF,siku moja kabla ya kustaafu wanakupigia simu wenyewe tena bila wewe kuwapa vocha,wanakupigia simu kukwambia HELA YAKO TAYARI.

Ukitaka kupata uhakika kwamba PSPF imekufa,nenda pale ofisi yao kuu posta, utakutana na wazee wametoka vijijini wanafokeana na watumishi pale ground floor,wazee wanadai hela,mtumishi anampiga maneno,wengine mpaka mwaka hawajalipwa

Hebu pata picha umechangia miaka karibu 35 halafu unaishia kupigwa maneno,mfuko umeliwa hauna pesa
 
asante kwa ushauri, ila umepiga kampeni ndani yake. Nilitaka tu utoe ushauri wako, ingetosha
 
Google uone jinsi wabunge wanavyoilalamikia PSPF,wanasema imefilisika na kuna kipindi zitto kabwe aliitaka serikali iingilie kati.

Usiandikie mate,GOOGLE hapo kwenye simu/laptop
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom