Naomba ushauri kuhusu changamoto hii niliyonayo kwenye biashara yangu ya kitimoto

bad spenko

Senior Member
Jun 22, 2020
125
137
Niende moja kwa moja kwenye point kama heading inavyojieleza.

Lengo la hii thread ni kuomba wajuzi wa hii biashara tushauriane. Nimeanzisha biashara ya kuuza kitimoto Dar maeneo ya Kibamba njia ya kwenda Muhimbili MUHAS.

Wakati naanzisha nilikua na kijana ambaye ni mzoefu wa hii kazi ya kuitengeneza lakini cha ajabu kijana niliekua nae baada ya wiki moja akaanza kulewa ovyo na kucheza betting nilipopata taarifa nikamkalisha chini abadilike lakini baada ya siku mbili alimwachia mtu funguo ili aendelee yeye simu akawa hapokei wala nini.

Nikaamua nimwache nibaki na huyu alieniletea lakini changamoto za huyu ni mchafu wa mavazi ila kazi anaiweza lakini sasa baadhi ya wateja wangu wananishauri kua huyu jamaa hakufai mazingira yake na huduma anayotoa atakupotezea wateja.

Sasa kuna dada nimempata na kazi anaiweza ila sasa nashindwa nitamsimamisha vipi ili nimwingize huyu dada napata wakati mgumu na mimi binafsi nafanya shughuli nyingine ya kuajiriwa kwa hiyo mda mwingi nakua sipo kwenye biashara yangu zaidi ni kwamba naenda jioni kwa jioni napiga hesabu zangu naondoka mda ninaokaa hapo ni mchache kama masaa 3 ivi.

Naomba kujuzwa au ushauri juu ya maelezo hapo juu wajuzi tafadhali. Nina hasira sana na maisha ya kujikwamua kwenye hali niliyonayo kwa sasa ina kama mwezi 1.

Msaada kwenu wakuu bado mi dogo janja nina 23 years. Nashindwa kuchukua maamuzi sahihi ya yupi nimweke hapo.

NAWASILISHA.
 
Kosa ulilofanya ni kumuweka huyo dogo wa pili kienyeji bila kumpa target wala masharti yoyote. Kwa sasa huna namna zaidi ya kumpiga chini kama ushamuonya na hakuna mabadiliko.

Sisi waTz upole wetu na kuchekacheka na wafanyakazi ndio unatucost sana
 
Kama biashara inalipa huyo mchafu unaweza kumpa majukumu mengine ila pia kumsisitiza abadilike awe msafi.

Nimeshauri hivyo kwasababu wafanyakazi wengi wakike hawaeleweki ukiwa unafanya kazi na mtoto wakike lazima uwe nambadala maana akipata bwana akienda kupigwa miti usiku mzima usitegemee kama kesho atakuja kazini lazima apumzike hiyo siku. Naongea kwauzoefu
 
Huwapi jobu disikripsheni mkuu,bailoozii na gaidilaini za kazi,lazima wakusumbue......daah usingetaja huyo mdudu ona usiku wote huu naanza kutamani
 
Kama mzunguko wa pesa ni mkubwa muajiri huyo dada ukimwambia ndio atahusika na kuserve kwa wateja wakat huyo kijana abakie jikoni tu.

Kama biashara ya kawaida mnunulie uniform za kazi kijana wako pea 2 then mwambie ukwel wateja wanalalamika hauko smart so sitegemei nikakukuta mchafu nikija vingnevyo mkataba utaisha.

NB: Yule kijana wa kwanza baada muda atarud tu kuomba hyo kazi.
 
Back
Top Bottom