Naomba ushauri kuhusu hili tatizo linalonikabili

Naomba ushauri kuhusu hili tatizo linalonikabili

Siku za assessment tu kwa UDSM sahau labda kwingine. Mimi nina maswali kadhaa ukijibu tutaendelea;
Kwanza : Hela za field aukupata au hamjapewa ?
Pili: Unasoma course gani hapo ?
Tatu: Je umeongea na marafiki zako au hauna marafiki ? Jibu kwanza alafu ntaendelea.
 
Nina mtu anafanya kazi hapo UD, naweza mwagiza akusaidie kama wewe ni genuine, unaweza mwona? lengo ni kuthibitisha kama wewe upo hapo UD na jama una uitaji huo, niwe mkweli tu, maana watu wengi wahuni washawaliza watu humu na hili linasikitisha!
Ukijiridhisha awasiliane nami nitamu assist chochote
 
1.Sina mkopo kabisa
2.Bachelor of Arts with Education
3.Marafiki hawana kitu japo ndio wanaonidai hio laki mbili.
Mmoja anadai Tsh120,000
Mwingine anadai Tsh70,000
Watatu anadai Tsh30,000
Tafuta nauli ukafanye PT kwenu I meant nyumbani kwenu Ili kuepuka gharama na madeni juu ya madeni . Zingatia itakusaidia.
 
Kwanini ujipe shida zaid,kama kuna uwezekano kafanyie kwenu au kwa Ndugu unae elewana nae au huna rafiki ukakae kwake then unaenda field?kama yupo Rafik mweleze hali halisi,na istoshe ndo utakapojua kipimo cha urafik wenu
 
dah pole saana ndugu nayo hayo huwakuta weng kwa wanawake ndo uwa simple maana ujiuza

namn humu wapo wenye roho zao utapata msaaada
 
Pole sana mkuu, ningekuwa vizuri ningekupa ASSIST..Usikate tamaa mambo yatakaa sawa
 
Nafanyia hapa hapa Dar Es Salaam
Daaaah hapo sina ujanja
Mie nko Mbeya,tukuyu kama ingekua huku ninge provide chakula na malazi,pia Dar nyumba ipo but ime pangishwa yote
Kama ingekua Mbeya kuna shule ipo karibu na nnapo kaa ninge kutafutia hapo then ungeishi kwangu bila shaka unge maliza field yako vizuri,but kwa Dar sina ujanja
 
Aseh we jamaa pole sana! Ina maana hauna ndugu wa kukusaidia kabisa?
Anyway, ningekuwa na uwezo wa kukusaidia ningefanya hivyo. Ulitakiwa uombe msaada humu kabla ya kuchagua kituo cha field, kwa mfano kuna jamaa yuko mbeya kasema yuko tayari ukakae kwake, lakn kwa kuwa kituo ushapangwa inakuwa ngumu..
 
ushauri wangu,hata mimi ni mwanachuo UOA mwaka wa kwanza nafanya BBA WITH EDUCATION kitu cha kwanza unachoambiwa ni kufanyia TP mazingira ya kwenu kwa ajili ya kukusaidia wewe kuwa na ufanisi zaidi.make hapo ulipo naimani hata nauli,hela ya kula na mahitaji mengine ni tatizo.wakati mwingine acheni kufanya mambo kwa mkumbo.mtu hujikuna pale mkono unapofikia
 
Nauli ni Tsh50,000 kwenda tu.
Halafu kuna nyumba tu hakuna mtu labda kwa ndugu.
Ni gharama zaidi kuliko kubaki Hostel na kufanya field jirani na Hostel za chuo.
Mfumo wa Aris umefungwa tayari siwezi kuedit kituo.
Mpaka mfumo unafunga ulikua wapi?,au ulitegemea za kuomba kama hivi au ulikua na option nyingine ndio imeingia mitini?
 
Back
Top Bottom